Mikopo Chefuchefu
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 3,373
- 6,756
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).
Suala hili huenda ndio limetugharimu kwa kusababisha ajali nyingi za malori hasa kwenye miteremko mikali.
Unaposhuka mteremko mkali gari ikiwa free, na kutumia breki ya kawaida, hufika hatua gari kuishiwa upepo, na hapa shida ndipo inapotokea.
Iwapo kama dereva angeshuka huku gari ikiwa kwenye gear, revolution za engine huwa juu na hivyo gari huwa linakuwa na upepo wa kutosha wakati wote.
Kama Lori likiendeshwa inavyostahili, nina uhakika hakuna lugha ya lori kufeli breki.
Katika magari ambayo uwezekano wa kufeli breki ni mdogo, basi ni haya malori. Gari lenye axle sita, linaanzaje kufeli breki axle zote? Haya malori kwanza yana breki za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi wakati wote.
Hivi inawezekanaje breki zote hizi zikafeli kwa wakati mmoja? Uwezekano wa kufeli kwa breki zote hizi kwenye roli ni asilimia 0.00%.
Serikali itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali kwenye miteremko ya milima ya Mbeya na Songwe pia iwapo itaweza kutega kamera (za kubaini revolution za engine) kwenye maeneo ya miteremko kubaini maroli ambayo yatakuwa yanateremka yakiwa kwenye free gear.
Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!
Kama mabasi tumefanikiwa kuyadhibiti, maroli hayawezi kutushinda!
Iwapo kuna uwezekano wa kufunga ving'amuzi vitakavyoweza kutusaidia kubaini roli linalotembea kwenye free gear, Serikali isisite kuchukua hatua ya kufunga ving'amuzi vya aina hii kwenye malori!

1. Gear ndogo ni aina ya kwanza ya breki. Ukiweka gear no moja au ile gear ya Crawler, hiyo tayari ni breki.
2. Bado kuna ile break ya retarder / engine stoper,
3. bado kuna breki ya kawaida ya mguu na pia
4. kuna hand break.