Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,399
Kura moja ya raia wa Lindi inabeba uzito kisiasa mara tano kuliko raia wa Dar es Salaam. Kwa nini?
Angalia namba (nazitumia za 2016 na 2010, 2020 sijaona lakini kimsingi ni vile):
Dar es Salaam wakazi 5,465,420 (2016), majimbo ya bunge 10, maana raia 546,000 = mbunge 1
Lindi wakazi 897,533 (2016), majimbo ya bunge 8, maana raia 112,000 = mbunge 1
Wastani kitaifa:
Tanzania bara wakazi 48,676,698 (2016), majimbo ya bunge 214, maana raia 227,000 = mbunge 1
Katika takwimu ya 2016 mikoa iliyohitaji kura nyingi kumpata mbunge 1 ilikuwa: Dar es Salaam, Mwanza, Kagera na Kigoma. Ilikuwa na wakazi milioni 13.7, waliweza kuchagua wabunge 36. Kama wastani wa kitaifa ungefuatwa, wangepata wabunge 60.
Mikoa iliyohitaji kura chache kwa wabunge wao ilikuwa: Iringa, Mtwara, Pwani, Katavi, Njombe na Lindi.
Ilikuwa na wakazi milioni 5.78, waliweza kuchagua wabunge 45.
Kama wastani wa kitaifa ungefuatwa, wangepata wabunge 25.
Kwenye mikoa mingine tofauti kati ya wastani na idadi halisi ya wabunge ilikuwa 1-1 tu.
Ninaiona leo tu. Je imewahi kujadiliwa?
(Chanzo: https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/majimbo/MAJIMBOApril_Kisw.pdf)