Kupombeka na aibu ya mwanamke...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Mwili wa mwanamke huathiriwa haraka na pombe, bila shaka hilo ni jambo linalofahamika kwa wale wanywaji na baadhi ya wasio wanywaji. Mwanamke ana mwili ambao kwa kawaida ni mwepesi kuliko wa mwanaume. Mwili wake pia una mafuta kwa asilimia kumi zaidi ya ule wa mwanaume na maji kwenye mwili wa mwanamke ni kidogo kuliko yaliyoko kkwenye mwili wa mwanaume. Kuwa na maji kidogo hufanya mwili wa mwanamke kushindwa kuzimua pombe inayoingia mwilini mwake haraka .

Naweza nikasema mwanamke ana mwili ambao una kiwango kidogo cha kimeng'enyo cha kuvunjavunja sumu ya pombe mwilini ambacho hufahamika kama alcohol dehydrogenise (ADH). Kwa hiyo, pombe hukaa kwa muda mrefu kwenye tumboni la mwanamke kabla haijabadilishwa kuwa mkojo.Hali hii ndiyo ambayo inasababisha mwanamke kulewa haraka, lakini pia kulewa kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na mwanaume. Hata hivyo, kutokana na mabadiliko ya kihomoni mwilini mwa mwanamke, kuna ugumu kidogo kwa mtu kuweza kutabiri namna pombe inavyofanya kazi kwenye mwili wa mwanamke. Lakini wale wanawake wanaotumia dawa za kuzuia ujauzito au vidonge vya uzazi kama vinavyofahamika, huwa wanalewa haraka zaidi na pombe hukaa mwilini kwa muda mrefu zaidi.

Hata kwenye maradhi yanayosababishwa na pombe, wanawake wanaonekana kuathirika haraka zaidi. Kwa mfano, maradhi ya ini hushambulia zaidi wanawake kuliko wanaume, hata kama wote wanakunywa kiwango sawa cha pombe. Bila shaka utashangaa ni kwa nini nimeanza kwa kuzungumzia pombe, tena kwa mwanamke. Nimeamu kuzungumzia pombe kwa wanawake kwa sababu, siku hizi idadi ya ushawishi wa kimakundi unaowahimiza wanawake kuingia kwenye ulevi umekuwa mkubwa sana. Wanawake kwa wanawake wanashawishiana sana kunywa pombe, wanaume wengi zaidi wanawashawishi wanawake kunywa na hata matangazo ya biashara yanafanya hivyo.


Kwa kuangalia matangazo ya biashara ya pombe, mwanamke hujikuta akiamini kwamba, pombe inaweza kumpa hisia tofauti, kumpa moyo wa kutenda asiyoweza kuyatenda na kumfanya aonekane ni wa kisasa zaidi. Lakini wanaume huwashawishi wanawake kunywa pombe kwa sababu, wanataka kutumia pombe hiyo kama mtego wa kuwanasa kirahisi. Kwa nini nasema hivyo, ni kwa sababu tafiti nyingi zinazohusu madhara ya pombe kwa wanawake, zinaonesha kwamba, matukio mengi ya kubakwa kwa wanawake na kudhalilishwa kwa aina mbalimbali, yanatokea kwenye mazingira ya pombe.
Lakini sio hivyo tu, utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Duke unaonesha kwamba, wanafunzi wa kike wanapokunywa pombe, hupoteza uwezo wao wa kushika masomo na hata kuvuta kumbukumbu ya kile walichokisoma.

Lakini pia wamegundua kwamba, pombe huongeza kiwango cha uwezekano wa mwanamke kupata kansa ya titi. Hivi sasa, pombe inahesabiwa kama kitu ambacho kinaweza kusababisha kansa kama ilivyo asbestos, benzene na vitu vingine vya aina hiyo.
Haja yangu siyo kumtisha mwanamke, bali kumwambia kwamba, akienda kunywa pombe, ajue kwamba, anapalilia ama kuandamwa na mambo gani. Tafiti zinaonesha kwamba, pombe ina mchango mkubwa katika kusababisha kujamiiana kusikopangwa na ubakaji. Kwa mjini, mwanamke ambaye anakunywa pombe, akikwambia hajawahi kufanyiwa jaribio la kufanyishwa mapenzi bila hiari yake, ni lazima atakuwa ananywea nyumbani kwake tu au anakunywa na mtu ambaye wanajuana na ni wapenzi na hakuna jipya kati yao.

Lakini hata kwa wapenzi wanaofahamiana kwa kila kitu ubakaji umeelezwa kutokea miongoni mwao.
Pombe hutumika kama sababu au kama njia ya kuhalalisha klitendo cha kujamiaana, ambacho hakikupangwa au hata kubakwa. Wakati mwingine ni kweli, mwanamke alionesha kukubali kushiriki tendo, lakini kilichomuongoza ni pombe na siyo utashi wake wa kiakili. Mwanamke akishakunywa kiasi fulani cha pombe, anakosa uwezo wa kujua au kuona dalili za kufanyiwa unyama kutoka kwa mwanaume. Kuna wakati uwezo wa kukataa iwe kimwili au kisaikolojia unakuwa umepotea.Pombe huharibu uwezo wa kuamua na kuhukumu kwa mnywaji kuhusiana na tendo la ndoa.

Hivyo watu wanapokwenda kunywa kukiwa na wazo dogo tu la kuhusu kujamiiana, wazo hilo hukuzwa sana na wanywaji baada ya kuaza kulewa. Hapo ndipo ambapo vurugu na udhalilishaji hutokea. Wanawake wanaokunywa pombe wanajua wanavyoamka asubuhi wakiwa na aibu na hali ya kuhisi dhaliliko kwa vitendo vilivyotokea usiku wakati wa kunywa. Wale wanaokunywa kwa kupewa ‘ofa' na jirani au rafiki wa kiume au wanaume wanaotaka kujenga nao urafiki, wengi huja kujutia jambo hilo. Takwimu zinaonesha kwamba nusu ya wanawake wote wanaoambukizwa maradhi ya zinaa, huambukizwa maradhi hayo wakati wakiwa wamekunywa, ambapo uwezo wao wa kujikinga huwa chini sana.
 
Najua hapa kutazuka zogo kutoka kwa wanawake.............Ngoja niingie mitini mapema.
 
Kabla hujaingia vichakani dingi, wanaume wanaolewa hawaambukizwi magonjwa ya zinaa? Takwimu za hosp zinaonesha wanawake zaidi kwa sababu wanaume huwa hawaendi hosp. Akiambiwa vipi mbona naumwa, anajibu kwa hasira ili asiulizwe. Mama akifika hosp wanampa dozi ya baba pia (nimeshuhudia hii...).
 
mwanamkee mlevi ni tatizo lisilobebeka.
wanawake walevi wengi wao wameshafanyiwa mchezo mchafu

mwili wa mwanamkee haustahili kabisa kuingizwa mipombe
 
mwanamkee mlevi ni tatizo lisilobebeka.
wanawake walevi wengi wao wameshafanyiwa mchezo mchafu

mwili wa mwanamkee haustahili kabisa kuingizwa mipombe

Mlevi na mnywaji nafikiri kuna tofauti hapo au nakosea Maria? Najaribu kulink na hicho ulichokiita mchezo mchafu!
 
Kabla hujaingia vichakani dingi, wanaume wanaolewa hawaambukizwi magonjwa ya zinaa? Takwimu za hosp zinaonesha wanawake zaidi kwa sababu wanaume huwa hawaendi hosp. Akiambiwa vipi mbona naumwa, anajibu kwa hasira ili asiulizwe. Mama akifika hosp wanampa dozi ya baba pia (nimeshuhudia hii...).
Haya mambo hayakuhusu, umefikaje humu..................unajua nitakuchapa wewe leo ukirudi nyumbani...........!

Inawezekana uliyoyasema yakawa na ukweli, lakini hebu tuangalie, hivi kama wanawake wasingekuwa wanakunywa pombe, si ingekuwa rahisi kwao kuchukua tahadhari, na muendelezo wa mduara katika kuambukizana maradhi ya zinaa ungekuwa ni mdogo.
pili, hivi ni nani anayeadhirika kati ya anayebakwa na anayebaka................Ni nani anayeingia kwenye fedheha? wakati mwanamke akiumia kwa sononi baada ya kubakwa, mwanaume anatembea kifua mbele huku akijisifu.......'nimemkomesha mwanamke yule, alikuw aakiringa sana'....................LOL
 
Sasa Baba tukuzushie zogo kisa umetuelimisha?! Si tutakuwa hatunazo jamani?
Aksante kwa somo hili. Ubarikiwe
Kuna wangu watatu humu (sitawataja leo maana wanajifahamu) huwa wananipa presha kila nikiweka mada.
Na ndio maana nimekuwa nikiwaogopa sana.
 
Hii maneno nilioteshwa jana usiku.................... Si unajua Maruhani yalivyo na nguvu.......LOL
Huyu Ngina kwa kweli nafikiria kubadili jina lake maana kila siku lazima anikwaze................Haya bwana salamu zitamfikia.

chonde chonde baba Ngina badili tu hayo ya wengine wanao sijui Ngani,Ngabu unajua wewe usiguse Ngina.
 
Hii maneno nilioteshwa jana usiku.................... Si unajua Maruhani yalivyo na nguvu.......LOL
Huyu Ngina kwa kweli nafikiria kubadili jina lake maana kila siku lazima anikwaze................Haya bwana salamu zitamfikia.
Khaaaaaa!
Kumbe kila siku uajidai huwa unaongea na malaika wanakupatia hizo habari kumbe ni maruhani???!!!
Maruhani ndio nn baba?
 
Heshima yako baba,
Asa mbona haya hukuniambia mapema mm wanao mpendwa,
Mpaka nakuja kusoma huku somo zuri na la maana km hili?
Any way nashukuru kwa vile unajua kbs mwanao sio mlevi!
 
Khaaaaaa!
Kumbe kila siku uajidai huwa unaongea na malaika wanakupatia hizo habari kumbe ni maruhani???!!!
Maruhani ndio nn baba?
Mwanangu naomba hii iwe ni siri usije ukamwambia mama yako eh!
Maruhani kwa mujibu wa Kamusi ya Kilugha chetu ni Jini Mahaba, ambaye ni mwanamke mrembo sana ambapo akikutokea kwenye ndoto anakwambia mambo mengi kwa Semi, Tafsida na Tamathali. Kiinachotakiwa ni kipaji cha kudadavua ili ujue ujumbe uliomo ndani ya ndoto hiyo. Kuna wakati anaweza kukutafutia mwanamke wa nje ya ndoa na usipomuomba utukufu mwanamke huyo anakupa adhabu. mie huwa naomba ili nisipewe adhabu..................... Si unajua mimi Baba yako nimuoga wa adhabu!
 
Back
Top Bottom