Kusajili laini za simu mtaani ni hatari, hatari kabisa

marcs

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
1,066
573
Nimeamua kuwatahadharisha wana jf na watanzania wote kwa ujumla kuwa kuna wizi ktk mawakala wanaosajili laini za simu mtaani kuwa ni wezi.
7e15f90e58b8347e8655931685b57d01.jpg


Ilikuwa tarehe 10/08/2016 mwaka jana saa 5 mchana kulitokea vijana watatu wakisajili laini za cm mtaani eneo la kigamboni Dar wakitoka kampuni moja ya cm yenye kulalamikiwa sana na wateja wao

Vijana hao walidai kusajili laini za chuo walinivutia sana kwa maneno yao nikawapa cm yangu yenye laini mbili moja nikaitoa ikabakia moja ktk cm wale vijana walikaa masaa mawili wakidai network inasumbua

Kumbe wale jamaa waliingiza namba zao wazijuazo hatimaye wakahamisha laki 800000 kutoka akaunt yangu ya cm halafu wakaifunga line kila mtu akinipigia anaambiwa cm uliyoipigia imefungiwa

Baada ya kugundua tatizo hilo nikawapigia huduma kwa wateja kwa kutimia cm nyingine wakaniambia kuna watu wamechezea cm yako kulikuwa kumepita sku mbili nikitumia cm yingine

Baada ya kuwapigia huduma kwa wateja wakanielekeza jinsi ya kuifungua ndo nikagutuka sasa kwamba watakuwa wale vijana waliokuwa wakisajili laini ikabid fasta kuangalia salio la akaunt yangu ktk cm

Haikusoma nikapiga tena huduma kwa wateja wakasema hauna salio la kutosha hivyo akaunti yako haiwezi kusoma nilishangaa sana nilikuwa na 800000 halafu isisome yule mhudumu nikamwomba anitazamie salio akasema nina tsh 50 tu

Nikaamua kufungua kesi kituo cha polsi kigamboni kesi yangu ikipelelezwa na afande Edgar alianza kufatilia zile pesa zimerushwa kwa nani lakini kampuni ya cm huska haikutoa ushirikiano wakawa wanapiga chenga namba zilianza na 07*******

Nilisumbuka miez miwili lakini siku moja nipo kkoo nikawaona wale vijana wakiwa wote wawl wakakimbia wKiwa na jezi zao lakini mmoja nikamkamata nikamwambia ukikimbia nitakuitia mwizi yule kijana hakukimbia nikamleta hadi kituo cha kigamboni kwa tx

Akatiwa ndanilakini alikaa wiki nzima lakini wale ndugu zake walikuja kumlipia ile pesa baada ya yeye kukiri kosa wizi kwa njia ya mtandao wakalipa ile pesa yote

Lakini yule mwizi alipokuwa anataka kutoka kuondoa afandr mmoja kasema kunajamaa mwingine katoka chang'ombe polisi kapigwa 3,000,000 kwa hiyo yule mwizi hatakiwi kuondoka afande yule kasema jamaa alieibiwa kaja hapa kituoni akiwa na picha ya huyu kijana kwenye cm

Kwa hiyo yule kijana hakuondoka akaanzwa kuuliza na polisi mnafanyaje mpaka mnachukuwa pesa bila kuna na namba za siri? Yule kijana akasema wao ni wafanyakazi wa kampuni ya cm kuna namba wakiingiza namba ya siri inaonekana ma wanahamisha pesa kiurahisi

Kwa hiyo mie nililipwa pesa yangu yule kijana akapelekwa chang'ombe kujibu shitaka la 3,000,000 wizi kwa njia ya mtandao tena yule kijana alidai kuwa hata kwa wale waliounganisha akaunt ya cm kwenda benk wanaiba pia kwa hiyo kuna wafanyakazi wa makampuni ya cm wasio waaminifu

1 ilikuaje wakajua kuwa akaunti ya ina tsh 50 kwa hapo tu nikajua kwamba pesa kwenye akaunt za cm c salama hata benk pia hutia namba za siri tu nakuiba. wana jf nimeamua kuwapa uzi huu mwaka huu mwe waangalifu na hawa vijana wa mtaani ni cpendi hata kuwaona walitesa familia yangu hadi watoto walikwamwa kwenda shule.

Be ware
 
Nimeamua kuwatahadharisha wana jf na watanzania wote kwa ujumla kuwa kuna wizi ktk mawakala wanaosajili laini za simu mtaani kuwa ni wezi.

Ilikuwa tarehe 10/08/2016 mwaka jana saa 5 mchana kulitokea vijana watatu wakisajili laini za cm

Safi sana ndo tanzania ya viwanda
 
Ukisajili lain ya simu mpesa au tigo pesa au airtel money wakufungulie wao kisha baadae badili password ila usiweke tarehe au mwaka wako wa kuzaliwa. Weka password nyingine kabisa utakua salama.
 
Nimeamua kuwatahadharisha wana jf na watanzania wote kwa ujumla kuwa kuna wizi ktk mawakala wanaosajili laini za simu mtaani kuwa ni wezi.

Ilikuwa tarehe 10/08/2016 mwaka jana saa 5 mchana kulitokea vijana watatu wakisajili laini za cm
Umefumaniwa nini mkuu?
 
Back
Top Bottom