'Kupiga kofi', Huenda ikawa chanzo cha ajali nyingi Mbeya!

Kitendo cha gari kufeli brake sio kwamba ilikuwa neutral,

kuna suala la brake kupata moto iwapo mlima ni mrefu na dereva kashuka na gia ndogo (high) (eneo hili ndio linasababisha ajali nyingi sana kwenye malori na hasa kwa madereva vijana)

Pia kuna suala la kukatika kwa pipe za upepo au valve pia husababisha gari kufeli brake

Pia uchakavu wa magari hasa ma trailer haya ya mtumba haya muda wowote yanamwaga upepo

Kwa mfano gari hiyo iliyopata ajali senjere ni Leyland Daf (CF au XF)

gari hizi zinatatizo sana la valve kuvuja upepo.

Kingine inabidi pia kutanua hayo maeneo ya milima yote mkoani Mbeya hi I inasaidia kukwepa iwapo gari imefeli brake.....

Ni mtazamo wangu tu

I

Hapa umeongea kitu cha msingi mkuu
 
Huwezi kushuka mloma senjele, mlima nyoka, milima ya uporoto au mlima uyole kwa lori lenye mzigo ukiwa free yaani huja engage gear yoyote. Hiyo ni miteremko mikali sana na hakuna dereva atafanya ujinga wa aina hiyo ili auze mafuta huku akijua kwa asilimia 95 hatafika mwisho bila kupata madhara (ajali).

Kuna mizigo mizito huwezi hata kushuka hiyo milima ukiwa nan high gear, ni lazima ushuke na low gear huku uki balance stop engine na brake ili ufike salama. Kumbuka uking'ang'ana na brake peke yake uwezekano wa kujam ni mkubwa sana kutokana na joto linalozalishwa na pengine ukasababisha moto.

Ni kweli kuna sehemu wengi wanaweka free lakini ni maeneo ya tambarare na miteremko midogo. Kwenye miteremko mirefu unaweza fanya hivyo kama huna mzigo yaani gari iko tupu.

Magari yana matatizo mengi ya kiufundi yanayoweza kutokea kuanzia kwenye umeme, compressor ya kufua upepo, pipe kupasuka, valve kujam, brake kama break kujam.

Kimsingi ni kuchukua tahadhari hasa kwenye miteremko mikali ikiwemo kukagua gari kabla ya kuanza kushuka kwenye hiyo miteremko.

Asante mkuu
 
Ni ngumu police kuwa good invesitigator
Lakini innawezekana kwani kuna kitengo kabisa
Ila ni tamaa tu zinawapelekea
Kwa wenzetu lazima uwe na diploma ndio unakuwa police inspector
Kwetu darasa la saba halafu una top up mshahara kwa rushwa

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).

Suala hili huenda ndio limetugharimu kwa kusababisha ajali nyingi za malori hasa kwenye miteremko mikali.

Unaposhuka mteremko mkali gari ikiwa free, na kutumia breki ya kawaida, hufika hatua gari kuishiwa upepo, na hapa shida ndipo inapotokea.

Iwapo kama dereva angeshuka huku gari ikiwa kwenye gear, revolution za engine huwa juu na hivyo gari huwa linakuwa na upepo wa kutosha wakati wote.

Kama Lori likiendeshwa inavyostahili, nina uhakika hakuna lugha ya lori kufeli breki.

Katika magari ambayo uwezekano wa kufeli breki ni mdogo, basi ni haya malori. Gari lenye axle sita, linaanzaje kufeli breki axle zote? Haya malori kwanza yana breki za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi wakati wote.

1. Gear ndogo ni aina ya kwanza ya breki. Ukiweka gear no moja au ile gear ya Crawler, hiyo tayari ni breki.​
2. Bado kuna ile break ya retarder / engine stoper,​
3. bado kuna breki ya kawaida ya mguu na pia​
4. kuna hand break.​

Hivi inawezekanaje breki zote hizi zikafeli kwa wakati mmoja? Uwezekano wa kufeli kwa breki zote hizi kwenye roli ni asilimia 0.00%.

Serikali itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali kwenye miteremko ya milima ya Mbeya na Songwe pia iwapo itaweza kutega kamera (za kubaini revolution za engine) kwenye maeneo ya miteremko kubaini maroli ambayo yatakuwa yanateremka yakiwa kwenye free gear.

Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!

Kama mabasi tumefanikiwa kuyadhibiti, maroli hayawezi kutushinda!

Iwapo kuna uwezekano wa kufunga ving'amuzi vitakavyoweza kutusaidia kubaini roli linalotembea kwenye free gear, Serikali isisite kuchukua hatua ya kufunga ving'amuzi vya aina hii kwenye malori!
Umeongea vitu ambavyo jeshi la Polisi ilitakiwa wavione siku nyingi zilizopita. Chuo chetu cha Ussfirishaji huwa mnafanya tafiti kweli za ajali Kwenye barabara za Tz? Eng. Kyando uko wapi?
 
Lakini innawezekana kwani kuna kitengo kabisa
Ila ni tamaa tu zinawapelekea
Kwa wenzetu lazima uwe na diploma ndio unakuwa police inspector
Kwetu darasa la saba halafu una top up mshahara kwa rushwa

Sent from my SM-G570F using Tapatalk

Kuwa investigator kweli ukaweza kung'amua whats happened mpaka ajali ikatokea ni kipande kirefu....
 
Umeongea vitu ambavyo jeshi la Polisi ilitakiwa wavione siku nyingi zilizopita. Chuo chetu cha Ussfirishaji huwa mnafanya tafiti kweli za ajali Kwenye barabara za Tz? Eng. Kyando uko wapi?

Mkuu narudia tena NIT hakuna mtu anaitwa Eng. Kyando
 
Mimi na lia sana na madereva wetu kwakweli ni bogasi sana sana kujua haki ya msingi ya gari kutengenezwa na kulitambua gari ni janga la kitaifa, utasikia dereva anakwambia mkuu njaa hii wacha nijaribu jaribu, matokeo yake ndio haya sasa.
 
Compressor huwa haifi ghafla huwa ni nadra sana ila madereva wa malori makubwa ya mizigo inatakatiwa kila asubuhi kuDrain maji kwenye mitungi ya upepo.
Madereva wengi huwa hawana habari hiyo mitungi ikijaa maji inaayapeleka kwenye Valves zote valve zina rubber seal hizo rubber seal zinazidiwa hadi zinapasuka.

Kama Unautaratibu wa kukausha maji kwenye matenki ya upepo halafu Ukakuta Oil jua kabisa Compressor inaingiza Oil kwa hiyo Ni Vizuri Kununua Compressor mpya halafu hii ya zamani unabadilisha Piston Rings. Ukiwa makini hata upige Kofi mambo safi ila sehemu tamu ni pale Pipe line halafu iwe Usiku wa nne hivi.
Sio kweli aise maana mm limeshanikuta na kama ningekuwa speed hapari yangu ingeisha maana ilikua gafla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo cha gari kufeli brake sio kwamba ilikuwa neutral,

kuna suala la brake kupata moto iwapo mlima ni mrefu na dereva kashuka na gia ndogo (high) (eneo hili ndio linasababisha ajali nyingi sana kwenye malori na hasa kwa madereva vijana)

Pia kuna suala la kukatika kwa pipe za upepo au valve pia husababisha gari kufeli brake

Pia uchakavu wa magari hasa ma trailer haya ya mtumba haya muda wowote yanamwaga upepo

Kwa mfano gari hiyo iliyopata ajali senjere ni Leyland Daf (CF au XF)

gari hizi zinatatizo sana la valve kuvuja upepo.

Kingine inabidi pia kutanua hayo maeneo ya milima yote mkoani Mbeya hi I inasaidia kukwepa iwapo gari imefeli brake.....

Ni mtazamo wangu tu

I
Pia kuweka runoff area kwenye milima korofi..... Gari ilifeli dereva alipeleke huko ... Mfano kama umeshatembelea migodini kwenye milima mikali wametengeneza njia za kukimbilia gari inapofeli brake.

Runaway truck ramp - Wikipedia

image.jpeg

image.jpeg
 
Mimi na lia sana na madereva wetu kwakweli ni bogasi sana sana kujua haki ya msingi ya gari kutengenezwa na kulitambua gari ni janga la kitaifa, utasikia dereva anakwambia mkuu njaa hii wacha nijaribu jaribu, matokeo yake ndio haya sasa.
Madereva wengi huwa unakuta kajifunzia Fiat au Benz tena kwa mazoea hawapendi ukimkuta ana gari la kisasa ukaanza kumueleza zile button na switch mpya kazi yake ni nini...yuko Mmoja nilikutana nae njia ya Kigoma kampuni ya Panone gari kali 113 360 STreamliner pulling double diff
Karibu na Malagarasi ari kashindwa kupanda mlima uliosimama.

Mimi nikamuendea nikamuuliza vepe akasema imekataa huku akiilaumu Barabara ya Kigoma nikainama chini nikaiangalia ile gari hata tone la Oil haimwagi nikamwambia washa gari akawasha nikamuambia dogo msaidizi wangu aangalie leakage ya upepo huenda ile gari ina jamm

Dogo akaniambia pipe ya Lock diff inavujs tukairekebisha nikaingia kwenye Stering nika piga Crawler nikaweka na Lock diff Mbona chuma iliondoka na half ecceleretor mpaka juu tena ili kuwa inauwezo wa kupanda na namba mbili jamaa akawa anatikisa kichwa nikaja kugundua hata Lock diff hajui matumizi yake tukaongozana nae mpaka Kasulu akaninunulia bia kadhaa na nyama choma kwa hiyo 50%ya matatizo ya malori ni madereva zilizobakia 25% Tajiri na Spear feki kutoka China na miundombinu..
 
Pole sana mkuu natumaini uliwahi kabla halijachanganya. Hilo litakuwa la kampuni yetu pendwa Benz single dif unapeleka bia tukuyu au kyela.
Hapana hii ilikuwa inapeleka mzigo kwa agent wa tbl usagara pale buhongwa nikawa nimelimimina kuja kwenda kati kamba hazifungi sikuwaza mara mbili nikalitupa mtaroni na liliisha kweli cabin kwisha cha kushukuru nilitoka salama mara ya pili natoka geita imeshona makreti ya bia tupu mteremko wa usagara ilipasua tairi ya mbele mwaka huohuo tu nikalimwaga tena mtaroni hii ilibidi kupimwa vyuma chakavu iliisha kupita maelezo na penyewe nilitoka bila kovu ila nilizinduka nikiwa bmc
 
Pia kuweka runoff area kwenye milima korofi..... Gari ilifeli dereva alipeleke huko ... Mfano kama umeshatembelea migodini kwenye milima mikali wametengeneza njia za kukimbilia gari inapofeli brake.
Itakuwa ni vizuri zaidi
 
Hapana hii ilikuwa inapeleka mzigo kwa agent wa tbl usagara pale buhongwa nikawa nimelimimina kuja kwenda kati kamba hazifungi sikuwaza mara mbili nikalitupa mtaroni na liliisha kweli cabin kwisha cha kushukuru nilitoka salama mara ya pili natoka geita imeshona makreti ya bia tupu mteremko wa usagara ilipasua tairi ya mbele mwaka huohuo tu nikalimwaga tena mtaroni hii ilibidi kupimwa vyuma chakavu iliisha kupita maelezo na penyewe nilitoka bila kovu ila nilizinduka nikiwa bmc
Pole mkuu nilijua mbeya maana kule miteremko ndio balaa. Usagara bale kuna mteremko ukitokea buhongwa. Geita umenikumbusha mbali sana kipindi hakuna lami tunakimbizana na Nyehunge kuwahi kufika Geita.
 
Nyehunge kakubilo bubiki kahunda huko unapiga gia vumbi la kutosha enzi magari ya digidigi mwarabu wa kayenze vurugu tupu acha tuzeeke tu maana tuliyoyafanya barabarani tukiwa na nguvu huwa nakumbuka nabaki kucheka tu
 
Mbeya ni nyanda za juu. Iko takrabini 1700metres kutoka usawa wa bahari (sina uhakika). Hili hufanya magari yanayokwenda Mbeya kuwa yanakwenda kwa kupanda mlima wakati magari yanayotoka Nbeya kwenda Dar kwenda yakiwa yanashuka mteremko.
Hili hufanya madereva wengi kushuka free na hiki ndicho huweza kuwa chanzo kikubwa cha ajali za maroli. Takwimu zinainesha, maroli mengi yanayopata ajali ni yale yanayotoka Mbeya kwenda Dar kuliko yale yanayotoka Dar kwenda Mbeya.
Hili huondoa factors zingine kama uzito wa mizigo, uchakavu wa gari au umahiri wa dereva na hapa tunabakiwa na factor moja tu ya miteremko mikali kama main suspect wa ajali.
Huwezi laumu ubovu, kama bovu mbona lilienda salama? Huwezi laumi umahiri wa dereva coz yeye ndiye aliyelipeleka.
Hapa tunalaumu unsafe acts yani madereva kuwa na tabia ya kushuka miteremko gari likiwa free hivyo kuishiwa upepo hivyo kulifanya lipoteze muelekeo.
Kuna Milima mabonde...

Ukiwa unaingia mbeya kabla kufika uyole kuna mlima maarufu kama mlima nyoka... Huu nao ni balaa... Ukivuka mwajelwa ukifika Meta kuelekea simike pale napo kuna kilima... Slope yake nzuri tu... Sio pabaya sana... At least barabara yake imekuwa pana kidogo.

Ukitoka hapo unaenda iwambi... Hapo kuna balaa na nusu... Pale almost kila mwaka lazima ajali itokee...

Ukishavuka songwe kama unaelekea Tunduma nako panda shuka zipo nyingi kiaina...

Una swali lingine?

Njia ya chunya ndo usipime... Kule kama gari halina gear 1,2,3 usiende nalo... Utaanza kuchemsha hapo Iganzo tu... Hata kawetire huwezi kufika.

Njia ya Tukuyu angalau kidogo...

Haya maisha bhana... kila mtu huwa yanamgonga kwa style yake.
Daaah aisee kweli ni changamoto mpaka nimeishiwa pozi!!
 
Retarder na engine brake ni vitu viwili tofauti.... Engine brake inakuwa kwenye exhaust valves while retarder inafungwa baada ya gearbox
Retarder unaweza kuitumia vizuri ukiwa na mzigo mwepesi. Ukiwa na mzigo mzito usije hata siku moja kuamini retarder utakufa unajiona hivihivi.
 
Back
Top Bottom