Kupotezwa, Kujipoteza, Kujitafuta na Kujipata!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,904
KUPOTEZWA, KUJIPOTEZA, KUJITAFUTA NA KUJIPATA.

Anaandika Robert Heriel.
Kuhani.

Nataka niwe kama Michael Jackson, Umejipoteza.
Nataka niwe Kama Yesu wa Nazareth, umeshapotea Huko.
Nataka niwe Kama Taikon wa Fasihi, umeshapoteza mwelekeo.
Nataka niwe kama Ronaldo, iiishii! Pole Sana.
Nataka niwe Kama Obama, Come one! Unajipoteza.

Huko ni Kujipoteza, huwezi kuwa kama fulani hata Dunia ipinduke, Jambo hilo haliwezekaniki.
Taka kuwa wewe "Be You" hivyo ndivyo tunaanza andiko letu.

Ukitaka kuwa kama Mimi basi huwaga nakushauri Kuwa wewe Kwanza ujione vile ulivyo mzuri, wamoto na Mungu alivyoweka uwezo wa ajabu ndani yako.

Kwenye Maisha kuna Kupotezwa na kujipoteza.
Moja ya sababu za Kupotezwa na kujipoteza ni kutaka kuwa kama Fulani.
Unakuta wazazi wanahangaika Usiku na Mchana usome ili uwe Daktari kama mtoto wa Fulani. Huko wanakupoteza labda iwe na wewe ndio unapenda kuwa Daktari, yaani ukijisikiliza Kwa ndani kabisa unajiona wewe ni Daktari Mkubwa na mwenye uwezo wa kipekee.

Hatuwi tulivyo Kwa sababu ya MTU Fulani alikuwa kama Sisi. Bali tunakuwa tulivyo Kwa sababu tunataka tuwe hivi tulivyo.
Hiyo ndio furaha yetu.

Huwezi kusoma au kutafuta Pesa ili uwe kama Fulani. Bali unasoma na kutafuta Pesa ili KUJIPATA Yule uliyekuwa unataka kuwa.
Upekee wako, uwezo wako, ubunifu wako, mitindo yako ya ajabu hiyo ndio itawafanya Watu wakuone kuwa unakitu cha ziada.

Taikon najaribu kusema, kama kijana unayohaja ya kujua unataka nini kwenye Maisha yako, na nini ukikifanya unajisikia furaha.
Sio nini wenzako wakikifanya unasikia Raha basi nawe ndio ufanye. Kuna tofauti ya kufanya kitu mwenyewe na kufanyiwa kitu. Ni mambo mawili tofauti.

KUJITAFUTA Baada ya kujipoteza au Kupotezwa,
Umepotea katika misitu minene yenye Giza la fikra na umaskini wa kifedha, hujui nini ufanye na kipi kinataka ukifanye.
Unandoto zisizoonekana wala usizozikumbuka pale unapofumbua macho yako, ukiyafumba macho yako unazondoto nyingi lakini ukiyafumbua huzioni, zimetoweka katika anga la juu Sana usiloweza kulifikia.

Maisha Kwa wengi yapo hivi, kujipoteza na Kupotezwa ni Constantly lakini kujitafuta hiyo ni hiyari yako yaani inategemea.
Hata hivyo elewa kuwa Hakuna atakayekutafuta utakapokuwa umepotea au utakapokuwa Umejipoteza au Kupotezwa.

Njia iko wapi, Dira iko wapi?
Dira Ipo katika Nafsi yako, ndani kabisa ya Nafsi yako ndio uelekeo wa Maisha yako ilipo. Macho yasikudanganye Kwa Yale uyaonayo katika Dunia Hii.
Angalia ni kipi Nafsi yako utaweza kukifanya katika Maisha yako ukiwa na furaha.
Kwako furaha ni nini? Ukishajibu swali Hilo Basi utakuwa umejipata.

Ukiona Jambo lolote unalifanya alafu linawafurahisha Watu na kuwasaidia Watu wengi na vile unavyojisikia Raha basi Huko ndiko KUJIPATA.
Ukiona unafanya Jambo lolote uwe NI kazi yako alafu wanaonufaika nalo ni wachache labda ni wewe, na familia yako basi jua bado safari yako ni ndefu Sana.

Kama ni fundi Nguo, basi Shona nguo kiasi kwamba Watu wakikuona wanasema NAAM huyu ndiye Fundi Nguo.
Kama ni fundi Nyumba, unapojenga nyumba basi waseme Hii nyumba imejengwa haswa. Fanya vitu vinavyogusa Watu Kwa uwezo wako WA juu kabisa.
Usijifanye unajua kuangalia Pesa Sana.
Ukiendekeza Pesa hutoipata,
Lakini ukithamini jina na heshima yako basi kuipata Pesa ni rahisi.
Kumbuka Pesa inaenda na inadesturi ya kufuata majina yenye heshima.

Ni Bora kazi usifanye ikiwa unajua itakuharibia jina lako. Huko ni Kujipoteza, au ukiona MTU anakuambia fanya hivyohivyo jua huyo anataka kukupoteza ili ujipe kazi ya kujitafuta.

KUJIPATA, ni kuwa na Matokeo chanya Kwa Watu. Yaani kwenye 100% basi asilimia 70% ya Watu waridhishwe na kazi zako.
Yaani wakuamini kuwa tukimpa Fulani kazi, basi kazi itafanyika Kwa kiwango cha juu Kabisa.

Kama ni mwalimu, basi fanya kazi yako Kwa weledi, yaani mzazi akimchukua mtoto anasema huyu mtoto kweli katoka kwa Mwalimu. Sio unakuwa Mwalimu Zobazoba! Mara nyingi Mwanafunzi anamuwakilisha Mwalimu wake.

Unaweza ukawa umeajiriwa na unalipwa Mshahara mzuri lakini ukawa bado unajitafuta yaani huna unachokifanya na hii inatokana na kulipua lipua kazi. Unakula mishahara ya Bure. Huna jina, huna heshima yoyote. Hakuna anayekuheshimu zaidi ya wale unaowalisha nyumbani kwako.

Unatakiwa MTU akija ofisini kwako kukutana na wewe, ajue kuwa hapa nimekutana na Chuma, fundi, Professional, Master, King, n.k. alafu uone kama hutojipata. Hakuna Raha kama jina lako kuheshimiwa, kukuzwa na kutukuzwa.
Watu wanafanya kazi Kwa weledi kutunza majina Yao.
Kijana, hakikisha Watu wanakuelewa vizuri, Hii itawafanya wakuamini. Ukipewa kazi yoyote jitahidi ulinde jina lako.
Ili jina lako liweze kutukuzwa kama lilivyo jina la aliyekuumba Kwa namna ya ajabu.

KUJIPATA itakusaidia mambo mengi, sio tuu jina lako kutukuzwa na kuheshimika. Bali;
I. litasaidia na kazi yako kufanyika Kwa urahisi.
ii. Biashara zako Kupata Wateja wengi kwani watakuwa recommended.
Hivyo ni sehemu ya Kutangaza soko lako.

iii. Ni rahisi Kupata connection na watu wengine ambao utawahitaji katika harakati zako.
iv. Itakufanya usikilizwe na mawazo yako kuheshimiwa, kuchukuliwa Kwa umakini.
Lakini kama ni MTU wa kulipua lipua mawazo yako Watu watayapuuza.
V. Watoto na familia yako kuheshimika.
Wapo Watoto wanaoheshimika Kwa majina ya Baba na Babu zao.
Sio Kwa sababu ya Pesa Bali Kwa sababu ya majina.

vi. Kuwa na furaha muda mwingi
Ukijipata utakuwa na furaha muda mwingi.
Moja ya dalili ya MTU ambaye hajajipata ni kuwa na Stress, kusumbuliwa na mambo yasiyoisha. Yaani MTU anaweza kuwa na Mshahara mzuri lakini bado akawa anajitafuta yaani Maisha yake hayajatulia.
Haoni Sababu ya kuishi, kila muda anahuzuni.
Lakini MTU akijipata muda mwingi atakuwa na furaha na Amani.

Usiruhusu MTU akupoteze wala usikubali ujipoteze mwenyewe.

a) Fanya mambo yako Kwa mipango
Mipango na malengo yako iwe documented/uwe umeiandika, ifuatilie Kwa umakini ukiwa katika utekelezaji.

b) Amini katika Mchakato, kuwa na Focus
Usitake maushauri ushauri yasiyo na kichwa wala miguu. Hata hivyo usikatae ushauri wa MTU.
Mipango yote uliyoipanga, na mikakati uliyoiweka tembea nayo hivyohivyo. Hakikisha kila ufanyalo ulilipanga na kuliandika hapo Kabla.

c) Usijiingize kwenye mambo yasiyokuhusu.
Usipende kujiingiza kwenye mambo ambayo hayakuhusu Wakati WA utekelezaji wa mipango yako.

d) muda wa kujitafuta uwe umeukadiria vya kutosha ikiwezekana uweka na Akiba ya muda.
Mfano; Mpango wako unahusu Miaka 15 ijayo. Wenye title isemayo;. "Mpango WA kujenga nyumba ya Milioni 100 Ndani ya miaka 15 Kutoka 2020- 2035"
Huo ndio Mpango. Basi utaongeza miaka 2 ya Akiba hivyo itakuwa miaka 17 ingawaje hutoiandika kwenye maandishi.
Miaka hiyo miwili ni kwaajili ya ku-clear Errors zinapokuwa zinajitokeza.

e) Usisikilize Kelele za Chura unapovuka mtoto.
Chura mtoni ni Aina mbili za Watu.
I) Wanaokuzomea na kukukatisha tamaa.
ii) Wanaokuchonganisha na kukuchochea na watu.

Watu wanaokuzomea na kukukatisha tamaa Kwa Yale ufanyayo usiewaendekeze. Hao ni Chura tuu. Ukitaka uwadhibiti katika Moja ya mikakati yako ya kudhibiti vyura basi ni kuwapuuzia na kuwadharau. MTU ukishamdharau na kumpuuza umeshamnyima nafasi ya kuendelea kukuzomea ataacha kukuzomea lakini kama atakuwa na Roho ngumu atakuwa anakusngenya Chini Kwa Chini Kwa chuki. Hiyo ni kawaida.

Kuna wale wa Chura wa kukuchonganisha au kukuchochea unapoingia katika migogoro na watu.
Mpigie huyo, mfukuze huyo Mkeo, Achana na Mumeo huyo hakufai, Nenda Mahakamani, au tupo Nyuma yako endelea kuitukana serikali(wakikuambia hujaitukana Ola umeikosoa) hawa Chura ni wabaya zaidi kuliko Chura wa awali. Wameponza wengi.
Wengi wameachana na wake na waume zao Kwa kuchochewa na vyura. Wengi wamejikuta matatizoni Kwa sababu ya Chura.

Usijifanye unahasira kuliko Busara na hekima. Utapotea na Kupotezwa.
Kabla ya kufanya lolote jipe muda wa kufanya maamuzi.
Maamuzi yanahitaji muda. Sio ukurupuke kama Zuzumaji. Utapotea na kamwe hutojipata.

Jambo likitokea, mwambie MTU ngoja nikatafakari. Nenda kakae Chini ufanye tathmini yako. Kisha kama huna uhakika na Maamuzi yako tafuta MTU unayehisi amekuzidi maarifa ambaye hauna ukaribu naye Sana. Hawa mara nyingi watakushauri ukweli pasipo wivu wala upendeleo. Tofauti na MTU anayekujua.

Wakati miaka inaenda Kwa wengine kwako utaona inaenda Kwa usahili kabisa kwani utakuwa unafanya vitu Kwa mahesabu.

Nakupa mfano No. 1. KIJANA ALIYEMALIZA CHUO ANAJITAFUTA AU KIJANA MWENYE MIAKA 23 ANATAKA KUJITEGEMEA.
Mpango ni kujitegemea.
Lakini lazima tujue Kwa kijana WA umri huu kwake kujitegemea inamaana ipi.
Tumpe jina, aitwe Dayusta.

Kujitegemea Kwa Dayusta maana yake ni kuweza kupangisha chumba kimoja au viwili, kuweza kulipia Kodi, kujilisha, kujivalisha, kulipa Bills kama umeme, maji, ulinzi, usafi, takataka, Vocha na kujinunulia Nguo.
Dayusta akipata hivi kwake atajiona amefanikiwa kwenye Maisha katika umri huo. Bila Shaka atakuwa sahihi.

Lakini Kwa umri wa miaka 30-35 maana yake itabadilika.
Kwani majukumu yataongezeka ikiwemo kutegemewa na Familia atakayoianzisha na iliyomzaa yeye na Mkewe.

Mpango WA kujitegemea utakuwa WA miaka 20 kutokea akiwa na miaka 23. Hivyo jumla atakuwa na miaka 43 mpaka atakapokamisha Misheni hiyo.

Mipango yake na mikakati ndivyo itaunda BAJETI.

1. Mwaka wa 1-3
Dayusta atanunua vitu vya ndani. Ikiwemo Godoro, kitanda, masofa, Majiko, mapazia, mazulia, Luninga, n.k. ndani ya miaka mitatu itamtosha Dayusta kukamilisha chumba alichokuwa anataka kukiita makazi yake Mapya ya kujitegemea.
Hapo atakuwa na miaka 26.

2. Mwaka 4- 7
Dastani atakuwa anaweka mambo yake Sawa ikiwezekana kuongeza mradi mwingine na kujifunza biashara nyingine. Huku akianza kuchumbia Mwanamke kwaajili ya kuanzisha familia Mpya. Hapa atakuwa na Mchumba.
Jukumu litakaloongezeka ni
i. Biashara Mpya
ii. Muda Kwa ajili ya biashara Mpya na Akili ya kujifunza hiyo biashara Kwa sababu haitakuwa inamlipa Bali yeye ndio atakuwa anajifunza.
iii.. Mchumba na kujifunza mahusiano na Mchumba mpya kwaajili ya ndoa.
Hapo atakuwa na miaka 30.
Itapendeza Mchumba akiwa na miaka 20-27

3. Miaka 8 - 12
Dayusta atakuwa anamiaka 34, atakuwa ameoa, ikiwezakana anamtoto mdogo asiyezidi Miaka 4.
I. Biashara ameanza kuielewa.
ii. Jukumu la Ubaba limeongezeka,
iii. Jukumu la kutoa 10% Kwa wazazi kitakuwa ni moja ya majukumu yake.
iv. Ndoto yake Ipo katikati. Ni kama anajipata lakini bado.

4. Miaka 13 - 16
Dayusta atakuwa na miaka 38.
i. Atakuwa na uzoefu WA biashara.
ii. Utulivu wa kiutuuzima utazidi kumfanya azidi kuwa Makini katika mambo yake.
iii. Atakuwa na mtoto wa pili na Mkewe anaweza kuwa na mimba ya mtoto wa tatu.
iv. atakuwa ameshanunua kiwanja mahali aidha kimoja au zaidi.

5. Miaka 17 - 20 ya Mpango.
Dayusta atakuwa na miaka 43.
I. Atakuwa na watoto watatu.
ii. Atakuwa amekamilisha ujenzi. Nyumba.

6. Miaka 2 ya Akiba kama nyongeza ya ku-clear Errors.
Dayusta atakuwa na miaka 45.
I. Atakuwa anakamlisha nyumba yake
ii. Kama alihitaji mtoto mwingine utakuwa ndio muda sahihi kwake.
Hivyo atakuwa na watoto wanne au watatu hivi.
iii. Jukumu la kuwalea wazazi litazidi kuongezeka kwani kadiri siku ziendavyo ndivyo wanavyozidi kuzeeka na nguvu ya kujihudumia wao wenyewe inapungua.
iv. Hapo mtoto wa Kwanza atakuwa na miaka 13-17. Na majukumu yake pia yatakuwa yameongezeka

Mipango sio matumizi, ingawaje Kwa sehemu kubwa vile Watu wapanavyo na wanayoyafanya ndivyo vile uonavyo Maisha Yao Kwa waliowengi.

KUJITAFUTA ni kuyafanya Maisha yako yawe vile yatakavyokupa furaha yako ya ndani. Na sio kuwapa Watu wa nje Furaha.

Nipumzike SASA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Sio kwamba ungeuleta huu uzi siku ya weekend mbona kama leo tumechoka sana na majukumu mkuu
 
ROBERT HERIEL umetema madini mazuri Sana hakika.Ninaamini vijana wakiusoma huu Uzi bila Shaka watakuwa na la kujifunza.
Hongera Sana mkuu kwa juhudi zako za kutuelimisha kila uchao.
May God bless you so much.
 
tawile kaka nmekuelewa sana this year inabid nijitafute niache hzi rat race
 
Kila nikitaka kuacha kuisoma panazidi kua tam mpaka nmeisoma mara tatu,,ubarikiwe mzee.
 
Back
Top Bottom