Kuruka doz kuna madhara?Msaada tafadhali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuruka doz kuna madhara?Msaada tafadhali.

Discussion in 'JF Doctor' started by tizo1, Dec 20, 2011.

 1. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Jaman madaktar habar.Nimeruka dozi 1 ya quinene .je kuna madhara gani?ina maana nianze upya?nipo siku ya tatu na nimesahau kumeza leo mchana.MSAADA TAFADHALI
   
 2. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Msaada tafadhari.....
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Tizo, pole na kuumwa.
  Dozi ya dawa inapangwa baada ya utafiti wa kina kuangalia minimum concentration ya dawa kwenye mwili inayoweza kuendeleza mapambano na ugonjwa na maximum ambayo itapambana bila kuleta madhara makubwa zaidi kwa mwili. Kama umeruka dozi unashauriwa kutumia dawa mara unapokumbuka na kuangalia muda uliobaki kwa ajili ya dozi inayofuatia. Kama upo karibu sana ni bora kuruka. Otherwise,ni muhimu kuchukua namba ya simu ya daktari ili uweze kuwasiliana juu ya maswali ya papo kwa hapo.
   
 4. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sio vizuri kuruka dozi au kukatisha kutumia dawa hasa kwa hizi dawa zinazotibu malaria,antibiotcs,antiprotozoals etc.unaposahau kutumia dawa hizo unasababisha wadudu ambao tayari wanakuwa wameshaanza kudhoofishwa na dawa wafufuke upya na mara nyingi hurudi kwa nguvu zaidi ya mwanzo na wengine huwa sugu.


  Lkn kwa vile imeshatokea bahati mbaya basi wewe endelea na dawa kama kawaida ila uwe makini zaidi na usirudie kosa.At least wewe umeonyesha kujali wakati kuna wengine huwa wanakatisha dozi wakifikiri tayari wamepona.Hao wako kwenye hatari kubwa ya kutotibika kirahisi hapo baadaye.
   
 5. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  asante kwa ushauri mzuri....
   
 6. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  asante sana
   
 7. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwakuwa umesahau ukiendelea haina shida ila kama umefanya makusudi jiandae kupelekwa kitandani.
   
 8. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Madhara ya kuruka dozi yako so broad.
  Kabla hatujaangalia issue yako ambayo inshort kwa ushauri wa hapo juu unatosheleza.
  Tunapaswa kujiuliza kuwa kwanini dawa za kutibu magonjwa mengi, mfano malaria
  na magonjwa ya zinaa zinabadilishwa mara kwa mara na bado zinafail ?!
  Sababu mojawapo ni hiyo ya kuruka dose
  na mbaya zaidi kutomaliza dose.
  Unaporuka dose ama kutomaliza dose unawapa nafasi vimelea kupambana kirahisi na dose ndogo iliopo na pengine kuishinda. Mwisho wa mapambano hayo vimelea hivyo vinakuwa vimejifunza jinsi ya kupambana na dawa husika. Bahati mbaya sasa vikihamishiwa kwa mtu mwingine na ku settle,kisha huyo mtu akatumia dawa ileile vitagangamala na kuishinda
  [ si viliishaisoma ilivyo bwana].
  Hapo ndo kinakuja kitu treatment failure ama vimelea sugu.
  ... Ndo mana tulitoka kwenye
  Kloroquine tukaenda SP kisha sasa ALu [ mseto ] kama tiba ya kwanza ya malaria. [Thanx Quinine kama tiba ya pili ya malaria haijafailure toka karne ile].
  Pia kutoka kwenye tetracycline capsule [cjui iko wapi siku hizi,iliaminiwa na kuwa maarufu sana enzi zake hasa huku kwetu vijijini] hadi sasa Ceftriaxone kama tiba
  ya gonorrhea.
  Tatizo ni watu kumeza dose mbili tatu wakipata nafuu na kujiona wamepona wanaacha dozi [SIO TIZO1].
  Jamani tusiwatese wanasayansi
  tuwape nafasi wafikirie kwanza
  matatizo makubwa [ Major Global Issues ] kama HIV / AIDS. Hivi
  vidogo tupambane navyo personally.

  Naogopa sana,mchezo kama huu unaochezwa na baadhi ya watumiaji wa ARVs. Tusije tukarudi
  enzi zile za ukipata HIV ndo basi tena.

  Mkuu Tizo1 ! Pole sana,endelea na dozi tu,lakini hakikisha husahau tena kwa hzo siku zilizosalia.
  Utapona kaka.
   
Loading...