Mimi sio mtaalam wa lugha kwamba sikuwahi kusoma kitaalam shuleni, ila nimwongeaji nimezaliwa naongea kiswahili hivyo nitakujibu kama mswahili hasa na sio mtaalam wa lugha ya Kiswahili
Mfano #1 "Barua ilipotelea ofisini kwako"
Ni neno sahihi kabisa na dhamira ya kutumia neno "ilipotelea" na sio "ilipotea" ni kutaka kuonesha eneo ambapo hiyo barua ilipotea hivyo uzito haupo tena kwenye barua iliyopetea bali eneo ambalo hiyo barua ilipotea
Mfano #2 "Barua ilipotelea nyumbani kwako"
Itakuwa sio sahihi sana kutumia neno "ilipotea" wakati dhumuni lako ni kusisitiza eneo ambalo hiyo barua ilipotea na asio kupotea kwa barua