Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Nadhani tuanze kujifunza sasa kuwa nafasi ya kugombea uraisi si ya mali ya mtu binafsi....halafu hao unaowasema hawajatangaza nia kiofisi........Je kama tukiamua 2015 ni zamu ya wanawake???........ Mdee...Migiro...Simba...Ghasia. ..Magige...Chana.....Kamata......nadhani ni mapema mno kwa hii poll.....labda kama unakusudio la siri....
 
Nenda mbele rudi nyuma zitto is my choice,ana kura yangu mimi na za ukoo wangu wote,tunasubili tamko lake,
 
katiba inashushwa miaka ya kugombea urais,halafu ndo itajulikana kua maharagwe sio mboga ya kumpaa mgeni!!
 

Hapo kwenye umri na pesa Ndio napatilia mashaka hata Mimi Ndio maana namuona Jamaa Kama mcameroon flani.
 
Kura yangu naipeleka kwa zitto kabwe,sbabu zangu nne ni hizi:

1:Atasaidia sana chadema kuisafisha chadema iondokane na dhana kwamba ni chama cha wakristo

2:Ataisaidia chadema kujivua gamba la ukaskazini kupita kiasi

3:Ataisaidia chadema kuzipata kura za waislam ambao wengi wao chadema si maarufu sana kwao

4:Atarejesha mahusiano ya chadema na vyama vingine vya upinzani kama cuf na nccr kwa kuwa zitto ni chadema moderate,sio conservative kama huyo mzee na mwenyekiti wake hasa ukizingatia kwamba zitto hajawahi kuwa mwanachama wa TANU wala CCM
 

Heshima aliyonayo DR Slaa ni kwasababu tu alikuwa kiongozi wa kanisa na umri alionao kulinganisha na zitto, zitto amekuwa kwenye siasa muda mfupi sana kulinganisha dk Salaa lakini amekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na uwezo wake,amekuwa maarufu sana hayo yote ameyapata muda mfupi tu. Watanzania wengi hatukuwa tukimjua dk Slaa hadi pale alipogombea uris 2010, kwahiyo heshima aliyonayo dk Slaa ipo kidini zaidi kwa waamini wake sio kisiasa, heshima na umaarufu alionao ZZK unatokana na uwezo eake mkubwa ktk siasa, kwahiyo kisiasa zzk yuko juu zaidi kuliko dk Slaa
"Kwa kuwa ‘my conscious is clear', (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli.by ZZK
​
 

wengi wape ' ni kauli dhaifu sana , kama una hoja ya msingi hata kama uko peke yako kwenye jamii simama na uitetee !! ndo wanaoitwa mashujaa hao!! ninavyojua jf ni jukwaa huru usitie dini humu!!
 
Wote wanafaa lakini zito apewe kwanza muda apevuke kisiasa. bado hajabarehe kisiasa.
 
ZzK bado Anawaza As za ud. Bado ana kidmind. Na hili la mshiko wa tanesco.
 
Watanzania msipoweka udini pembeni nadhani mtafika pabaya kwa hali hiyo yakumpenda mtu kwasababu ya dini fulani.mtu unaulizwa ZITTO VS SLAA nani bora , badala kutaja kuchangia mada ya ubora unachangia mada ya udini, huu ni upuzi mtupu
:flypig:
 
Zitto amelewa madaraka na sifa,ni mnafiki na hayuko straight...pia ana uchu wa madaraka...mara nyingi sana amekuwa akienda kinyume na makubaliano ya viongozi wenzake wa chadema..kwa kifupi kanajisikia sana anadhani she is exceptional..hatuko tayari kuwa na kiongozi dhaifu wa namna ya zito....half msisahau kuwa Wema sepetu nie atakuwa first lady...
 
Ni wewe na wengine wachache mno ambao mlikuwa bado mnajua Hayati Mwl Nyerere bado Rais wa TZ ndiyo hamkumjua Dr. Slaa.
Ina maana hata orodha ya mafisadi iliyotajwa pale CDM[SUP]2 [/SUP]haukuijua hadi mwa 2010?.
 
Tuwe tunakuwa waangalifu katika kulinganisha. Kwangu Mimi, Dr.W. Slaa ni Mount Everest, na Zitto ni termite mound (kichuguu cha mchwa).
 
He kumbe wanao vote hapa in Favour of ZITTO wengi ni CCM, Hii inamaanisha nini?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…