'Kupiga kofi', Huenda ikawa chanzo cha ajali nyingi Mbeya!

Ajali za Mbeya zinatokana na ubovu wa BARABARA. kuanzia Inyala MPAKA Tunduma ni mbovu SANA. ni BARABARA ya Lami, lkn ina matuta makubwa mithiri ya viazi. ni shida KUBWA. niliona last December nilivyokuwa natoka Mpanda.
Ila kama kuna mpango wa Kuipitisha Barabara ya Kwenda Zambia nje ya Mbeya City ingesaidia sana kupunguza hatari ambayo huenda inalisubiri jiji la Mbeya
Contena lililojaa Baruti lije kugongwa na Tenka la Mafuta ya Petroli moto na mlipuko unaweza kuuwa watu laki moja.
 
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).

Suala hili huenda ndio limetugharimu kwa kusababisha ajali nyingi za malori hasa kwenye miteremko mikali.

Unaposhuka mteremko mkali gari ikiwa free, na kutumia breki ya kawaida, hufika hatua gari kuishiwa upepo, na hapa shida ndipo inapotokea.

Iwapo kama dereva angeshuka huku gari ikiwa kwenye gear, revolution za engine huwa juu na hivyo gari huwa linakuwa na upepo wa kutosha wakati wote.

Kama Lori likiendeshwa inavyostahili, nina uhakika hakuna lugha ya lori kufeli breki.

Katika magari ambayo uwezekano wa kufeli breki ni mdogo, basi ni haya malori. Gari lenye axle sita, linaanzaje kufeli breki axle zote? Haya malori kwanza yana breki za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi wakati wote.

1. Gear ndogo ni aina ya kwanza ya breki. Ukiweka gear no moja au ile gear ya Crawler, hiyo tayari ni breki.​
2. Bado kuna ile break ya retarder / engine stoper,​
3. bado kuna breki ya kawaida ya mguu na pia​
4. kuna hand break.​

Hivi inawezekanaje breki zote hizi zikafeli kwa wakati mmoja? Uwezekano wa kufeli kwa breki zote hizi kwenye roli ni asilimia 0.00%.

Serikali itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali kwenye miteremko ya milima ya Mbeya na Songwe pia iwapo itaweza kutega kamera (za kubaini revolution za engine) kwenye maeneo ya miteremko kubaini maroli ambayo yatakuwa yanateremka yakiwa kwenye free gear.

Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!

Kama mabasi tumefanikiwa kuyadhibiti, maroli hayawezi kutushinda!

Iwapo kuna uwezekano wa kufunga ving'amuzi vitakavyoweza kutusaidia kubaini roli linalotembea kwenye free gear, Serikali isisite kuchukua hatua ya kufunga ving'amuzi vya aina hii kwenye malori!
Saa nyingine tujifunze kutoka mikoa ya jiran au nchi jiran. Wao wamefanikiwa vipi na mbeya wanafeli wapi. Hakuna sehemu yenye milima mingi na mikali kama Rwanda au hata Kagera Sana Sana wilaya za Ngara, karagwe na kyerwa. Lakini ajali za malori si nyingi kama mbeya.
 
Watu wa TBS wangekuwa wanatembelea maduka ya Amana hawa jamaa wanauza Mchina tupu wananunua kipuri halisi SAAB SCANIA halafu wanapeleka China kinaenda kutengenezwa kama kile na hawatoi gerentii jambo baya zaidi Vipuri Original vya Upande wa Upepo ni kampuni ya WABCO original lazima zina Serial numbers
Hawa jamaa wanakwenda kuCopy cat Wabco halafu wengi huwa wanaswali sana utakuta sala tano ila huku anauwa watu.
Hiiiii hapana, haiwez kupita hiv hiv lazima tuirusheTBS wafuatilie huu upuuzi wa hao Dealers Mkuu. Ni wauaji kama wengi tu
 
Huo ni uongo mkubwa usifanye masihara Lorry limepakia mzigo wa tani 10 alafu uweke FREE mteremukoni.
Jaribu kuweka free kwenye gari ndogo utaona mziki wake.

Kwa kifupi haya magari ni mabovu tu
Madereva wengi huweka free kwenye slope acheni ubishi lengo nkuokoa mafuta. Ni jambo LA hatari
 
Maoni yangu ni haya : kwa kuwa madereva wengi WA malori ni vichwa MAJI!!! Sasa ni wakati muafaka mkoa WA Mbeya kuweka kituo cha polisi maeneo. Korofi kisha kuweka madereva wazoefu ! Pindi lori linapokifa eneo korofi lenye mteremko mkali basi dereva ( kichwa maji)ashuke alipie kiasi fulani lori apewe dereva aliyeaminiwa nackupewa mafunzo na polisi alivushe eneo korofu kisha dereva kichwa maji arudishiwe lori na dereva aliye nacmafunzo arudi pale alipotoka hamtasikiaajali za ovyoi
 
Madereva wengi wa magari ya mizigo wamekuwa na tabia ya kuweka free malori wakati wakiwa kwenye miteremko ili kuokoa mafuta, mafuta ambayo baadaye huyanyonya kwenye vidumu na kwenda kuyauza (kama faida baada ya kumaliza safari na mafuta kubaki).

Suala hili huenda ndio limetugharimu kwa kusababisha ajali nyingi za malori hasa kwenye miteremko mikali.

Unaposhuka mteremko mkali gari ikiwa free, na kutumia breki ya kawaida, hufika hatua gari kuishiwa upepo, na hapa shida ndipo inapotokea.

Iwapo kama dereva angeshuka huku gari ikiwa kwenye gear, revolution za engine huwa juu na hivyo gari huwa linakuwa na upepo wa kutosha wakati wote.

Kama Lori likiendeshwa inavyostahili, nina uhakika hakuna lugha ya lori kufeli breki.

Katika magari ambayo uwezekano wa kufeli breki ni mdogo, basi ni haya malori. Gari lenye axle sita, linaanzaje kufeli breki axle zote? Haya malori kwanza yana breki za aina nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi wakati wote.

1. Gear ndogo ni aina ya kwanza ya breki. Ukiweka gear no moja au ile gear ya Crawler, hiyo tayari ni breki.​
2. Bado kuna ile break ya retarder / engine stoper,​
3. bado kuna breki ya kawaida ya mguu na pia​
4. kuna hand break.​

Hivi inawezekanaje breki zote hizi zikafeli kwa wakati mmoja? Uwezekano wa kufeli kwa breki zote hizi kwenye roli ni asilimia 0.00%.

Serikali itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali kwenye miteremko ya milima ya Mbeya na Songwe pia iwapo itaweza kutega kamera (za kubaini revolution za engine) kwenye maeneo ya miteremko kubaini maroli ambayo yatakuwa yanateremka yakiwa kwenye free gear.

Vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!

Kama mabasi tumefanikiwa kuyadhibiti, maroli hayawezi kutushinda!

Iwapo kuna uwezekano wa kufunga ving'amuzi vitakavyoweza kutusaidia kubaini roli linalotembea kwenye free gear, Serikali isisite kuchukua hatua ya kufunga ving'amuzi vya aina hii kwenye malori!
kufunga ving'amuzi sio suluhisho,mazingira ya barabara yanaweza sababisha ajali,ubovu wa gari na uzembe wa dereva waweza sababisha ajali pia lakin mtoa post ameng'ang'ania ving'amuzi tu,hujui miundo mbinu ya barabara yaweza sababisha ajali,ina maana madereva wote wanaopata ajali wanakuwa wameweka free,pole sana ajali zina mambo mengi,,
 
Sasa hapo ni kwamba madereva hawajui mfumo wa breki unavyofanya kazi au ni nini?
Hiyo mitelemko iko Mbeya tu, au kuna uhusiano gani wa madereva wa hiyo njia, hiyo mitelemko, ajali katika hilo eneo na uuzaji mafuta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malori makuu kuu Una Scania R420 treila Doll au Bachu excel BPW breki nyama tele Napiga kofi anan hadi Tunduma
Hehehe una Actros Mp4 au Volvo IPad inavuta body ya Tank aluminium ya Serin au Superdoll kwa nn nisilitwange Kofi Embassy Kuubwa mkononi Na mziki lainii....Gari kali mpaka unaogopa kupakia kuku Na mkaaa hahaha,Yani ukiuza ngao Na riflecta zake unapata Ist 10 Na HOWO 1..hehehe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi na lia sana na madereva wetu kwakweli ni bogasi sana sana kujua haki ya msingi ya gari kutengenezwa na kulitambua gari ni janga la kitaifa, utasikia dereva anakwambia mkuu njaa hii wacha nijaribu jaribu, matokeo yake ndio haya sasa.
Au unaenda Congo una pulling zaidi ya tani 30 yani unaendesha gari mbili wakati mmoja alafu tajiri kakupa milage laki mbili Na nusu(Kazi tembo mshahara sungura)fakeni hujafika hata Ruvu clutch ishaanza nuka ...ukifika misugusugu mfukoni umebaki Na elfu kumi hahaha...lazima uchochore kwa mawazo(bangi nyingi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hehehe una Actros Mp4 au Volvo IPad inavuta body ya Tank aluminium ya Serin au Superdoll kwa nn nisilitwange Kofi Embassy Kuubwa mkononi Na mziki lainii....Gari kali mpaka unaogopa kupakia kuku Na mkaaa hahaha,Yani ukiuza ngao Na riflecta zake unapata Ist 10 Na HOWO 1..hehehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umenifurahisha saana halafu uko peke yako hakuna hadisi ya Tingo halafu haina vituo vya hovyo hovyo laaah!!...heshima yako mkuu.
 
2. Ukiona dereva wa lori ana "piga kofi" kwenye mteremko hata kama liko tupu kuna mawili, hajui mfumo wa breki za lori ukoje na/au katumia kilevi kinachomfanya asiwe na maamuzi sahihi barabarani.
Mkuu unapotosha jamii mtu makini na anaelijua gari lake kuwa break system iko mswanu ndio anaweza kupiga free salama dereva mpumbavu ni yule anayejipia Kofi wakati gari kapewa chaka ndio tripu ya kwanza mimi nimekuwa barabarani na magari mabovu na magari mapya na magari mazima.sijawahi kufanya ajali na nimeshuhudia madereva wapumbavu wakipiga mzinga mbele yangu
 
Mimi binafsi sipendi gari kubwa zinazotumia Disc brake tena serikali ingeweka sheria Matenka ya mafuta yasitumie kabisa Disc brake kwenye miteremko mirefu zinawaka moto unajua wenzetu Huko ulaya mizigo yao ukizidi ni Tani kumi na nane halafu milima yote wameitoboa kwa hiyo kama Unatoka France kwenda Italy umepakia tani 20 unatembea na High range gears Low ni ya kundokea

Sasa sisi ni nchi Masikini tani 30 miteremko mireefu kama Ule wa Bugarama au Maumahiu william cross ni hatari sana kuna jamaa yangu aliungua burundi.
 
Upande wa Vilevi bia moja ya kutoa Baridi haina matatizo kabisa Mirungi haina shida kwenye Driving tena Redbull iliasisiwa huko thailand kwa ajili ya Madereva wa Malori ya Long haul.....tukija kwenye Bangi bangi inaweza kukukataa ukachanganya mambo

Mimi wakati na Drive HGV bangi ilishanikataa hasa usiku nikawa sivuti mpaka Tunduma au Kigali au Buja.

Pombe ukizidisha bia moja usiendeshe gari ni ujinga utakufa bado kijana utaacha watoto mke wakiteseka bure mara mkeo ataolewa na jamaa lingine watoto wako halitawajali.
 
Nimecheka kwa sauti sana... Hahaaaaaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom