Uchaguzi 2020 Kurugenzi ya Ikulu imechagua upande katika kampeni? Inashawishi watu wamchague Mgombea wa CCM, Dkt. Magufuli

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,366
2,000
Salaam Wakuu,

Hivi karibuni kumekuwepo na kukengeuka au kulewa sifa hadi kujisahau kwa Watendaji wanaomsaidia Rais kusambaza Habari kwa Umma. Siamini kwamba imepwaya kama watu wanavyosema.

Wameshindwa kufuata au kujikita kwenye weredi na Utaratibu katika kufanya kazi za Ikulu hadi wanaharibu.

Hivi Karibuni Taifa lilipata Msiba wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu B. Mkapa. Ikatoka taarifa ambayo ilitia shaka hadi watu wakawa hawaamin taarifa kwani ilikuwa haijajitosheleza. Mbaya zaidi hata Wimbo wa Taifa haukupigwa.

Tuache hiyo.

Sasa tupo Wakati wa Uchaguzi, lakini Ikulu na taasisi ya Rais kwa Ujumla wake, Wanatumia bajeti ya kuwezesha Kampani na Mchakato wa Mgombea wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Dr. Magufuli.

Ipi Mipaka ya Kurugenzi ya Habari Ikulu?

Je, Wanaruhusiwa mumsaidia mgombea wa Chama Chochote au ni Matumizi Mabaya ya Madaraka na kujipendekeza?

Viapo wanavyoapa vipoje?

Ukiangalia tovuti za Ikulu, kuna Kampeni za CCM tu na maneno ya kukashifu, kukejeli na kudhalilisha vyama vingine.

Kwa mtazamo hawatendi haki, bora wangejikita kwenye majukumu yao ambayo ni;

(i) Kupata na kusambaza taarifa kwaajili ya kuhabarisha umma juu ya sera, programu kazi na maboresho yanayofanyika Ikulu tu.

(ii) Kuratibu utoaji wa taarifa za Ikulu tu kwenye vyombo habari.

(iii) Kufanya mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu ofisi ya Rais na Watendaji wa Ikulu

(iv) Kuratibu maandalizi ya nyaraka za Ikulu

(v) Kuratibu maandalizi na uzalishaji wa makala za ofisi ya rais katika magazeti na majarida mbalimbali na

(vi) Kuhuisha taarifa za Ikulu kwenye tovuti ya Ikulu.

Sio kufanya Kampeni na kuonesha Upande wa Chama cha SIASA. Sababu pale Ikulu ni Ofisi ya CCM bali ni Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Ikulu ya Watanzania wote bila kubagua vyama.

Naamin hatutaona YouTube ya Ikulu wwkituwekea tena Kampeni za CCM na Matangazo ya kuonesha Upande wa CHAMA. Huwezi jua Uchaguzi ukiisha Ikulu ataingia nani.

Gerson Msigwa jitafakari. Upo wapi Utawala wa Sheria?
 
johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
634
1,000
Ndio maana picha zote kwenye TV kuhusu matangazo mubashara ya chama pendwa, hufanana kana kwamba mpiga picha ni mmoja?
 
Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
717
1,000
Kurugenzi ya Ikulu inakuja na vi slogan vya "TUTAELEWANA" na mapichapicha kibao, what a shame kwa mtumishi wa umma anayelipwa mshahara na watanzania wote walio na vyama na wasio na vyama pia. Ni vizuri kuzingatia maadili ya utumishi wa umama wa kutofanya mambo ya siasa katika utendaji wa umma.

Sijui kama ataweza kubadilika sasa kwani alikwisha haribu tangia mwanzo ambapo akiacha kufanya sasa anaweza kuulizwa kwa nini hafanyi tena.
 
Dunamist

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
474
1,000
Nilikuwa live hapa YouTube channel ya Ikulu nikiangalia uchukuaji fomu wa JIWE
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,188
2,000
Hii Ni awamu ya vituko sana MUNGU tusaidie wapite na kuondoka at least tutapumua

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hii mitano hawakujua kama ita kwisha, sasa wana shangaa wana takiwa kurudi tena kwa wanancji. Sijui kule waliko kutelekeza hata kwrnda kuwashukuru wale wachache walio mpa kura ata kwrndaje huko kuomba kura??
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
4,871
2,000
Awamu ya kishindo hii, ni kusifu na kuabudu tu... ni nani anakulipa mshahara!!
 
jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
2,083
2,000
Salaam Wakuu,

Hivi karibuni kumekuwepo na kukengeuka au kulewa sifa hadi kujisahau kwa Watendaji wanaomsaidia Rais kusambaza Habari kwa Umma. Siamini kwamba imepwaya kama watu wanavyosema.

Wameshindwa kufuata au kujikita kwenye weredi na Utaratibu katika kufanya kazi za Ikulu hadi wanaharibu.

Hivi Karibuni Taifa lilipata Msiba wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu B. Mkapa. Ikatoka taarifa ambayo ilitia shaka hadi watu wakawa hawaamin taarifa kwani ilikuwa haijajitosheleza. Mbaya zaidi hata Wimbo wa Taifa haukupigwa.

Tuache hiyo.

Sasa tupo Wakati wa Uchaguzi, lakini Ikulu na taasisi ya Rais kwa Ujumla wake, Wanatumia bajeti ya kuwezesha Kampani na Mchakato wa Mgombea wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Dr. Magufuli.

Ipi Mipaka ya Kurugenzi ya Habari Ikulu?

Je, Wanaruhusiwa mumsaidia mgombea wa Chama Chochote au ni Matumizi Mabaya ya Madaraka na kujipendekeza?

Viapo wanavyoapa vipoje?

Ukiangalia tovuti za Ikulu, kuna Kampeni za CCM tu na maneno ya kukashifu, kukejeli na kudhalilisha vyama vingine.

Kwa mtazamo hawatendi haki, bora wangejikita kwenye majukumu yao ambayo ni;

(i) Kupata na kusambaza taarifa kwaajili ya kuhabarisha umma juu ya sera, programu kazi na maboresho yanayofanyika Ikulu tu.

(ii) Kuratibu utoaji wa taarifa za Ikulu tu kwenye vyombo habari.

(iii) Kufanya mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu ofisi ya Rais na Watendaji wa Ikulu

(iv) Kuratibu maandalizi ya nyaraka za Ikulu

(v) Kuratibu maandalizi na uzalishaji wa makala za ofisi ya rais katika magazeti na majarida mbalimbali na

(vi) Kuhuisha taarifa za Ikulu kwenye tovuti ya Ikulu.

Sio kufanya Kampeni na kuonesha Upande wa Chama cha SIASA. Sababu pale Ikulu ni Ofisi ya CCM bali ni Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Ikulu ya Watanzania wote bila kubagua vyama.

Naamin hatutaona YouTube ya Ikulu wwkituwekea tena Kampeni za CCM na Matangazo ya kuonesha Upande wa CHAMA. Huwezi jua Uchaguzi ukiisha Ikulu ataingia nani.

Gerson Msigwa jitafakari. Upo wapi Utawala wa Sheria?
Isikutishe dikteta yahaya jamei alimiliki kila kitu kuanzia dola,tume,polisi,mahakama na kila kitu lakini vyoote vilishindwa kumuokoa.
aanayemiliki wananchi ndie mwenye nguvu kuliko anayemiliki dola
 
abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
617
1,000
Salaam Wakuu,

Hivi karibuni kumekuwepo na kukengeuka au kulewa sifa hadi kujisahau kwa Watendaji wanaomsaidia Rais kusambaza Habari kwa Umma. Siamini kwamba imepwaya kama watu wanavyosema.

Wameshindwa kufuata au kujikita kwenye weredi na Utaratibu katika kufanya kazi za Ikulu hadi wanaharibu.

Hivi Karibuni Taifa lilipata Msiba wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu B. Mkapa. Ikatoka taarifa ambayo ilitia shaka hadi watu wakawa hawaamin taarifa kwani ilikuwa haijajitosheleza. Mbaya zaidi hata Wimbo wa Taifa haukupigwa.

Tuache hiyo.

Sasa tupo Wakati wa Uchaguzi, lakini Ikulu na taasisi ya Rais kwa Ujumla wake, Wanatumia bajeti ya kuwezesha Kampani na Mchakato wa Mgombea wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Dr. Magufuli.

Ipi Mipaka ya Kurugenzi ya Habari Ikulu?

Je, Wanaruhusiwa mumsaidia mgombea wa Chama Chochote au ni Matumizi Mabaya ya Madaraka na kujipendekeza?

Viapo wanavyoapa vipoje?

Ukiangalia tovuti za Ikulu, kuna Kampeni za CCM tu na maneno ya kukashifu, kukejeli na kudhalilisha vyama vingine.

Kwa mtazamo hawatendi haki, bora wangejikita kwenye majukumu yao ambayo ni;

(i) Kupata na kusambaza taarifa kwaajili ya kuhabarisha umma juu ya sera, programu kazi na maboresho yanayofanyika Ikulu tu.

(ii) Kuratibu utoaji wa taarifa za Ikulu tu kwenye vyombo habari.

(iii) Kufanya mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu ofisi ya Rais na Watendaji wa Ikulu

(iv) Kuratibu maandalizi ya nyaraka za Ikulu

(v) Kuratibu maandalizi na uzalishaji wa makala za ofisi ya rais katika magazeti na majarida mbalimbali na

(vi) Kuhuisha taarifa za Ikulu kwenye tovuti ya Ikulu.

Sio kufanya Kampeni na kuonesha Upande wa Chama cha SIASA. Sababu pale Ikulu ni Ofisi ya CCM bali ni Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Ikulu ya Watanzania wote bila kubagua vyama.

Naamin hatutaona YouTube ya Ikulu wwkituwekea tena Kampeni za CCM na Matangazo ya kuonesha Upande wa CHAMA. Huwezi jua Uchaguzi ukiisha Ikulu ataingia nani.

Gerson Msigwa jitafakari. Upo wapi Utawala wa Sheria?
Kwan mkiingia chadema madarakani mtamuacha pale???? Hata yeye lazima atetee ugal
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,273
2,000
Nilikuwa live hapa YouTube channel ya Ikulu nikiangalia uchukuaji fomu wa JIWE
Watanzania tunachukulia poa, lakini moja kati ya alama za udikteta ndio hizi. Mipaka ya serikali na mtu binafsi haionekani, mambo ya Magufuli kwenda kuchukua fomu, leo yanaripotiwa na msemaji wa ikulu ya Rais.
 
HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
6,970
2,000
Tuache unafiki, hata ikitokea bahati mbaya Lissu akaingia Ikulu, basi wale mandondocha wenu wa CHADEMA watajaza mpaka picha za kutanua vidole na M4C kwenye website za Ikulu na serikali.

Watumishi mnaweza kuwalazimisha wavae magwanda na wawe wanatanua vidole kila wakati.
Kwahiyo tuache unafiki!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom