Peleka pale Msamvu, Mabasi yote ya dar yanasafirisha;
Abood, BM, nk Ile buti ya kule nyuma ni kubwa sana Godoro halifiki hata robo. Sina hakika na bei ila wanaweza kukuchaji hapo kama shs 30,000. Ila komaa nao kwani bei zinaongeleka....
Mtu kusafiri toka Moro mpaka Dar nauli ni moja kwa abiria wote, kitanda na godoro gharama hutokana na ukubwa na uzito, hivyo jibu si rahisi kutoka kwangu.
Hata hivyo tumia basi linalofika eneo unakoishi mfano Mbagala na Gongo la Mboto, malori utapata gharama za ziada kutoka Jangwani yanakoishia kwenda kwako.