Kupigiana simu kwa wanandoa

Kupigiana simu kwa wanandoa

Habarini za asubuhi wakuu, natumai ni wazima sana. Leo nina swali kwa wanandoa au wenye mahusiano ya mbali, mimi mume wangu sio kwamba anafanya Kazi nje ya mkoa ila amesafiri kikazi kwa muda tu ana kama almost 2 months.

Ila mwenzangu huyu hapigi simu ni sms tu sasa mimi hicho kitendo kinaniudhi sana na akipiga kidogo utaskia dk zimeisha, sasa najiuliza dk zimeisha anaongea na kina nani?

Sasa swali langu kwa wanandoa hasa wenye upendo na wake /waume /wapenzi wao wanaweza kaa hata siku 3 bila kumpigia simu mwenza wake yaani ni kawaida au kuna shida pahala?

Naomba maoni yenu hasa kwa wanaume walioko serious na wake/wapenzi wao I mean wenye upendo wa Agape.
Anakupenda kawaida tu hyo. Kiufup... Ukiona mapenz hayana mawasiliano mazur ujue kuna shida... Hzo sabab sjui mtu hapend kuongea na sim bla bla ni kujitoa ufaham tu ila kiukwel ni kwamba mtu mnaependana na kujaliana mtapigiana na kuwasiliana... Mbona mkiwa mnatongozana na kutakana au kipind cha u bf na u gf mlikua mnapigiana.. why now.. ushajiuliza?
 
😅😂😬 upendo wa agape kwa binadamu ni haipo.

But kiukweli hiyo hali unayopitia ni ngumu. sometimes wanaume tuna mambo mengi sana kichwani, usipokuwa msaada kwenye mambo yangu, mwisho ni ukimya kama huo.
 
Habarini za asubuhi wakuu, natumai ni wazima sana. Leo nina swali kwa wanandoa au wenye mahusiano ya mbali, mimi mume wangu siyo kwamba anafanya kazi nje ya mkoa ila amesafiri kikazi kwa muda tu ana kama karibia miezi 2.

Ila mwenzangu huyu hapigi simu ni ujumbe tu, sasa mimi hicho kitendo kinaniudhi sana na akipiga kidogo utasikia dk. zimeisha, sasa najiuliza dk. zimeisha anaongea na kina nani?

Sasa swali langu kwa wanandoa hasa wenye upendo na wake/waume/wapenzi wao, wanaweza kaa hata siku 3 bila kumpigia simu mwenza wake, yaani ni kawaida au kuna shida pahala?

Naomba maoni yenu hasa kwa wanaume waliokuwa makini na wake/wapenzi wao, namaanisha wenye upendo wa Agape.
Nikuambie tu Mkuu, kama mnawasilianakwa namna hiyo inatosha. Mambo ya ndoa yanautata sana, kuna jambo ambalo nyie mnavyolifanya na mnaliona la kawaida na huenda upendo upo ila mtu mwingine hapa JF atakuambia oooh mara unaibiwa mara blah blah..! Kwahiyo kama mnawasiliana kwa namna hiyo na hakuna shida nyingine acha kuyakuza bidada.

Jambo jingine nikuombe wewe na wanawake wenzako, kwa asili nyie wenzetu huwa mnapenda kutendewa zaidi ila kwenye kutenda ni zero. Nianze na jambo la kupigiana simu, hivi kwenye mahusiano kuna mahali imeandikwa mwanaume tu ndio anatakiwa kupig simu?? Unapoona yulo kimya jiunge dakika mpigie muongee vya kutosha sio lazima wewe tu ndio upigiwe. Hii tabia haya mke wangu anayo, niliwahi kumwambia wazi kama nimivyoandika hapa. Nashukuru Mungu amebadilika. Huwa anapiga tunaongea vya kutosha tu na mimi ikitokea ninazo dakika nampigia bidada tunaongea mpaka dakika zinaisha.
Sasa wewe ukiona yuko kimya, jiunge dakika 100 za mitandao yote alfu mpigie.
Alfu kusema, hizo dakika zinaloisha unajiuliza anaongeaga na nani zinaisha!?? Hivi kwanj kwenye simu yake ipo namba yako tu!?? Acha wivu wa kishamba utakufa mapemA na nimeona unapenda kuyakuza mambo, ohooo utaugua pressure muda si mrefu.
 
Habarini za asubuhi wakuu, natumai ni wazima sana. Leo nina swali kwa wanandoa au wenye mahusiano ya mbali, mimi mume wangu siyo kwamba anafanya kazi nje ya mkoa ila amesafiri kikazi kwa muda tu ana kama karibia miezi 2.

Ila mwenzangu huyu hapigi simu ni ujumbe tu, sasa mimi hicho kitendo kinaniudhi sana na akipiga kidogo utasikia dk. zimeisha, sasa najiuliza dk. zimeisha anaongea na kina nani?

Sasa swali langu kwa wanandoa hasa wenye upendo na wake/waume/wapenzi wao, wanaweza kaa hata siku 3 bila kumpigia simu mwenza wake, yaani ni kawaida au kuna shida pahala?

Naomba maoni yenu hasa kwa wanaume waliokuwa makini na wake/wapenzi wao, namaanisha wenye upendo wa Agape.
Tunakupa maoni ili iweje? Unataka kumrekebisha mume wako? Anza kwako. Ukiamka asubuhi mpigie simu kwa zaidi ya dakika 20. Siku ifwatavyo fanya hilo zoezi. Atakuja kujitambua. Umuhimu wako. Lasivyo mnapotezeana muda bila malengo
 
Aisee Mimi Hakuna kitu kinaniboa Kama kupiga piga na kupigiwa pigiwa Simu, hata juzi Kati Kuna demu nimezinguana naye alinipigia simu Mara 5 nikakausha Mara zote,Kuna muda nilikuwa namuahidi nitampigia simu kumbe ndo imetoka hio hatokaa aone Simu yangu.
 
Mi tulianza ivoivo mpaka penz likafa, yaan anaanza simu, atakuja kukaa miez 6, mwisho atakuja na sababu nachoka sana ivo ndo maana sijisikii kusex Leo.

Watu hubadilika
Tafuta kibenten akuondolee utoko, itaziba alfu uugue ufe uzikwe ikiwa nzima ina kilometa chache.
 
Naomba niwe nakupigia mimi kila baada ya muda kidogo,uta enjoy sn
 
ndio mara yake yakwanza kufanya hivyo??

kwa ukawaida wanaume wengi hasa mkishakua mmeoana wavivu kupiga simu, mimi mume wangu akiwa nje ya nyumba yake akikupigia sim asbh mchana na usiku imetoka tena saa zingine usiku atakuuliza hali zetu hakuna la ziada ni usiku mwema wife imetoka had asbh

unamjua mumeo kuliko yoyote hayo mawazo chonganishi usiyape nafasi kabisa wewe kama anakumbuka hata kukusalimia ujue anajali kuhusu wewe shida angekua hakutafuti kabisa

zoea tu ukiona inakupa gagaziko ongea naye mueleze ukweli mpe muda pengine atabadilika
 
Mi tulianza ivoivo mpaka penz likafa, yaan anaanza simu, atakuja kukaa miez 6, mwisho atakuja na sababu nachoka sana ivo ndo maana sijisikii kusex Leo.

Watu hubadilika
Mm tunawasiliana through sms lkn no call yaani hata ile kumiss sauti ya mke wake?
 
Back
Top Bottom