Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 54,475
- 43,828
Dr. P.W. Slaa na Mr. Zito Z. Kabwe ni wanasiasa mashuhuri hapa nchini.
Pamoja na kuwa Zito ana kasoro zake nyingi tu, bado ni kijana anayeuzika sana kwenye siasa za Tanzania. Ameshajijenga vizuri sana. Kuna siku alimbeza mwenzake Tundu Lissu bungeni, nikaona kuwa huyu jamaa kumbe kweli anatakiwa aekue kidogo. Sometimes busara zinaongezeka kulingana na muda.
Kama Zito kabwe atampisha Dr. W.P. Slaa agombee uraisi uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfanyia kampeni ya dhati, CHADEMA itafanya vizuri sana kwenye uchaguzi. Lakini kukiwa na kutofautiana kati ya Zito na Slaa, basi CHADEMA inaweza ikakosa mafanikio kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Matokeo ya mwaka 2015 yatachangia sana matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Napendekeza, Dr. Slaa aachiwe agombee mwaka 2015 na baada ya hapo akiwa raisi aongoze kwa miaka mitano tu, amuachie Zito, akikosa astaafu siasa, ataheshimika sana kisiasa hapa Tanzania kuliko wale ambao wanasema wamestaafu alafu baada ya muda mfupi wanarudi. Zito pia anatakiwa amrudishe David Kafulila CHADEMA ili washirikiane kuhakikisha Kigoma inakuwa ngome muhimu ya CHADEMA.
Mkuu mwaka 2020 Dr Slaa atakuwa na miaka 95.