Umri wote huo anaishi kwako, mpe miezi kadhaa ahame asikuletee tabu maana wakati mwingine huwa tunakaa na wadogo zetu kwa kudhani tunawasaidia maisha kumbe tunawaharibu bila kujijua, umri huo ni kuwa na kwake na kama anapokea misosi toka kwa mke wa mtu hata kama asingekuwa mke wa mtu basi huyo mdogo wako hana kifua cha utafutaji au kwa maana nyingine ameanza kuonyesha kuwa na zile tabia za kulelewa. Mjengee mazingira ya kurudi nyumbani kwa baba na mama maana akiwa kule atapata nafasi ya kujipanga kwa vitendo kwani kuna watu huwa wakikaa kwa ndugu zao hujisahau kama pale sio kwao hivyo anatakiwa a-struggle ili atoke