dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Salaam Wakuu,
Hivi karibuni kumekuwepo na kukengeuka au kulewa sifa hadi kujisahau kwa Watendaji wanaomsaidia Rais kusambaza Habari kwa Umma. Siamini kwamba imepwaya kama watu wanavyosema.
Wameshindwa kufuata au kujikita kwenye weredi na Utaratibu katika kufanya kazi za Ikulu hadi wanaharibu.
Hivi Karibuni Taifa lilipata Msiba wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu B. Mkapa. Ikatoka taarifa ambayo ilitia shaka hadi watu wakawa hawaamin taarifa kwani ilikuwa haijajitosheleza. Mbaya zaidi hata Wimbo wa Taifa haukupigwa.
Tuache hiyo.
Sasa tupo Wakati wa Uchaguzi, lakini Ikulu na taasisi ya Rais kwa Ujumla wake, Wanatumia bajeti ya kuwezesha Kampani na Mchakato wa Mgombea wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Dr. Magufuli.
Ipi Mipaka ya Kurugenzi ya Habari Ikulu?
Je, Wanaruhusiwa mumsaidia mgombea wa Chama Chochote au ni Matumizi Mabaya ya Madaraka na kujipendekeza?
Viapo wanavyoapa vipoje?
Ukiangalia tovuti za Ikulu, kuna Kampeni za CCM tu na maneno ya kukashifu, kukejeli na kudhalilisha vyama vingine.
Kwa mtazamo hawatendi haki, bora wangejikita kwenye majukumu yao ambayo ni;
(i) Kupata na kusambaza taarifa kwaajili ya kuhabarisha umma juu ya sera, programu kazi na maboresho yanayofanyika Ikulu tu.
(ii) Kuratibu utoaji wa taarifa za Ikulu tu kwenye vyombo habari.
(iii) Kufanya mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu ofisi ya Rais na Watendaji wa Ikulu
(iv) Kuratibu maandalizi ya nyaraka za Ikulu
(v) Kuratibu maandalizi na uzalishaji wa makala za ofisi ya rais katika magazeti na majarida mbalimbali na
(vi) Kuhuisha taarifa za Ikulu kwenye tovuti ya Ikulu.
Sio kufanya Kampeni na kuonesha Upande wa Chama cha SIASA. Sababu pale Ikulu ni Ofisi ya CCM bali ni Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Ikulu ya Watanzania wote bila kubagua vyama.
Naamin hatutaona YouTube ya Ikulu wwkituwekea tena Kampeni za CCM na Matangazo ya kuonesha Upande wa CHAMA. Huwezi jua Uchaguzi ukiisha Ikulu ataingia nani.
Gerson Msigwa jitafakari. Upo wapi Utawala wa Sheria?