Kupigana mabusu kila mara hadharani ni mapenzi au ushamba

Kupigana mabusu kila mara hadharani ni mapenzi au ushamba

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,789
Reaction score
7,174
Wanajamvi,

Kumekuwepo na vitabia vingi vya kuiga toka kwa wenzetu lakini hili lina kila dalili za wazi za wizi kwa wapendanao, utakuta mwanana dada mpo naye kwenye hazara , akiwa na mumewe kila dakika 20 anamgeukia na kumpiga busu, wakati mwingine hata kudendeka, hii hali imekuwa kero sana ya wakina dada kujishetua kuonyesha wanajua kupenda sana wawapo kwenye hazara, au ni utambulisho wa kujionyesha kuwa tayari dume hili lishamilikiwa?

Hali hii inawatokea sana hasa wasanii wa TV , Video, Miziki na Watangazaji, hivi jamii hii ndio wanaojua mapenzi peke yao mpaka wawe wanayaonyesha kila saa?
 
Ni ushamba tu na ulimbukeni huo mapwnz ni faragha zaid ya hp ni ujinga
 
Ni ulimbukeni na kuiga tamaduni zisizo faa. Na anayetetea ni limbukeni pia kama wako wasiwasi wa nini kufanya mambo ya faragha hadharani?au umekopeshwa umuumize mtu roho?
 
Abroad Kawaida sana,mpaka mate kwa raha zenu na watu wanakatiza hapo hapo hakuna anayeshangaa,ila kibongo hata ukiwa na mpenzi wako utashangaa wengine wanaangalia
 
Hali ni Sasa na kuweka ngao kwenye chandarua mbu wasisogee. Au ni kutoa onto kwamba huyo mtu tayari anamilikiwa
 
ni mapenzi maana hawana haja ya kuficha , wewe unataka wafiche kwani inakuuma nini? au ulikuwa ukimtamani huyo mwanamke
 
mi cpend show zakijinga hadharani watu wanaopendana inajulikana tu wanavyokula/kunywa walivyo tu kila mtu kumjali mwenzie
 
Abroad Kawaida sana,mpaka mate kwa raha zenu na watu wanakatiza hapo hapo hakuna anayeshangaa,ila kibongo hata ukiwa na mpenzi wako utashangaa wengine wanaangalia

Hii kitu hata mim hua inanikeraga sanaa...ila vile wakiniangalia na mimi huku nazidisha madoido watajuaje nimedata bila kuwaonyesha
 
Lkn kwa wabongo wengi wao ni wale wanaoachwa, hivyo hupenda kuwaonesha watu hadharani ili wawasimulie wale waliowaacha kuwa kapata mtu anayempenda
 
Back
Top Bottom