Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,875
Wenzetu waliwarithisha watoto wao elimu ujuzi na maarifa vyenye manufaa kwenye jamii na bila kulazimisha bali kwa miongozo sahihi na utaratibu maalum.
Kuna nguvu kazi kubwa tu ya Taifa inaangamizwa na nguvu ya kurithi mikoba mikoba ya uganga na ushirikina mikoba ya kuagua kienyeji mikoba ya kuloga na kumiliki majini.
Tuna shuhuda za watu tukizisikia humu zinasikitisha mno vijana wasomi walioelimika wazalendo waliokuwa tayari kulitumikia taifa lao wamekatishwa ndoto zao nyingi baada ya kulazimishwa kuacha yote na kurudi nyumbani wakamilikishwe kilinge wakamilikishwe mikoba.
Dunia sasa inabadilika ukweli unachukua nafasi yake kwa nguvu wazee wanaona uhalisia ulipo , acha mtoto arithi kwa mapenzi yake mwenyewe kwa utashi wake hapa hakuna shida kabisa.
Tulikuwa na wazee watemi wenye kupenda kulazimisha mambo hata yasiyo na msaada kwa familia wala jamii bali sifa za kinazi na za kijinga kabisa za mtu kusifiwa kumiliki majini mengi au matunguli chumba kizima nk nk
Mwamko wa sasa ni mkubwa lakini je hawa wajuzi wanaopotelea kwenye ndumba za kurisishwa tutawasaidiaje?
Kitu kibaya kabisa kwenye huu utaratibu wa kurisishwa ni kwamba ukikataa hakuna jambo lako hata moja litakalosonga , kila kitu kitaparaganyika kuanzia familia mpaka kipato na hata kazi na maendeleo yoyote uliyoanza kuyapata