Nasikitika sana kuona hadi kipindi hiki cha sayansi na teknolojia kuna watanzania wasiojua kujibu swali au kuchangia mada, nawafananisha na viongozi wanaoingia madarakani na kusahau majukumu yao. Mtoa mada ni binadamu kama mimi na wewe, na sidhani kama alikua na lengo baya kuleta mada kama hii, ni nzuri na inaleta changamoto, cha msingi ni kuchangia kwa kwa ufasaha kama watanzania tulio na akili timamu sio kukurupuka na hoja zisizo na msingi. Nashangaa sana kuona wachangiaji wanaoingiza mada za udini au ukabila.
kURA
Kura yangu naiweka kwa Dr. Slaa
Ni kiongozi mwenye uzoefu wa muda mrefu kuliko Mh Zito,
Umri wake ni ndani ya sheria na si wa kuhitaji tena mambo ya ujana
Si mtu anaependa sifa zisizo na msingi
Hapendi kushukuriwa kwa jambo ambalo ni wajibu wake
Mtoa mada angenipa nafasi ningetoa sababu za ziada ila kwa kuwa aliweka kigezo naishia hapo.