Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu acheni kufanya kazi kama gazeti au chombo cha propaganda

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,117
18,710
Nimekuwa nikifuatilia taarifa zinazotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, na kuona mara nyingi sana watoa taarifa ambazo kwa kweli zinapaswa tu kuripotiwa na magazeti ya kila siku badala ya kuzitoa kama taarifa rasmi kwenye headed paper ya kurugenzi.

Je, Kurugenzi ya Mawasiliano wameamua kuwa kuwa chombo cha propaganda za kisiasa za Raisi Magufuli badala ya kuwa chombo ambacho kinatoa taarifa muhimu na rasmi kwa wananchi?

Kwa mfano hili la Rais kufanya mazoezi na kutoa mchango wa milioni 20 kwa ajili ya wavuvi. Kweli hivi vitu ni vya kutolea taarifa rasmi kwenye headed paper ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu?

Kuna vitu vidogo vidogo vingi tu ambavyo Kurugenzi ya Mawasiliano huwa inaamua kuvitolea taarifa rasmi ambavyo kwa kweli wala havistahili kupewa hadhi ya taarifa rasmi kutoka Ikulu. Hii inashusha hadhi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na kufanya waonekane kama ni gazeti la mtaani au chombo cha Propaganda cha Rais. Tafadhali jirekebisheni.
 
Hadi aibu
 
Hili swala hata mimi limenipa ukakasi kidogo, Kwanza Ile taarifa ilirekodiwa Kwa simu Kama uminglaia vizuri huko mitandaoni. Kimsingi mimi binafs ni "PR officer" by professional, ili kitu kiwe habari mpaka ikahitajika kutolewa maelekekezo tena kupitia "news release" Ile ya Jana haina hata sababu moja ya kutolewa taarifa rasmi . Hiki kitengo kimegeuka kuwa cha propaganda bila hata aibu..........hata Kwa mwandishi wa habari makini hawezi akaichukua Ile habari Kama priority, Kwa sababu inakosa "criteria" nyingi za kuwa habari!!!!!
 
Milioni 20 aliyoitoa ni sehemu ya kodi tunazolipa hivyo sio vibaya tukipewa taarifa. Kama sijakosea bwana mkubwa analo fungu la mengineyo ambalo kwa mwezi linafika shilingi milioni 100.
Tatizo ni kwamba ili tupate hiyo taarifa siyo lazima Kurugenzi ya Mawasiliano iitoe kama taarifa rasmi. La sivyo siku moja Magufuli atatembelewa na mjomba wake pale Ikulu na Kurugenzi ya Mwasialo watatupa taarifa rasmi, "Leo Raisi Magufuli ametembelewa Ikulu na mjomba wake toka Chato"
 
Kama umeshindwa kumfundisha kazi Mbowe ili aachie madaraka baada ya kuichakaza saccos , utaweza kuifundisha kazi kurugenzi ya ikulu??
Siku zote duniani kunakuwa na watu wa aina mbili - mashabiki wasiojua lolote na wanaokwenda upande wowote kwa kusukumwa, na wale walio na uwezo wa kufikiri, wanaowasukuma mashabiki. Ni rahisi kuona uko wapi kati ya haya makundi mawili.
 
Tatizo ni kwamba ili tupate hiyo taarifa siyo lazima Kurugenzi ya Mawasiliano iitoe kama taarifa rasmi. La sivyo siku moja Magufuli atatembelewa na mjomba wake pale Ikulu na Kurugenzi ya Mwasialo watatupa taarifa rasmi, "Leo Raisi Magufuli ametembelewa Ikulu na mjomba wake toka Chato"
Hahahaha, nimependa msisitizo wa hoja yako.
 
Nimekuwa nikifuatilia taarifa zinazotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, na kuona mara nyingi sana watoa taarifa ambazo kwa kweli zinapaswa tu kuripotiwa na magazeti ya kila siku badala ya kuzitoa kama taarifa rasmi kwenye headed paper ya kurugenzi.

Je, Kurugenzi ya Mawasiliano wameamua kuwa kuwa chombo cha propaganda za kisiasa za Raisi Magufuli badala ya kuwa chombo ambacho kinatoa taarifa muhimu na rasmi kwa wananchi?

Kwa mfano hili la Rais kufanya mazoezi na kutoa mchango wa milioni 20 kwa ajili ya wavuvi. Kweli hivi vitu ni vya kutolea taarifa rasmi kwenye headed paper ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu?

Kuna vitu vidogo vidogo vingi tu ambavyo Kurugenzi ya Mawasiliano huwa inaamua kuvitolea taarifa rasmi ambavyo kwa kweli wala havistahili kupewa hadhi ya taarifa rasmi kutoka Ikulu. Hii inashusha hadhi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na kufanya waonekane kama ni gazeti la mtaani au chombo cha Propaganda cha Rais. Tafadhali jirekebisheni.
Unawaonea ndugu unajua aliewaweka anataka kusikia nini,?
 
Acheni watu wafanye kazi zao

zama zinabadilika msikariri
Kwa hiyo wakifanya upupu tukae kimya kwa kuwa zama zimebadilika? Watu wote wakianza kula kinyesi cha ng'ombe bado sintakula, maana wewe unadokeza utakula.
 
Back
Top Bottom