Kura ya NDIOOO na HAPANA bungeni inanikera

mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,506
661
Hii tabia ya kukubali hoja bungeni kwa kusema ndio kwa wanaokubali na hapana kwa wanaokataa na kisha spika kufanya maamuzi kwa kile alichosikia ni ujinga na kuwadanganya watanzania. Hivi kwa nini wasitumie mfumo wa kompyuta ambapo kila mbunge atabonyeza kitufe mezani kwake cha ndio au hapana kisha kwenye screen itakayokuwa hapo pembeni ya spika inaonesha ndio ni ngapi na hapana ni ngapi in figures. Mimi naona hilo halitushindi ila ni kwa ajili ya maslahi ndio maana halikufanywa. Muda umefika sasa wa kuanza kutumia hivi vitu
 
yani huu mfumo unakera kiukweli na hauko fair,hauna ufanisi na hauna tija as if wanafanya masiala..
 
Bora huo mfumo ungetumika kuliko huo wa sasa ambao unawanyima wengine uhuru.
 
Hii tabia ya kukubali hoja bungeni kwa kusema ndio kwa wanaokubali na hapana kwa wanaokataa na kisha spika kufanya maamuzi kwa kile alichosikia ni ujinga na kuwadanganya watanzania. Hivi kwa nini wasitumie mfumo wa kompyuta ambapo kila mbunge atabonyeza kitufe mezani kwake cha ndio au hapana kisha kwenye screen itakayokuwa hapo pembeni ya spika inaonesha ndio ni ngapi na hapana ni ngapi in figures. Mimi naona hilo halitushindi ila ni kwa ajili ya maslahi ndio maana halikufanywa. Muda umefika sasa wa kuanza kutumia hivi vitu
Kwa mfumo wa Kompyuta nahisi mambo yatakuwa yale yale. Kama mitandao ya kujumlisha kura kwenye uchaguzi Mkuu mwaka 2010 ilikwama, unategemea jipya gani la miujiza kwenye Bunge ambalo wapinzani ni wachache?
 
Kwenye uchaguzi mkuu kura zilikuwa zinahesabiwa vituoni kisha wanapeleka kwa DED ambaye ni RO kisha ded pamoja maafisa usalama wa mikoa, wilaya na baadhi ya wahusika wengine wanayachakachua na kutuma tume ya uchaguzi. Kwa hili nalosema mimi ni mfumo ambao ukibonyeza ndio majibu yanatokea kwenye screen moja kwa moja na yanaonekana na wote. Kuna hoja ambazo wanaoitikia ndio kati ya wabunge 345 ni 172 na hapana ni 173 hapa Masikio ya makinda yatajuaje uhalali wa kura au ni maamuzi ya Mtu mmoja kwenye maisha ya wtz.
 
Muda umefike watumie technology katika voting badala ya kelele za ndio na hapana!
Watumie machine,itakuwa na uhakika na italiongezea bunge imani.
 
Halafu bi kidude anabaki waliosema NDIO wameshinda, mxiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii upupu mtupu
 
Back
Top Bottom