masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Bunge la Ulaya limeazimia kuufuta mradi wa bomba la mafuta toka Uganda hadi Tanga Tanzania.
Sababu za kitoto wanazotoa ati ni uharibifu wa mazingira na haki za binadamu!!
Huu ni uhujumumu wa moja kwa moja kwa uchumi wa nchi za kiafrika zinazotaka kujikomboa katika umasikini kwa kutumia malighafi zilizo katoka nchi zao.
Unafiki wa EU unaonekana wazi kabisa.
Tanzania enzi za Mwalimu Nyerere tulijenga bomba la mafuta la TANZAM, bomba hili linafanya kazi hadi leo hii.
Lakini kwa vile mafuta hayo yanatoka kampuni zao, huko ni kimya kabisa.
Vile vile leo hii EU inalilia bomba la gesi toka Urusi lisizimwe ili nchi zao ziendelee kupata gesi kuendesha uchumi wao.
Nchi hizi za Ulaya, EU, wnapendelea nchi za kiafrika ziwe tegemezi kwao daima dumu.
Tanzania lazima tulaani msimamo huu wa EU na bunge lao.