Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu acheni kufanya kazi kama gazeti au chombo cha propaganda

Kwakweli, yaani hiyo Kurugenzi inachuana na kijarida kiitwacho Tanzanite kwa sasa
 
Kurugenzi kutoa habari zaidi ni kitu kizuri. Si kibaya.

Kila kitu anachofanya rais kiwe wazi kwa matamshi rasmi ya Ikulu.
 
Hehehehehe! Kazi ipo.

Kuna siku tutaambiwa taarifa rasmi, "Rais Kamnunulia Maua Mama Jesca Valentine Day"
Kwamba hilo ni jambo zuri au baya tunaweza kujadili.

Lakini, kuripoti hilo kama limefanyika kweli, hakuwezi kuwa jambo baya.

Kwa sababu, kama kufanya hivyo ni uambo baya, wananchi watapata nafasi kujua.

Kama hilo ni jambo zuri, wananchi watapata nafasi kujua.

Mimi sitapinga hilo.

Naweza kutaka kupewa habari nyingine zaidi. Kama rais anapata wapi hela anazotumia nje ya bajeti, kwa sababu gani anatumia hela nje ya bajeti.

Mtu anayeandika habari za rais kumnunulia mkwmewe maua siku ya Valentine ni mzuri kwa uwazi.

Anajiweka katika mazingira ya kutoweza kukataa kueleza hela za kununua Dreamliner zilipitishwa na bajeti gani.
 
Kurugenzi kutoa habari zaidi ni kitu kizuri. Si kibaya.

Kila kitu anachofanya rais kiwe wazi kwa matamshi rasmi ya Ikulu.
Hatujaelewana Mkuu. Hatusemi Kurugenzi ya Mawasiliano haipaswi kutoa taarifa. Lakini misingi ya press release, hasa kwa taasisi kama IKulu ni kwamba sio unaripoti vitu visivyo na maana au umuhimu kwa taifa. Sasa Magufuli kutoa milioni 20 tena ya kushitukiza akiwa mazoezini kwa ajili ya wavuvi pale Kigamboni ina umuhimu gani kwa mkulima wa Pamba wa Shinyanga hadi itolewe kama taarifa rasmi kwa ajili ya Watanzania wote? Kumbuka Magufuli sio raisi wa Dar es Salaam na press release za Ikulu sio kwa ajili ya Dar es Salaam

Hawa Kurugenzi ni kwamba wanafanya kazi sio kama professional reporters, bali kundi la mashabiki wa Magufuli ambao wanaona kila kitu anachofanya Magufuli ni taarifa rasmi kwa Watanzania wote. Hilo ndilo tunakataa. Kama hawajui ni nini kinapaswa kuwa taarifa rasmi ya kutolewa kama press release basi waondoke pale. La sivyo waanzishe kijarida cha kila siku wakiite "Kutoka Meza ya Magufuli" na kutoa vijihabari vidogo vidogo kama hivyo. Hizi press releaze zinasomwa na watu wengi na sana sana zinatutia aibu tunaonekana kama just another SH country.

Acha tuiheshimu Press Release au Taarifa Rasmi kutoka Ikulu na kuipa status inayokubalika, sio vitaarifa ambavyo hata gazeti la kawaida la kila siku haviziweki kwenye chapisho kwa kuwa wanaona sio news.
 
Kwamba hilo ni jambo zuri au baya tunaweza kujadili.

Lakini, kuripoti hilo kama limefanyika kweli, hakuwezi kuwa jambo baya.

Kwa sababu, kama kufanya hivyo ni uambo baya, wananchi watapata nafasi kujua.

Kama hilo ni jambo zuri, wananchi watapata nafasi kujua.

Mimi sitapinga hilo.

Naweza kutaka kupewa habari nyingine zaidi. Kama rais anapata wapi hela anazotumia nje ya bajeti, kwa sababu gani anatumia hela nje ya bajeti.

Mtu anayeandika habari za rais kumnunulia mkwmewe maua siku ya Valentine ni mzuri kwa uwazi.

Anajiweka katika mazingira ya kutoweza kukataa kueleza hela za kununua Dreamliner zilipitishwa na bajeti gani.
Soma hapo juu, nimekupa maelezo yenye kujitosheleza. Yaani unaona Magufuli kumpa Mama Jeca maua siku ya Velentine ni jambo linapaswa kujadiliwa kama n sawa kutolewa press release na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu? Eeehe, nisije nikawa napoteza muda wangu kukuelimisha juu maana ya press release na zinapaswa kutolewa wakati gani, hasa na Ikulu.
 
Hujaelewa nilichokuambia.

Kama Ikulu ya Magufuli ni washamba, hawajui kipi cha kutolea press release na kipi si cha kutolea presa release, then uwazi wao kutoa press release kishamba ni jambo zuri.

Ama sivyo, wasipotoa press release kishamba, walipa kodi tutajuaje kwamba Ikulu ya Magufuli ni washamba?

Unataka wafiche ushamba wao kusiwe na press releases za kishamba tusiujue kama Ikulu ya Sani Abacha?

Wacha waandike ushamba wao tujue mpaka spelling mistakes zao.

Kesho mtu akiandika kitabu cha utawala wa Magufuli awe na ushahidi wote walioutoa wenyewe.

Unawakataza wasitupe ushahidi wa ujinga wao?
 
Hujaelewa nilichokuambia.

Kama Ikulu ya Magufuli ni washamba, hawajui kipi cha kutolea press release na kipi si cha kutolea presa release, then uwazi wao kutoa press release kishamba ni jambo zuri.

Ama sivyo, wasipotoa press release kishamba, walipa kodi tutajuaje kwamba Ikulu ya Magufuli ni washamba? Unataka wafiche ushamba wao kusiwe na presa releases za kishamba tusiujue kama Ikuku ya Sanu Abacha?

Wacha waandike ushamba wao tujue mpaka soelling mistakes zao. Kesho mtu akiandika kitabu cha utawala wa Magufuli awe na ushahidi wote walioutoa wenyewe. Unawakataza wasitupe ushahidi wa ujinga wao?

Hapana Mkuu. IKiwa wife nyumbani anafanya vitu vya kuaibisha, ni vema kumweka sawa kabla majirani wengi hawajajua ili kuficha aibu. Sasa hawa jamaa wanachofanya aibu ni yetu wote. Soon or later Wakenya wataanza kutucheka. Ndio maana inabidi tuwashitue mapema. Ukweli ni kwamba wengi wetu tunaona aibu kusoma hizi press release za Ikulu kwa kuwa zinatuaibisha kama Watanzania. Ndio maana tunataka warekebishe haraka.
 
Acheni tupate matukio yoote yanayofanywa na jembe letu! Mwenye wivu akajirushe katikati ya kundi la mamba
Nilisema watu wenye akili kama unayoonyesha hapa, Rais akivaa suti ya Mfalme isiyoonekana mtashangilia na kumsifia kuwa kapendeza imemkaa mwilini vizuri sana. Kuna wengine tutaona aibu kwamba rais wetu anajidharirisha yeye na nchi yetu. Hata kama tunampenda kiasi gani hatutashangilia na kumsifia kuwa kapendeza kama atakavyotaka au kutegemea tufanye. Sasa hiyo ndio tofauti kati ya wewe na mimi.
 
Hapana Mkuu. IKiwa wife nyumbani anafanya vitu vya kuaibisha, ni vema kumweka sawa kabla majirani wengi hawajajua ili kuficha aibu. Sasa hawa jamaa wanachofanya aibu ni yetu wote. Soon or later Wakenya wataanza kutucheka. Ndio maana inabidi tuwashitue mapema. Ukweli ni kwamba wengi wetu tunaona aibu kusoma hizi press release za Ikulu kwa kuwa zinatuaibisha kama Watanzania. Ndio maana tunataka warekebishe haraka.
Unapofananisha vitu fananisha sawasawa.

Magufuli ni mfanyakazi wako. Housegirl. Si wife.

Kama ana madhaifu makubwa hivyo, ni vizuri uyajue umfukuze uweke mwingine.

Sasa wewe unataka afiche mapungufu usiyajue?
 
Unapofananisha vitu fananisha sawasawa.

Magufuli ni mfanyakazi wako. Housegirl. Si wife. Kama ana madhaifu makubwa hivyo, ni vizuri uyajue umfukuze uweke mwingine.
Sasa wewe unataka afiche mapungufu usiyajue?

Do, kazi kweli kweli. Jifunze lugha na suala la mifano au kitu kinaitwa kwa kiingereza "analogy". Sijui kama wewe ni Mkristo. Unakumbuka Yesu alisema usipokula mwili wangu na kunywa damu yangu huiingii ufalme wa mbinguni na watu wakamwacha wakisema huyu ana kichaa? Basi wewe ungekuwa kundi la wale waliomwacha.
 
Nakwambia hivi. Kanuni ya kwanza ya analogy hujui.

Unamfananisha mfanyakazi wako anayekuja kukuomba kazi kila baada ya miaka mitano na mke ambaye kama wewe unafuata mifano ya kibiblia umeamriwa kuwa naye maisha yote.

Hujui hata kanuni za kufananisha mambo.

Unataka kumfanya housegirl awe mkeo.
 
Tatizo ni kwamba ili tupate hiyo taarifa siyo lazima Kurugenzi ya Mawasiliano iitoe kama taarifa rasmi. La sivyo siku moja Magufuli atatembelewa na mjomba wake pale Ikulu na Kurugenzi ya Mwasialo watatupa taarifa rasmi, "Leo Raisi Magufuli ametembelewa Ikulu na mjomba wake toka Chato"
au mwanae toka CALLMEJAY
 
Nakwambia hivi. Kanuni ya kwanza ya analogy hujui.

Unamfananisha mfanyakazi wako anayekuja kukuomba kazi kila baada ya miaka mitano na mke ambaye kama wewe unafuata mifanyo ya kibiblia umeamriwa kuwa naye maisha yote.

Hujui hata kanuni za kufananisha mambo.

Unataka kumfanya housegirl awe mkeo.
Mkuu, awe atakaa mika mitano au 10, huwezi kuacha kitu kibaya kiendelee ili watu waone udhaifu wake upate sababu ya kumtoa.

Kwa hiyo suala la analogy niliyotoa haijali kama ni mke au housegirl, suala ni kwamba ni mtu ambaye kwa wakati huo anaathiri reputation yako. Kwa hiyo mimi hata kama sintapenda vitu anavyofanya Magufuli na labda hata kwamba asishinde uchaguzi ujao, pale ambapo kuna kitu anakosea nitapenda arekebishe ili mambo yawe mazuri.

Labda nikuulize. Ikiwa wewe ungekuwa mfanya biashara wa usafiri wa mabasi, tuseme njia ya Dar-Arusha. Je uneona kuwa basi ambalo linashindana katika ruti yako lina tatizo ambalo linaweza kusababisha likapinduka, usingesema ili hilo basi lipinduke ili abiria waje kwako kwa kuona udhaifu wa ile kampuni unayoshindana nayo ya kutofanyia maintanance mabasi yao?

Sasa mie siko hivyo. Hata kama ni washindani ningewashauri warekebishe hiyo kasoro ili isije ikaathiri watu, pamoja na kuwa ni washindani wangu.
 
You are focused on the symptom instead of the underlying disease.

Mtu ana kifua kikuu cha UKIMWI, wewe unasema tumpe Cofta tuondoe kikohozi, kikohozi kinaleta aibu.

Badala ya kushukuru anakohoakohoa ujue huyu ana tatizo utafute suluhisho la kudumu.
 
You are focused on the symptom instead if the underlying disease.

Mtu ana kifua kikuu cha UKIMWI, wewe unasema tumpe Cofta tuondoe kikohozi, kikohozi kinaleta aibu.

Badala ya kushukuru anakohoakohoa ujue huyu ana tatizo utafute suluhisho la kudumu.
Do, Mkuu naanza kukuogopa! Yaani wewe una ile mentality ya kukomboa nchi kama wapigania uhuru wa msituni, yaani guerilla warfare philosophy, ambayo huwa tunasema lazima iwe na collateral damage. Taratibu Mkuu, sisi sote ni ndugu, na tunajenga banda moja japo tunabishana design la banda.
 
To the contrary.

I hardly give a f*.ck.

I'm practically celibate.
 
Back
Top Bottom