Kuna madhara gani nikiweka ''lamination'' kwenye cheti changu ?

adriz de mbusii

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
16,747
Reaction score
37,588
Moja kwa moja..

Siku za nyuma nilienda Veta kuchukua cheti changu , niliistaajabu baada ya kupewa yule Dada aliyenipa aliniambia nisiweke lamination bila kuniambia sababu.

Naomba kujua wajuzi je , ipi inawezekana kuwa sababu ya kuniambia hivyo na je , Kuna madhara yeyote niliweka ? maana vyeti vyangu vingi vya O_level , Advance , kuzaliwa , best student nk vyote nimewekea lamination.

Na bila lamination sidhani kama nitatoboa kwenye utunzaji , na hata nikitoboa itakuwa kwa mbinde sana labda

#UziTayari
 
Sioni kama kuna madhara maana lamination inasaidia kukitunza na kukilinda cheti chako na kuharibika either maji, kuchanika nk, labda ungemuhoji zaidi ili kujua labda protocol zao zinatoa sababu gani ya kutokukifanyia lamination
 
Bila hiyo lamination sioni cheti kikidumu walau miaka 3

Na hizi movement za kuhama hama hapa mjini 🙌

Sijawahi kujua ni kosa kuweka lamination kwenye vyeti, maana ndiyo njia rahisi ya utunzaji wa nyaraka kibongo bongo
 
Nilitia kwenye begi kusafiri nacho mahali nikaweka ndani ya Daftari ikisaidia kidogo lakini Kuna sehemu pembeni mikunjo imeanza tayari
 
Kitie lamination then toa kopi moja ambayo utakuwa ukiitumia kama original baada ya kuwa certified na Mwanasheria

Ni risk kutembea na document original kama hiyo
 
Moja kwa moja..

Siku za nyuma nilienda Veta kuchukua cheti changu , niliistaajabu baada ya kupewa yule Dada aliyenipa aliniambia nisiweke lamination bila kuniambia sababu.

Naomba kujua wajuzi je , ipi inawezekana kuwa sababu ya kuniambia hivyo na je , Kuna madhara yeyote niliweka ? maana vyeti vyangu vingi vya O_level , Advance , kuzaliwa , best student nk vyote nimewekea lamination.

Na bila lamination sidhani kama nitatoboa kwenye utunzaji , na hata nikitoboa itakuwa kwa mbinde sana labda

#UziTayari
Hakuna hasara. Halafu huyo dada achana naye, cheti ni cha kwako namna unavyohifadhi yeye haimhusu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom