Kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa, nasubiri kuona!

Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
494
674
Naona watu wanafurahia kuruhusiwa kwa mikutano ya vyama, ila tatizo sijui kama limezungumzwa na kuwekewa mipaka

1. Kuna kitu kimeitwa lugha ya staha, je, ni pamoja na kutokosolewa? Je, ni nani anayeamua kuwa wewe lugha uliotumia sio ya staha? Ni polisi?

2. Double standards. Huko nyuma kulikuwa na lugha ya kujibu mapigo haswa pale upande unapoelemewa na tuhuma... polisi wameelekezwa cha kufanya haswa kwa CCM?

3. Kufumbia macho matendo ya kihalifu ndani ya siasa. Ipo misururu ya matukio yaliofanyiwa watu na wenzao wa upande wa pili na mpaka leo mamlaka husika ziko kimyaaaa! Yakijitokeza si wapo watakaoona wanachokozwa?

4. Vyama vingine mpaka sasa ama vina migogoro ya ndani ambayo mingine msajili wa vyama anahusika au vyama havijafanya chaguzi kwa mujibu wa katiba zao!

5. Kwa maoni yangu, msajili ameshindwa kusimamia siasa kwa haki bila kujihusisha na siasa zenyewe...no professionalism at all!!
Anaua siasa badala ya kujenga!!

6. Kufanikiwa kwa siasa zetu bila wafanyakazi wa serikali, polisi na msajili kujizuia kwa kudhamiria, itakuwa ni ngumu !!
 
Kauli ya Rais ni SHERIA.

TBC wakumbuke kufanya coverage ya mikutano yote ya vyama vya siasa bila upendeleo Kwa Chama tawala.
 
Wakiweza kutofautisha kati ya siasa na harakati hawatatukanana, ila wakianza harakati watajikuta wanatukanana na sio kutoa fikra mbadala. Mao anasema politics is a war without a blood shed and war is a politics with a bloodshed, so watz wanaweza wao wakaamu waache utamaduni wa kuvumiliana wa-act kama wanaigeria Hilo sasa liko mikononi mwa wanasiasa wenyewe.
 
Back
Top Bottom