TinyMonster
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 248
- 154
Nimeona nilisemelee hili mapema kabla kampeni hazijaanza, kiukweli kurugenzi ya mawasiliano CHADEMA imepwaya sana suala la organization ya huu mkutano mkuu. Mtu anaweza kuwaza kuwa uhaba wa vyombo vya habari kwenye Mkutano ni kwa sababu vyombo vya habari vina uoga lakini ukweli ni kwamba newsroom nyingi hazikuwa na taarifa za uhakika kuhusu kama kitakuwa kikao cha ndani au wataruhusiwa kurusha live matokeo yake wengi wakaishia kutuma mwandishi na cameraman mmoja badala ya crew ya live.
Kitu kingine katika zama hizi ambazo vitu vingi vinaenda kupitia YouTube ilitakiwa CHADEMA Digital wawe na live link moja ambayo wangesambaza kwa waandishi wote ili ambaye anataka kupeleka hewani anafanya kuichukua, kwa hili ACT Wazalendo walilifanya siku wanamtambulisha Membe na matokeo yake walipata visibility kubwa mno na ninaamini hata Jumatano kwenye Mkutano Mkuu wao watafanya hivi hivi, Tumaini Makene na wenzako mnaweza kujifunza hiki kitu.
Ushauri wangu ni kwamba idara iamke iwe aggressive kwenye kusukuma brand ya CHADEMA na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari, tuache kufanya vitu kwa mazoea kwa sababu wakati sisi tunatembea wenzetu wanakimbia. Na muhimu zaidi tafuteni vijana ambao ni tech savy wanaojua kufanya graphic designing na video editing wakae ofisini kipindi chote kizima cha uchaguzi wasaidie kwenye social media.