Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.

Jamani huu ni ulinganifu usiyo wa haki. Haiwezakani Kulinganisha milma Kilimanjaoro (Dr Slaa) na Mlima Sekenke (zito).
let's be fair wajameni!
 
ningekuwa sijui ndo mnawaita mods ningempiga ban muanzisha uzi...mbona watu hamna adabu siku hizi?zitto anashindanishwa na lusinde..slaa na obama
 
Zito kwanza atubu ndio apate haki ya hata kufikiriwa na dokta wa ukweli president 2015 dr.slaa.
Baada ya ushindi mnono tunahitaji mwanasheria mkuu awe tundu lisu ashughulikie matatizo yote ya sheria kandamizi zilizo nchini zilizowekwa na magamba.
 
dr.slaa ni mwadilifu, hatumiwi na watu wa ccm kama anavyofanya zito kabwe,leo bungeni karopoka kuwa mwandiko wa tundu lisu na mbaya sana.huyu hawezi kutunza siri hafai kuwa kiongozi wa taifa,bado ananuka maziwa.
 
Viongozi hupatikana kwa kuandaliwa au kuzaliwa. Napenda kusema Dr. Slaa ni kiongozi na anafaa kuwa Rais wa nchi hii
 
ningekuwa sijui ndo mnawaita mods ningempiga ban muanzisha uzi...mbona watu hamna adabu siku hizi?zitto anashindanishwa na lusinde..slaa na obama

Wewe ni nyangema kweli na cyo great thinker, acha umagamba wako manake now days zitto keshakuwa kibaraka wa magamba na hakuna asiyejua hili.
 
kura yangu ni kwa zitto kabwe.kumpa kura slaa labda awe kalani wa mahakama maana siwezi chagua mtu anayefanya kazi kwa kusikiliza majungu na kwa sasa anaendesha chama kwa nguvu ya mchumba wake josephine mshumbuzi.kumchagua slaa ni sawa na kuipa laana nchi yangu maana huyu mzee kila kitu kachelewa mpaka mapenzi kayajulia uzeeni

wewe magamba unapigaje kura huku au umetumwa tu kukivuraga chama chetu? KWANI MBONA JK WAKO AU NAPE WAKO ANA DHAMBI KAMA UNAYOMPAKAZIA RAIS WETU MTARAJIWA?
 
dr.slaa ni mwadilifu, hatumiwi na watu wa ccm kama anavyofanya zito kabwe,leo bungeni karopoka kuwa mwandiko wa tundu lisu na mbaya sana.huyu hawezi kutunza siri hafai kuwa kiongozi wa taifa,bado ananuka maziwa.

Uadilifu ni pamoja na kutochanganyachanganya wake, mambo ya kiimani n.k. Sijui ni nani alipata watoto angali akiwa padri! Mtampa Uraisi then atamwacha mke wa mtu hivi hivi na kupata kimwana mwingine.
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.


Sioni sababu ya kuendelea kulinganisha Mount Kilimanjaro na Kichuguu.
 
Hii nidharau kubwa.Huwezi kupambanisha Barcelona FC na Lipuli ya Iringa.


Wacha weeee molemo, lakini mpira unadunda Lipuli ya Iringa wanaweza kumfunga FC Barcelona. Si unamhonga tu refa halafu anawapa penati? Halafu refa akifukuzwa kazi anapewa mshiko na Lipuli iliyochukua Kombe.Shtuka. Unafikiri Lipuli wanaingia kwenye mechi hawapigi mahesabu???
 
msipime mto na Bahari DR slaaa juuu walahi mkimuweka zito ntampa kura yangu hata LO wa sa
 
watz tuacheni woga kinachotakiwa hapa ni maoni kama huna maoni bora kunyamaza, pia msipende vitu laini laini sometime tujifunze kujenga hoja. Kwa maoni yangu zito anakwalifai kwa kua kwanza ameonyesha kujali maslahi ya umma zaidi ya chama na kwakua tunataka raisi wa tanzania siyo raisi wa chama uyu jamaa anafaa. pili set up yake ya maisha haina madoa madoa kama mzee wetu, embu fikiria saizi raisi anakesi za ndoa mara kaoa mke wa mtu nk kama tukimweka mzee jamaa wa kile chama watapata mwanya wa kutuchafua, tatu zito ameonyesha uwezo wa kusimamia maamuzi ya taasisi ndo maana chati yake inapanda mzee weyu tunampenda sana ila ana staili ya zamani siasa nyingi, mwisho kwa attempt ambazo mzee ameshajaribu nadhani kuna haja ya kuweka kijana presentable mwenye elimu na energy ya kutosha kuendeleza mapambano ili kuleta mabadiliko
 
tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya zitto zuberi kabwe ama wilbroad peter slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na kwa nini? Toa sababu kuu nne tu.
we endelea na propaganda zenu mumeishiwa na 2015 hiyoooo! Chadema ina majembe tupu ndo maana umeanza na hao wawili.
 
Haraka yote hii ni ya nini? Bado tuna miaka miwili mbele yetu ili kufika wakati muafaka wa kuzungumzia wagombea uongozi katika nafasi mbalimbali.
Hii kura ya maoni hapa haitusaidii chochote, sana sana itapalilia makundi ndani ya chama ambayo yanaweza kukivuruga chama na kuondosha mshikamano miongoni mwa wanachadema.

Kama ninavyoshauri kila mara, wanachadema tuachane na hizi sarakasi za uraisi kwa sasa. Tujielekeze katika kujenga na kuimarisha chama ngazi za chini-misingi, matawi na kata kwakuwa huko bado hakuko stable.
Rai yangu kwa wanachadema na wanaoiunga mkono chadema hapa JF naomba tuachane na mijadala isiyo na tija kwa maendeleo ya kisiasa na kidemokrasia. Tusipoteze muda kujadili mambo ya uraisi kwa sasa hakuna tija yoyote kwa mustakabali wa nchi yetu.

Bwana mwita huo ni msimamo wako watu watauheshimu. Nadhani tuwaache watu wawe huru kujadili kila wanachohitaji kujadili. Ndo uzuri wa mitandao ya kijamii. Opinion polls huwa ni muhimu sana ningeshauri wahusika wa JF waongeze hizi polls ziwe nyingi halafu watu wewe wanazichanganua na kutoa reports. Zinasaidia sana kupima upepo na mwelekeo wake. Kama kweli zito na slaa wanafikiria kugombea urais mwaka elfu mbili na kumi ni mbili ni vyema wakajua maoni ya watu ili waanze kuyafanyia kazi. hivyo ni vizuri. Kama unataka na wewe tupime kitu kilete humu badala ya kujaribu kuwanyamazisha watu kutoa maoni yao.
 
Mwanzisha thread hii ana lengo gani kumlinganisha Dr. Slaa na Zitto? au ndio mbinu za kutaka kukivuruga CDM? Nashauri CDM wapuuze kura hizi za maoni kwan kwa vyovyote vile huwezi kumlinganisha dr. slaa na zitto
 
Mwanzisha uzi ungempambanisha Slaa na CCM bana! Sasa hii ndiyo nini? Au Zitto anagombea kwa tiketi ya CCM?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom