kurithi majina

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
habari zenyu bhana. wana jamvi me kuna jambo huwa linanikera (samahan kama kuna mtu nitamkwaza) kuna ile kasumba ya kurithi jina. mf. et bibi yangu aliitwa tabu/shida then nami nikipata mtoto nimuite shida/tabu yan hili haliniingii akilini ukizingatia jina linaweza kuleta uhalisia wa maisha ya mtu. mara babu aliitwa masumbuko/matatizo afu nkipata mtoto wa kiume nimuite majina hayo. dah inawia vigumu kweli. sijui ninyi wanajamvi huwa mnalichukuliaje?? karibuni. . . .
 
Kurithi majina kama: Shida, Tabu, Masumbuko, Havijawa, Havinitishi, Chausiku n.k. Si utaratibu mzuri ktk jamii zetu. Binafsi hata mie sipendi kurithisha watoto majina ya ajabu ajabu kama haya.
 
Kumbe kuna ambao kama mimi,afazaliii.....nilijua niko peke yangu! Mie Tuli wangu kalazimika kupewa jina la doto wakati hana pacha hivi inakuaje????!!!huu utaratibu siuelewi na wala sioni umaana wake fyuuuuu
 
Kama unaona unalipa, ufuate, na kama unaona haulipi, usiufuate. Kwani ukizaa mtoto mwenye jukumu la kumuita jina si ni wewe na mwandani wako?
The unseen is illustrated by the seen.
 
haya majina maawil mi hoi
 
kabla ya kumpa mtoto jina, liwe la kizungu, kiswahili, kikabila lazima ujue maana yake jamani, la sivyo utamtia mtoto nuksi....
Kwa nini umuite mtoto taabu, shida, masumbuko,matatizo, majuto? Yaani shida na tabu zakoumtupie mtoto? Hapana....

Na kabla hujamrisisha mtoto jina angalia maana ya jina na tabia za mwenye jina, usikute mwenye jina mlevi na mzizi unamtwisha mtoto jina baadae utaja lalama kuwa mtoto mlevi?

Si vyema kurithisha watoto majina kwa kweli....
 
Kurithi majina kama: Shida, Tabu, Masumbuko, Havijawa, Havinitishi, Chausiku n.k. Si utaratibu mzuri ktk jamii zetu. Binafsi hata mie sipendi kurithisha watoto majina ya ajabu ajabu kama haya.

mkuu,asante kwa mchango wako bt jamii nyng hasa wazaz wetu wanalazimisha ooh mtoto aitwe jina la babu / bibi yake. afu ukute mtoto kapata tatizo la ugonjwa / mchango kwa watoto jambo ambalo ni kawaida kwa watoto. utasikia muite flan atapona au analilia jina. shit!
 
Kumbe kuna ambao kama mimi,afazaliii.....nilijua niko peke yangu! Mie Tuli wangu kalazimika kupewa jina la doto wakati hana pacha hivi inakuaje????!!!huu utaratibu siuelewi na wala sioni umaana wake fyuuuuu

me mwenyewe mwanzon mama alitaka kumpa mwanangu jina la mdogo wake (marehemu) alieitwa tabu kisa et alikuwa anampea sana. weee nlikomaa kdg nikosane nae. unampandikizia mtoto matatzo tu kumpa majina ya ajabu. i hate ths kha!
 
Kama unaona unalipa, ufuate, na kama unaona haulipi, usiufuate. Kwani ukizaa mtoto mwenye jukumu la kumuita jina si ni wewe na mwandani wako?
The unseen is illustrated by the seen.

c ndo hapo mkuu, et anakuja babu/bibi yako anakwambia hyu anafanana na marehemu babu mzaa bibi/babu afu ukute alikuwa anaitwa masumbuko/tabu/matatizo. kha utafikiri we umekosa jina la kumpa mwanao. me huwa nakereka sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom