Kupigiana simu kwa wanandoa

Kupigiana simu kwa wanandoa

Sijui kuhusu yeye kama kuna shida mahala ama lah!!

Binafsi mimi ni mvivu kinoooma kupiga simu, huu ni udhaifu wangu, kuongea muda mrefu kwenye simu naona tabu,
Mke wangu yupo km 500 kutoka nilipo mimi, anajua kuwa hilo ni tatizo langu, imebidi siku hizi awe ananikumbusha fulani umewasiliana nae, umemjulia hali, haya wasiliana nae sasa hivi unipe mrejesho.

Kwake imekuwa si tatizo katika mara 20 tutakazo ongea kwenye simu basi mara 19 kapiga yeye, akiwa likizo kwa siku anaweza piga simu hata mara 5.
Nikimpigia anafurahi kuwa naanza badilika kwa ajili yake, ila nisipopiga sio kesi anajua ndio udhaifu wangu.

Kwanza ngoja nimpigie mara ya mwisho kupiga mimi ni majuzi aliponitxt nimpigie salio limeisha
Basi kama ni hivo iwe hivohivo hata kwa michepuko maana huko ndo unakuta unapiga masaa mawili
 
Hili jambo mie lilileta ugomvi sana.

Kimsingi mie ni mvivu sana kupiga simu. Napiga simu tu pale ambapo naona ni muhimu kwangu. Kwa mfano nikisafiri napiga simu asubuhi kuuliza wameamkaje na mipango ya siku.

Baada ya hapo nitapiga simu usiku kuwa mmeshindaje na kiujumla mambo yalikuwaje?

Hili alikuwa hapendi but alikuja kuzoea. Mie mpaka wazazi wanajua hivyo.
Bora hata wewe unapiga hizo mbili yeye hapigi hizo mambo zote ni through chatting
 
Piga wewe simu, hakuna kitu mwanaume anafurahia km wewe kuonyesha kumjali, wewe haupigi simu dakika zako unampigia nani?

Ungeanza kujiuliza hilo swali wewe mwenyewe ujijibu alafu ndio ulilete humu.
Mm nampigia karibia sm zote tunazoongea ni mm napiga
 
Habarini za asubuhi wakuu, natumai ni wazima sana. Leo nina swali kwa wanandoa au wenye mahusiano ya mbali, mimi mume wangu siyo kwamba anafanya kazi nje ya mkoa ila amesafiri kikazi kwa muda tu ana kama karibia miezi 2.

Ila mwenzangu huyu hapigi simu ni ujumbe tu, sasa mimi hicho kitendo kinaniudhi sana na akipiga kidogo utasikia dk. zimeisha, sasa najiuliza dk. zimeisha anaongea na kina nani?

Sasa swali langu kwa wanandoa hasa wenye upendo na wake/waume/wapenzi wao, wanaweza kaa hata siku 3 bila kumpigia simu mwenza wake, yaani ni kawaida au kuna shida pahala?

Naomba maoni yenu hasa kwa wanaume waliokuwa makini na wake/wapenzi wao, namaanisha wenye upendo wa Agape.
Duuuh.. Okay binafsi nafikili ilo tatizo hutokana na vitu viwili moja tabia, wapo watu hiyo ni tabia yao yani hata nikikuliza swali apo kuwa iyo hali ilikuwepo hapo nyuma kama itakuwa katika upande huu wa tabia nadhani jibu utalipata and jambo la pili ni upendo, mahusiano ya kimapenzi ni kitu tata sana na ni tatizo kubwa katika wakati wa awali pale ndo shida huanzia kama ulingia kwenye mahusiano kwa tamaa tuuy bila ya kupendana kweli huwa tatizo sana kwa mwenza wako lkn kama mnapendana kweli mapenzi ya dhati hutoweza kuwa kimya kwa kipindi kilefu bila ya mawsiliano na mwenzawako never.. Japo kuwa kwenye mausiano kuna changamoto lkn hali iyo haitadumu kwa kipindi kilefu.
 
Anakujali? anakuthamini? anakutunza kama mkewe?

If yes then chukulia kama hiyo ndo weakness yake as hujaolewa na malaika mama, akitext mjibu ukimiss kuongea nae wewe mpigie maadam hajakukataza kumpigia mana hiyo ndo ingekua mbaya!

Vinginevyo unajitafutia vidonda vya tumbo mama!
 
upendo wa agape kwa binadamu ni haipo.

But kiukweli hiyo hali unayopitia ni ngumu. sometimes wanaume tuna mambo mengi sana kichwani, usipokuwa msaada kwenye mambo yangu, mwisho ni ukimya kama huo.
Msaada kvp
 
Ulishajaribu kumpigia akagoma kupokea/kuongea kwa muda huo mrefu unaotaka? Ama unasubiri upigiwe tu?
 
ndio mara yake yakwanza kufanya hivyo??

kwa ukawaida wanaume wengi hasa mkishakua mmeoana wavivu kupiga simu, mimi mume wangu akiwa nje ya nyumba yake akikupigia sim asbh mchana na usiku imetoka tena saa zingine usiku atakuuliza hali zetu hakuna la ziada ni usiku mwema wife imetoka had asbh

unamjua mumeo kuliko yoyote hayo mawazo chonganishi usiyape nafasi kabisa wewe kama anakumbuka hata kukusalimia ujue anajali kuhusu wewe shida angekua hakutafuti kabisa

zoea tu ukiona inakupa gagaziko ongea naye mueleze ukweli mpe muda pengine atabadilika
Asante sana
 
Ngoja nijaribu kukupa ushauri mdogo tu, kwanza hakuna formula katika haya mambo kwa maana hakuna hili sawa na hili sio sawa. Wanandoa kawaida mnajuana tabia kwa mambo mengi na simu mojawapo unaweza kujuwa mwenzako anapenda nini na tabia zake ni zipi. Wako watu hawapendi kuongea sana tu sio kwa sababu hawana mapenzi. Lakini pia kuna watu wanakimbia maongezi kwa kuogopa kusikia jambo labda huwa halipendi kusikia na wewe ndio kwanza unamwambia wako watu wanakimbia majukumu. Lakini kikubwa je hizi ni tabia zake au ni kitu kipya? kama ni tabia zake basi puuzia kama ni tabia mpya ni vizuri ukamuuliza kwa vizuri tu au wewe mpigie uone atatoa sababu gani za kukata maongezi lakini na maongezi yawe mazuri sio mtu akisikia simu tu anaogopa nini tena? anaona kama gubu hivi maongezi matamu taratibu atarudi kwenye mstari. Kwa ufupi hakuna formula kuna watu wanaongea hata mara 4 kwa siku na wana cheat na wako mara moja wako vizuri tu wewe amua formula yenu ya mawasiliano usi copy ya mwingine.
 
Duuuh.. Okay binafsi nafikili ilo tatizo hutokana na vitu viwili moja tabia, wapo watu hiyo ni tabia yao yani hata nikikuliza swali apo kuwa iyo hali ilikuwepo hapo nyuma kama itakuwa katika upande huu wa tabia nadhani jibu utalipata and jambo la pili ni upendo, mahusiano ya kimapenzi ni kitu tata sana na ni tatizo kubwa katika wakati wa awali pale ndo shida huanzia kama ulingia kwenye mahusiano kwa tamaa tuuy bila ya kupendana kweli huwa tatizo sana kwa mwenza wako lkn kama mnapendana kweli mapenzi ya dhati hutoweza kuwa kimya kwa kipindi kilefu bila ya mawsiliano na mwenzawako never.. Japo kuwa kwenye mausiano kuna changamoto lkn hali iyo haitadumu kwa kipindi kilefu.
Mawasiliano yapo hapa naongelea call na sio sms au whatsapp yaani ukae useme kweli nimemiss sauti ya mke wangu ngoja nimpigie
 
Ulishajaribu kumpigia akagoma kupokea/kuongea kwa muda huo mrefu unaotaka? Ama unasubiri upigiwe tu?
Hii ndo Shida ya wanaume mkishapata mnachotaka mbona wakati unamtongoza mkeo hukusubir akufuate akutongoze mwenyewe?
 
Habarini za asubuhi wakuu, natumai ni wazima sana. Leo nina swali kwa wanandoa au wenye mahusiano ya mbali, mimi mume wangu siyo kwamba anafanya kazi nje ya mkoa ila amesafiri kikazi kwa muda tu ana kama karibia miezi 2.

Ila mwenzangu huyu hapigi simu ni ujumbe tu, sasa mimi hicho kitendo kinaniudhi sana na akipiga kidogo utasikia dk. zimeisha, sasa najiuliza dk. zimeisha anaongea na kina nani?

Sasa swali langu kwa wanandoa hasa wenye upendo na wake/waume/wapenzi wao, wanaweza kaa hata siku 3 bila kumpigia simu mwenza wake, yaani ni kawaida au kuna shida pahala?

Naomba maoni yenu hasa kwa wanaume waliokuwa makini na wake/wapenzi wao, namaanisha wenye upendo wa Agape.
Njoo dm
 
Hii ni ndoa changa naona, wazoefu tunajua.
 
Back
Top Bottom