Napika,nasafisha nyumba na kupiga pasi bado unaniita mkoloni ?Kumbe na wewe ni mkoloni ehh?Mbona ndoa yako itakua na kazi!Labda ukaoe kijijini!
Napika,nasafisha nyumba na kupiga pasi bado unaniita mkoloni ?
Bado hubebi mtoto mgongoni unamwachia tu yeye mwenyewe.
Asante LD!!Uporoto swali la kuchagua kazi ndo tatizo!Kama unampenda kweli mwenzako sidhani kama vitu vidogo hivi vinaweza kua ishu!
Ila ujue lizzy hii ndo sababu kubwa ya ndoa nyingi za siku hizi kutodumu.Wanaume tumekuwa na akili sijui za namna gani?Yaani eti ili uonekane dume la maana ukishaoa ukitoka tu kazini unatakiwa upitie nyumbani halafu ukishasalimia uhamie baa na marafiki mpate moja mbili mpaka chakula kiive home ndo urudishe tumbo zako ule wakati huohuo mkeo kashajichokea ka punda kalala zake na bado unamsumbua ukishashiba unataka mzigo.Hiyo ni roho ya ubinafsi na ni ukandamizaji wa kijinsia.Wanawake mko wapi kwa hili?kimichio ningekugongea thanks sema niko via m!asante kwakutokua na akili mgando!
LD kwa maelezo yako nimekuelewa ila kazi bado tunayo mimi na wewe maana vijana wa kileo hii dhana imewakaa sana ila tukaze buti.hapa ndipo pale ninaposemaga hakuna mke/mume asiye mwema ila ni mwema kwa nani?? Kwani anaweza asiwe mwema kwako lakini kuna mtu mwingine angeishi naye angekuwa mwema sana na kila siku angekuwa anamshukuru mungu.
Kama hicho tu cha kupika, kumbeba mtoto mtu anaweza kuona ni kitu kibaya tena kibaya sana, huyu sio mume kwangu.
Hicho cha kuwaonea washikaji zako aibu wakati unanisaidia shughuli za nyumbani, wala hutaki wajue inamaana hawana hata cha kujifunza ktk hilo, huyo sio mume mwema kwangu.
Kama hayo mambo utafanya tu kwa sababu naumwa, yani ugonjwa tu, wala huna mapenzi ya kunisaidia hivo vishughuli tayari we sio mume kwangu. Basi nikitaka kusaidiwa siku hiyo najifanya kichwa kinauma nameza panado nalala.
Sikulazimishi wala sikuambii nisaidie. Lakini ndo ntakuwa naumia tu ndani kwa ndani.
Bado hubebi mtoto mgongoni unamwachia tu yeye mwenyewe.
Asante LD!!Uporoto swali la kuchagua kazi ndo tatizo!Kama unampenda kweli mwenzako sidhani kama vitu vidogo hivi vinaweza kua ishu!
Kubeba`mtoto mgongoni au kuosha vyombo/nguo mtanisamehe kinadada,naweza cheza na mtoto kumuogesha/kumlaza lakini mgongoni HAPANA!
LD kwa maelezo yako nimekuelewa ila kazi bado tunayo mimi na wewe maana vijana wa kileo hii dhana imewakaa sana ila tukaze buti.
Tusisahau wengine hufanya shughuli fulani ziziotarajiwa na jamii kwa sababu ya limbwata.
Weeh! temea mate chini hahaha! labda nimbebe mamii kumpeleka chumbani lol!Hahahahahahahahaha kama nakuona umebeba mtoto mgongoni
Weeh! temea mate chini hahaha! labda nimbebe mamii kumpeleka chumbani lol!
Ila ujue lizzy hii ndo sababu kubwa ya ndoa nyingi za siku hizi kutodumu.Wanaume tumekuwa na akili sijui za namna gani?Yaani eti ili uonekane dume la maana ukishaoa ukitoka tu kazini unatakiwa upitie nyumbani halafu ukishasalimia uhamie baa na marafiki mpate moja mbili mpaka chakula kiive home ndo urudishe tumbo zako ule wakati huohuo mkeo kashajichokea ka punda kalala zake na bado unamsumbua ukishashiba unataka mzigo.Hiyo ni roho ya ubinafsi na ni ukandamizaji wa kijinsia.Wanawake mko wapi kwa hili?
Kila mtu ana sehemu kachora mstari kwamba hapa mi hapana sasa mimi mstari wangu huo sivuki hapo najuwa nikikubali hilo linafata 'leo natoka na rafiki zangu usiku kaa na mtoto'.Atiiii kama unaweza mtu mwenye 50kg washindwa nn katoto kako kenye 10kg tu. Acha bana!!