Kusamahe: Kuna mengine huwa hayasameheki?

Kusamahe: Kuna mengine huwa hayasameheki?

KIKUNGU

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
845
Reaction score
587
Padre alihubiri huwezi kutubu dhambi zako kama wewe mwenyewe hujasamehe waliokutenda/kuumiza kwa kutokutubu dhambi zako unakuwa umejenga ukuta na mungu wako kwa kuwa na dhambi unakuwa umemuasi mungu wako kwa kuishi kwako katika dhambi kuna-invite majanga mengi katika maisha yako personally.

Majanga hayo yaweza kuwa magonjwa,umasikini,failures,mikosi Lakini hata katika kuishi kwako ukiwa si mwenye dhambi yaani kwa kuishi ukiwa hujavunja amri zote kumi za mungu bado dhambi zilizotendwa na generation nne za nyuma yako bado zinaweza kutesa, muulize baba yako au wazee kama kuna madhabahu walizo abudu huko nyuma Haya yalikuwa maudhui ya somo la leo.

Niko kwenye mid forties,nimelelewa kwenye ukatoliki sawia,natimiza wajibu wangu kama mkatoliki,natenda dhambi ndio, nawajibika kutubu na huwa natubu.Kwa mara ya kwanza leo katika maisha yangu ya dini nimekutana na mahubiri hayo hapo, padre alikuwa anaquote vitabu tofauti kusupport his arguments.Nimemkubali na nimekubali kitu ambacho for the last few years nilikuwa sijalikubali kusamehe

My ex alinitenda kutendwa ambako namshukuru mungu alinipa ujasiri wa kutokulipiza kisasi,for a year nilienda kukabidhi silaha polisi kwa sababu shetani alikuwa ananiteka,ningeweza kufanya kitu kibaya.

Nilimwacha mke wangu,nili-move on, sikuwahi kumsamehe ila nilikwa najaribu kusahau.Kila nilipofikiria kile alichonifanyia tumbo lilikuwa linatetemeka. Baada ya mahubiri ya leo nilipata muda wa kutubu,nimemsamehe my ex,kutoka moyoni.

Our divorce was one of the messiest divorce ambazo huwezi kufikiria,yaani hata arrangements za kuwaona watoto,kulipia school fees ni through our solicitors.Nimempigia simu leo my lawyer ili aweke appointment na lawyer wa my ex ili waweze kutukutanisha nimwambie kwamba nimemsamehe kama ambavyo nimetubu leo kanisani.

Wana MMU naomba tushare hii topic ya KUSAMEHE. Je umashatendwa/umizwa kiasi cha kushindwa kusamehe?Sio kuumizwa kwenye ndoa/mapenzi tu,hapana hata maisha ya kawaida,ulidhulumiwa na mtu/watu,kuna mtu/watu walikatisha ndoto zako za maisha.

Yaani yale mambo mabaya uliyofanyiwa na mtu/watu kiasi ukikumbuka au ukimuona mtu/watu waliokutenda unasikia moyo kukuenda mbio au tumbo kukuuma.

Je uliwasamehe/utawasamehe?.Bila kusameheana tutakuwa tunajenga kweli taifa lenye maadili na lenye kumpendeza mungu kuazia kwenye familia au mtu mmoja mmoja au familia na familia?

cc @Kaunga The Boss Karucee snowhite Sikonge Kongosho
 
Good for you....kusamehe ingawa ni kuzuri sio kila mtu yuko gifted na a big heart to forgive....kutokusamehe kunatokana na kuwa na a very poor in your heart....na kujiona uko perfect au kujiona entitled...
 
Yani mi mtu akiniuzi kabla hata hajaniomba msamaha huwa nasamehe mapema hata kama kosa gani kuna mtu alinitapeli niliumia na ghafla nikamsamehe so forgiving is the best thing to me haitajalisha kosa gani
 
kusamehe ama kutosamehe inategemea sana.

Kuna wengine unawasamehe sababu wame-earn forgiveness, kuna wengine unawasamehe sababu ni wa muhimu kwako, kuna wengine unaona ni karaha tu.
 
Good for you....kusamehe ingawa ni kuzuri sio kila mtu yuko gifted na a big heart to forgive....kutokusamehe kunatokana na kuwa na a very poor in your heart....na kujiona uko perfect au kujiona entitled...

You are right The Boss,nilishindwa kusamehe for the last four years lakini leo nafikiri mungu alimtumia mtumishi wake kunifikishia message kwani padre from nowhere alikuja simama nilipokuwa nimekaa na aliniuliza swali kama nimeshawahi kusamehe ili hali ndio siku ya kwanza kwenda kwenye hili kanisa ughaibuni.You needs a big heart to forgive,yes
 
kusamehe ni jambo la busara sana na kila mtu anataman kusamehe. Tatizo ni kwamba ni watu wachache sana wenye huu ujasili. Tendo hili linaitaji ushujaa, ujasili na ukomavu zaidi kulifanya. Ee Mungu tunaomba utujalie moyo wa kusamee
 
Yani mi mtu akiniuzi kabla hata hajaniomba msamaha huwa nasamehe mapema hata kama kosa gani kuna mtu alinitapeli niliumia na ghafla nikamsamehe so forgiving is the best thing to me haitajalisha kosa gani

Una big heart,Pricess Sayuni according to The Boss.
 
Una big heart,Pricess Sayuni according to The Boss.

Ni kweli mkuu forgiveness kwangu ni kitu cha muhimu sana hata kama ni kosa gani nalichukulia kwa pande zote na uzito.wake kwa kutoa msamaha na forgive and forget then life goes on without any problem
 
Namshukuru Mungu sana coz am grown up now na nimejifunza kusamehe na kujisamehe mimi mwenyewe. Hapo mwanzo nilikuwa mtu wa kukaa na vinyongo moyoni pale inapotokea nimeumizwa na mtu wa karibu yangu. Nilikuwa siwezi kumwambia mtu eti labda fulani umenikosea. Ilikuwa mtu akinikosea, ntalala kitandani kwangu ntalia weee, nikimaliza kulia ndo uhusiano na huyo aliyeniumiza unaishia hapo. Sitojihusisha na huyo mtu kwa njia yoyote ile.
Inatesa kwa kweli kukaa na kitu moyoni na unaweza ukawa unazuia pia baraka zako kwa njia hiyo. Tujifunze kusamehe na kujisamehe sisi wenyewe.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kama hii dhambi itanipeleka moton acha niende tu......
[MENTION=22799]@ladyinaction nimesoma comments zako kwenye uzi flani, ulisema that guy aliekuumiza hutomsamehe tena!!

Same comment kwenye uzi huu, ushauri wangu, Omba upate ujasiri na moyo wa kusahem, utashikilia huyo mtu mpaka wapi dada yangu?

Huna sehem yeyote ya kumpeleka msaheme tu, angalia kisa kama hicho kilimchomtokea huyo Mkuu, ukweli ni kwamba inatubid tusamehe tu. yan kwa vyevyote vile, I have a story nikisema hutokaa uamini. Lakini wapi, you forgive na maisha yanaendelea.

Kama una amini katika Mungu na akusaidie uweze kuruka kizingiti hiki.

Ubarikiwe.
 
KIKUNGU jifunze haya...yatakusaidia..

ukisamehe haina maana umekubali kilichotokea kuwa na sahihi
kusamehe sometimes ni ku let go.....
kusamehe pia ni kujisamehe wewe mwenyewe

sababu mahusiano yaki collapse haliwezi kuwa kosa la mtu mmoja 100 percent

mahusiano ya wawili yaki collapse basi wote kwa namna moja au nyingine mmechangia kufika hapo

hata kile kitendo cha wewe kuingia tu kwenye mahusiano na mtu huyo ni 'kosa' lako pia..
ambalo unapaswa kujisamehe na kumsamehe ,mwenzio...

halafu love inapaswa kuwa free...usiwe unatazama uliyomfanyia kama vile alipaswa kukushukuru au kuyathamini,,
yote uliyomfanyia uliyafanya kwa sababu ya love in your heart.....na sio necessary ya love uliyopewa...

to love is to give.....so ulimpenda na uliyafanya yote........hupaswi kugeuza deni au kudai 'kushukuriwa'
 
Last edited by a moderator:
Kusamehe siwezi........
Kuna mtu alinikosea sana cku nikimsamehe basi sumu itahusika
 
na labda swali kwa mtoa mada, kisamehe kunajumuisha kurudiana na mkewe?

Hata kama si kurudiana lakini.mawasiliano ya mara kwa mara?

Ha ha ha ha wewe Kongosho wewe,no i have moved on.Mawasiliano ya mara kwa mara hasa issues za watoto
 
Kusamehe siwezi........
Kuna mtu alinikosea sana cku nikimsamehe basi sumu itahusika

Tinna cute,acknowledge uwepo wa mungu,je na wewe usisamehewe hata na mungu wako pia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom