Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimekuwa nikifuatilia taarifa zinazotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, na kuona mara nyingi sana watoa taarifa ambazo kwa kweli zinapaswa tu kuripotiwa na magazeti ya kila siku badala ya kuzitoa kama taarifa rasmi kwenye headed paper ya kurugenzi.
Je, Kurugenzi ya Mawasiliano wameamua kuwa kuwa chombo cha propaganda za kisiasa za Raisi Magufuli badala ya kuwa chombo ambacho kinatoa taarifa muhimu na rasmi kwa wananchi?
Kwa mfano hili la Rais kufanya mazoezi na kutoa mchango wa milioni 20 kwa ajili ya wavuvi. Kweli hivi vitu ni vya kutolea taarifa rasmi kwenye headed paper ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu?
Kuna vitu vidogo vidogo vingi tu ambavyo Kurugenzi ya Mawasiliano huwa inaamua kuvitolea taarifa rasmi ambavyo kwa kweli wala havistahili kupewa hadhi ya taarifa rasmi kutoka Ikulu. Hii inashusha hadhi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na kufanya waonekane kama ni gazeti la mtaani au chombo cha Propaganda cha Rais. Tafadhali jirekebisheni.