Kupigwa Marufuku Makanisa ya Kilokole, Gwajima amjibu mkuu wa mkoa wa Arusha, ni mtoto wa Dawa

kenzi

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
425
461
Baada ya mkuu wa mkoa wa arusha kusema kuwa makanisa ya walokole yadhibitiwe kwa kuwa wanapiga kelele (Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa)

Gwajima ameamua kumjibu mkuu huyo

Amesema kuwa Tanzania ni nchi huru kila mtu ana haki ya kuabudu, muda wowote na wakati wowote

Amesema kuwa waumini wa madhehebu ya kilokole wako milioni, kwa hivyo huwezi kuwazuia.

Apinga agizo hilo la mkuu wa mkoa wa Arusha
 

Attachments

  • AUD-20160412-WA0001.mp3
    730.2 KB · Views: 155
kwingineko duniani: Gwajima acha ubishi tanguliza busara
Pastor Gets Jail Time for Noisy Church
Gospel church fined because singing and preaching was too loud for neighbours
California Church Threatened With $500 Per Day Fine After Gospel Choir Accused of Excessive Noise — but They’re Fighting Back
Church Noise – Welcome to the Church of Noise
Is this Louisiana church's service too loud? Yes, authorities say
Oakland church gets warning after neighbors complain of choir noise
Lagos shuts religious houses, hotels over noise pollution
NEMC bado hawajatoa sheria ya kupambana na huu usumbufu, ila lazima itakuja na kunakuwa na maximum tolerable Volume kwa makanisa,night clubs,misikiti, viwanda,mikutano,matangazo ya barabarani na nje ya hapo unashtakiwa na kulipa faini au kufungwa.

inabidi kuwa na kiasi,
waislamu wanawaita wenzao waje kuswali sioni shida(ila kama wanakera pia wawemoderated). Mabar yapigwe marufuku au wawekewe limit ya sauti,
Kuhusu walokole inabidi wawe na kiasi, Kama unamuomba na kumsifu Mungu wako aliye sirini kuna haja gani ya kupaza sauti kwa wasiohusika. Tena saa nane usiku masaa kadhaa non stop.

Mkuu wa mkoa amekuwa biased kwa kusahau wapaza sauti wengine, hii haiwafanyi walokole wanaopiga kelele sana usiku kuwa na uhalali wa kuwazuia wananchi wengine wasilale. Hekima inahitajika. Sheria iwekwe yenye limit ya sauti. na ukivunja uwe ni mlokole,muislamu,disko,mdundiko mimi kama jirani nikushtaki unilipe fidia ya kunisumbua usiku nishindwe kupumzika kesho nifanye kazi kwa ufanisi offisini.

Pia bibilia inawataka watu wa dini kuwaheshimu viongozi wa serikali hata kama wanamapungufu. kumuita muwakilishi wa rais kwa kejeli mtoto wa dawa au kumfananisha na jini Mungu hakubaliani na udhaifu huo. Hapo mtumishi kateleza atutake radhi.
 
Basi sawa .....


Haya maneno haya. .....Mtoto wa dawa. ....

Mungu naomba uwape watumishi wako hekima.
We umeelewaje hiyo kauli? mie sikuona tatizo na kauli hiyo imejaa hekima.. MTOTO WA DAWA ina maana yake sema ufafanuzi wake tumeelewa tofauti; wenye hekima ya kimungu wameipata loud and clear. USINIULIZE MANA KWA MITAZAMO YETU TUTABISHANA MPAKA KESHO!!
 
Back
Top Bottom