'Kupiga kofi', Huenda ikawa chanzo cha ajali nyingi Mbeya!

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,252
2,000
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).

Suala hili huenda ndio limetugharimu kwa kusababisha ajali nyingi za malori hasa kwenye miteremko mikali.

Unaposhuka mteremko mkali gari ikiwa free, na kutumia breki ya kawaida, hufika hatua gari kuishiwa upepo, na hapa shida ndipo inapotokea.

Iwapo kama dereva angeshuka huku gari ikiwa kwenye gear, revolution za engine huwa juu na hivyo gari huwa linakuwa na upepo wa kutosha wakati wote.

Kama Lori likiendeshwa inavyostahili, nina uhakika hakuna lugha ya lori kufeli breki.

Katika magari ambayo uwezekano wa kufeli breki ni mdogo, basi ni haya malori. Gari lenye axle sita, linaanzaje kufeli breki axle zote? Haya malori kwanza yana breki za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi wakati wote.

1. Gear ndogo ni aina ya kwanza ya breki. Ukiweka gear no moja au ile gear ya Crawler, hiyo tayari ni breki.​
2. Bado kuna ile break ya retarder / engine stoper,​
3. bado kuna breki ya kawaida ya mguu na pia​
4. kuna hand break.​

Hivi inawezekanaje breki zote hizi zikafeli kwa wakati mmoja? Uwezekano wa kufeli kwa breki zote hizi kwenye roli ni asilimia 0.00%.

Serikali itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali kwenye miteremko ya milima ya Mbeya na Songwe pia iwapo itaweza kutega kamera (za kubaini revolution za engine) kwenye maeneo ya miteremko kubaini maroli ambayo yatakuwa yanateremka yakiwa kwenye free gear.

Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!

Kama mabasi tumefanikiwa kuyadhibiti, maroli hayawezi kutushinda!

Iwapo kuna uwezekano wa kufunga ving'amuzi vitakavyoweza kutusaidia kubaini roli linalotembea kwenye free gear, Serikali isisite kuchukua hatua ya kufunga ving'amuzi vya aina hii kwenye malori!
 
tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,777
2,000
Huwezi kupiga kofi gia lorry kwenye mteremko kwa dereva making na mtaalamu wa kuendesha lorry.....Mara nyingi huwa Ni wale madereva wageni Ni barabara au ubovu wa gari au kufeli kwa break tu.
 
Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,343
2,000
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).
Kama kuna makampuni hayafungi Car tracking systems kwenye malori yao basi naamini yapo too much outdated!.
Siku hizi tracking systems zinaonyesha mpaka kiwango cha mafuta kilichopo na hata dereva akifungua mfuniko wa tank mmiliki unapewa taarifa labda alibomoe pembeni:D na kilibomoa sijui atahakikisha vipi gauge zako zinabaki vile vile!..
 
Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,633
2,000
Kuna Main Valve ikifeli?!..huo upepo kwa kusukuma utapita wapi?Retarder sio engine stopper kupiga neutral lazima uangalie na mzigo ulopakia na eneo
Kumbe kuna mahali unachangiaga point za kisomi?., kuna thread ukivurugwa unaishia kurusha vi GIF vya mabomu ya kujitenge nezea ya Cossovo na Ukraine.Nimeamini hata kichaa kuna siku anapona.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,216
2,000
Huwa nashangaa pindi police au accident reports zinapotoka unashindwa kujua wamefikia uamuzi gani katika uchunguzi wao?
Au huwa hawajui kabisa mfumo mzima wa gari?
Ifike mahali waajiriwe watu wanaoweza kutoa mafunzo na pia kupima na kutoa sababu za ukweli badala ya kukimbilia Rushwa tu
Watu kila leo wanakufa lakini unakuta hakuna somo lililosomeka hapo what a waste of taxpayers money

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Fast Forward

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
406
500
Kitendo cha gari kufeli brake sio kwamba ilikuwa neutral,

kuna suala la brake kupata moto iwapo mlima ni mrefu na dereva kashuka na gia ndogo (high) (eneo hili ndio linasababisha ajali nyingi sana kwenye malori na hasa kwa madereva vijana)

Pia kuna suala la kukatika kwa pipe za upepo au valve pia husababisha gari kufeli brake

Pia uchakavu wa magari hasa ma trailer haya ya mtumba haya muda wowote yanamwaga upepo

Kwa mfano gari hiyo iliyopata ajali senjere ni Leyland Daf (CF au XF)

gari hizi zinatatizo sana la valve kuvuja upepo.

Kingine inabidi pia kutanua hayo maeneo ya milima yote mkoani Mbeya hi I inasaidia kukwepa iwapo gari imefeli brake.....

Ni mtazamo wangu tu

I
 
Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
4,275
2,000
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).

Suala hili huenda ndio limetugharimu kwa kusababisha ajali nyingi za malori hasa kwenye miteremko mikali.

Unaposhuka mteremko mkali gari ikiwa free, na kutumia breki ya kawaida, hufika hatua gari kuishiwa upepo, na hapa shida ndipo inapotokea.

Iwapo kama dereva angeshuka huku gari ikiwa kwenye gear, revolution za engine huwa juu na hivyo gari huwa linakuwa na upepo wa kutosha wakati wote.

Kama Lori likiendeshwa inavyostahili, nina uhakika hakuna lugha ya lori kufeli breki.

Katika magari ambayo uwezekano wa kufeli breki ni mdogo, basi ni haya malori. Gari lenye axle sita, linaanzaje kufeli breki axle zote? Haya malori kwanza yana breki za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi wakati wote.

1. Gear ndogo ni aina ya kwanza ya breki. Ukiweka gear no moja au ile gear ya Crawler, hiyo tayari ni breki.​
2. Bado kuna ile break ya retarder / engine stoper,​
3. bado kuna breki ya kawaida ya mguu na pia​
4. kuna hand break.​

Hivi inawezekanaje breki zote hizi zikafeli kwa wakati mmoja? Uwezekano wa kufeli kwa breki zote hizi kwenye roli ni asilimia 0.00%.

Serikali itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali kwenye miteremko ya milima ya Mbeya na Songwe pia iwapo itaweza kutega kamera (za kubaini revolution za engine) kwenye maeneo ya miteremko kubaini maroli ambayo yatakuwa yanateremka yakiwa kwenye free gear.

Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!

Kama mabasi tumefanikiwa kuyadhibiti, maroli hayawezi kutushinda!

Iwapo kuna uwezekano wa kufunga ving'amuzi vitakavyoweza kutusaidia kubaini roli linalotembea kwenye free gear, Serikali isisite kuchukua hatua ya kufunga ving'amuzi vya aina hii kwenye malori!
Hivi rotation na revolution ni tofauti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,252
2,000
Ebu naomba Geographia ya Mbeya kwanza !!
Mbeya ni nyanda za juu. Iko takrabini 1700metres kutoka usawa wa bahari (sina uhakika). Hili hufanya magari yanayokwenda Mbeya kuwa yanakwenda kwa kupanda mlima wakati magari yanayotoka Mbeya kwenda Dar kwenda yakiwa yanashuka mteremko.
Hili hufanya madereva wengi kushuka free na hiki ndicho huweza kuwa chanzo kikubwa cha ajali za maroli. Takwimu zinainesha, maroli mengi yanayopata ajali ni yale yanayotoka Mbeya kwenda Dar kuliko yale yanayotoka Dar kwenda Mbeya.
Hili huondoa factors zingine kama uzito wa mizigo, uchakavu wa gari au umahiri wa dereva na hapa tunabakiwa na factor moja tu ya miteremko mikali kama main suspect wa ajali.
Huwezi laumu ubovu, kama bovu mbona lilienda salama? Huwezi laumi umahiri wa dereva coz yeye ndiye aliyelipeleka.
Hapa tunalaumu unsafe acts yani madereva kuwa na tabia ya kushuka miteremko gari likiwa free hivyo kuishiwa upepo hivyo kulifanya lipoteze muelekeo.
 
Sting

Member
Aug 13, 2015
43
125
Huwezi kushuka mloma senjele, mlima nyoka, milima ya uporoto au mlima uyole kwa lori lenye mzigo ukiwa free yaani huja engage gear yoyote. Hiyo ni miteremko mikali sana na hakuna dereva atafanya ujinga wa aina hiyo ili auze mafuta huku akijua kwa asilimia 95 hatafika mwisho bila kupata madhara (ajali).

Kuna mizigo mizito huwezi hata kushuka hiyo milima ukiwa nan high gear, ni lazima ushuke na low gear huku uki balance stop engine na brake ili ufike salama. Kumbuka uking'ang'ana na brake peke yake uwezekano wa kujam ni mkubwa sana kutokana na joto linalozalishwa na pengine ukasababisha moto.

Ni kweli kuna sehemu wengi wanaweka free lakini ni maeneo ya tambarare na miteremko midogo. Kwenye miteremko mirefu unaweza fanya hivyo kama huna mzigo yaani gari iko tupu.

Magari yana matatizo mengi ya kiufundi yanayoweza kutokea kuanzia kwenye umeme, compressor ya kufua upepo, pipe kupasuka, valve kujam, brake kama break kujam.

Kimsingi ni kuchukua tahadhari hasa kwenye miteremko mikali ikiwemo kukagua gari kabla ya kuanza kushuka kwenye hiyo miteremko.
 
Sting

Member
Aug 13, 2015
43
125
Mbeya ni nyanda za juu. Iko takrabini 1700metres kutoka usawa wa bahari (sina uhakika). Hili hufanya magari yanayokwenda Mbeya kuwa yanakwenda kwa kupanda mlima wakati magari yanayotoka Nbeya kwenda Dar kwenda yakiwa yanashuka mteremko.
Hili hufanya madereva wengi kushuka free na hiki ndicho huweza kuwa chanzo kikubwa cha ajali za maroli. Takwimu zinainesha, maroli mengi yanayopata ajali ni yale yanayotoka Mbeya kwenda Dar kuliko yale yanayotoka Dar kwenda Mbeya.
Hili huondoa factors zingine kama uzito wa mizigo, uchakavu wa gari au umahiri wa dereva na hapa tunabakiwa na factor moja tu ya miteremko mikali kama main suspect wa ajali.
Huwezi laumu ubovu, kama bovu mbona lilienda salama? Huwezi laumi umahiri wa dereva coz yeye ndiye aliyelipeleka.
Hapa tunalaumu unsafe acts yani madereva kuwa na tabia ya kushuka miteremko gari likiwa free hivyo kuishiwa upepo hivyo kulifanya lipoteze muelekeo.
Magari mengi yanayorudi Dar huya yamebeba copper kutoka katanga au zambia. Copper ni nzito japo kuwa kiujazo inaonekana ni ndogo na wengi wanaopakia copper lori inakuwa na balance sana kwasababu ni mzigo wa chini hata hivyo sio sababu ya mtu kuweka free kwenye mteremko kama wa pipeline au kitonga.
 
Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,163
2,000
Kama kuna makampuni hayafungi Car tracking systems kwenye malori yao basi naamini yapo too much outdated!.
Siku hizi tracking systems zinaonyesha mpaka kiwango cha mafuta kilichopo na hata dereva akifungua mfuniko wa tank mmiliki unapewa taarifa labda alibomoe pembeni:D na kilibomoa sijui atahakikisha vipi gauge zako zinabaki vile vile!..
mkuu usicheze na ngozi nyeusi aisee, wanaweza sana
 
Di Ty

JF-Expert Member
Jul 11, 2014
574
1,000
Ebu naomba Geographia ya Mbeya kwanza !!
Kuna Milima mabonde...

Ukiwa unaingia mbeya kabla kufika uyole kuna mlima maarufu kama mlima nyoka... Huu nao ni balaa... Ukivuka mwajelwa ukifika Meta kuelekea simike pale napo kuna kilima... Slope yake nzuri tu... Sio pabaya sana... At least barabara yake imekuwa pana kidogo.

Ukitoka hapo unaenda iwambi... Hapo kuna balaa na nusu... Pale almost kila mwaka lazima ajali itokee...

Ukishavuka songwe kama unaelekea Tunduma nako panda shuka zipo nyingi kiaina...

Una swali lingine?

Njia ya chunya ndo usipime... Kule kama gari halina gear 1,2,3 usiende nalo... Utaanza kuchemsha hapo Iganzo tu... Hata kawetire huwezi kufika.

Njia ya Tukuyu angalau kidogo...

Haya maisha bhana... kila mtu huwa yanamgonga kwa style yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom