Kupendwa na usiyempenda .....!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupendwa na usiyempenda .....!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kongosho, Oct 23, 2011.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  naomba ni-share na wanajamvi hiki kisa kinachonitesa kwa saa...
  Hapo zamani za mwaka 1987 nikiwa nimemaliza fom 4 alitokea kijana mmoja akaniambia ananipenda, let me call him mr. X, wakati huo na yy alikuwa amemaliza fom 4. Tulisoma wote kuanzia darasa la kwanza alipofika la 5 akahamia bongo hadi aliporudi tukiwa tumemaliza fom 4 na straight akaniambia ananipenda. Nilimkataa sababu sikuwa tayari kuwa na mahusiano, nikaenda high school mkoa mwingine na yy akaenda shule lakini he kept in touch na kipindi hicho ilikuwa ni barua. Nikamaliza high school lakini yy ilibidi arudie mwaka lakini alijitahiti sana kurudi mkoani toka dar just to say hello to me.
  Mie niliendelea chuo kikuu lakini kila siku alikuwa akiniambia how much he loved na ni kweli nilijua fika ananipenda lakini mie nilimwona as a friend and brother. Mr hakujali akaniambia mie bado nakupenda mtoto so hoja, still sikuweza kumkubali. Baada ya masomo nilipata kazi dar nikamia hapa na yy akarudi mkoani tulikotoka ila mara kwa alikuja dar na kunitafuta na tulikuwa tunawasiliana almost kila siku. Mwaka jana akaniuliza kwani yy anatatizo gani for years amekuwa akiniambia ananipenda na nimemkataa, na jibu langu ilikuwa nampenda as a friend and a brother. Na kweli nilikuwa nampenda sana japo sio kimahusiano ya mapenzi. Na nilikuwa nikienda kuona wazazi mkoa kitu cha kwanza ilikuwa ni kumtafuta kokote alipo, hiki kitu kilikuwa kinamuudhi sana mama yangu maana alikuwa akisema unakuja home hata kula huli unaenda kwa mr x akati sie tumekuandalia rasmi.
  Mwaka huu mwezi wa 4 alipata misukosuko ambayo akashindwa kuibeba emotionaly sababu alinipigia akaniambia moyo umamwenda mbio for almost 2weeks, mie nikajua ni mshtuko wa yaliyompata na time will heel him. Kwa almost 8days nikawa sijampigia sababu ya kubanwa na majukumu and then 26 may night almost saa nne nikapokea sms toka kwake akiniambia kalazwa ghafla siku hiyo. Kwenye saa nne na robo usiku nikampigia japo hakuweza kuongea sana nikamwambia ntakupigia kesho pumzika wa sasa. And then mie nikalala, kesho yake asubuhi sana naambiwa he is no more, i almost fainted.
  I felt guility maana ni kama vile alinifanyia 'I wont forget you even on my dying bed' maana alifariki saa tano na nusu usiku the same day.
  Had leo inaniumiza sana nashindwa kujisamehe kwa kutompenda. One week ago nimeota tumeonana akawa anataka kunipelewa mahali nikamwambia ngoja nijiandae kabla sijamaliza kujiandaa nikaamka. Kumwambia dada angu akaniambia nimkemee sana sio vizuri ndoto za aina hii.
  Jamani ukimpenda mtu akasema hakupendi elewa, just understand, it happens.
   
 2. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,452
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  Una Dhambi ya Kuua
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Umeua bila kukusudia mkuu.
   
 4. O

  Optimistic Soul JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  usijiskie vibaya, mapenzi ni kupendana na hakuna kujifunza kupenda (haina training hii kitu), kua na mtu unaempenda na yeye akupende, jamaa hakua muelewa tu, me mtu akiniambia hanipendi nasepa fasta bila kupoteza muda. jiskie amani tu kwani ulishamwambia ukweli
   
 5. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  pole sana ila yanatokea sana mm niliwai kumwambia mtu simpendi akanywa sumu mama yake akaja kuniita eti nimlazimishe kunywa maziwa koz ni mm sababu mama yangu akamwambia yule mama embu nitolee balaa hapa kwaiyo unataka kumfanya mwanangu ajisikie vibaya kua kafanya kosa na alitakiwa amkubalia mwanao sio ndio kutaka kumjengea nn mtoto kua kila mtu akimfata amkubali koz asipofanya ivo atajiua loh!
  ila msela alipelekwa medical akaponea chupuchupu hadi leo yuko na chronic vidonda tumbo koz ya dawa ya kupulizia kahawa alikunywa ........ila kwasasa ni rafiki yangu mkubwa tu na ashaoa na anaelewa sasa kua ule ulikua ni utoto........so ucjickie vibaya kwani ni kweli hukumpenda na ulimwambia ila yy hakusikia
   
 6. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duuh inasikitisha lakini, assume ndio ungekuwa wewe unamhangaikia mtu for almost 11 year afu anakutolea nje. It hurts more than you thnk, muombe mungu akupe mume bora maishani mwako...
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu kupenda hakulazimishwi wala mtu halazimishwi kupenda na kujifanya unampenda mtu kumbe humpeni sio kumtendea haki sababu in the long run unaweza kuanza kumfayia visa na kumchukia na kudhani ulimfanyia favor.

  Ila kwenye case yako ni kwamba umepoteza rafiki na kama binadamu au rafiki wa kawaida lazima inakuuma kwa kutokuwepo kwenye saa zake za mwisho....(kama rafiki)


  Sasa hii imekwenda kwenye extreme.., kama wewe ambavyo hulazimishwi kupenda nae ndivyo hivyo hivyo.., jamaa kosa alilofanya ni kutoku-move on.., na nani amesema angekupenda wewe asingekufa...? pia huenda imekuwa vizuri ameondoka akiwa bado rafiki yako mwenye nafasi kwenye roho yako.., you never know huenda ungemkubali ungemfanyia visa (sababu humpendi ) na mkapoteza huo urafiki...

  RIP (whomever you are) you were a gentleman haukuficha kilichopo rohoni wala haukuleta chuki....

  Na mleta mada don't feel guilty sio kwamba amekufa sababu ya penzi lako (nature has taken its cause) lakini next time rafiki akikupigia simu yupo hoi jaribu kutafuta muda kwenda kumuona
   
 8. K

  Kahamba Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa hakuna wa kulaumiwa. Love comes automatically. Huwezi kujifunza kumpenda mtu. Ila mtu akikupenda na akaeleza nia yake, kama humpendi mwambie ukweli. Usiseme, " Ah ngoja nimzuge". Hiyo ndo mbaya, madhara yake baadaye huwa makubwa.
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  inaumiza sana ila mara nyingi ni ngumu kujilazimisha kupenda.
  Hii story imeniumiza sana maana..........
   
 10. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  wewe unajua kuumia au unajifanya tu?tutolee upupu wako hapa.lione..wewe mtu amekufa unashindwa hata kusema R.I.P unang'ang'ania kupenda...pumbavu.
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  tulikuwa tukiishi mikoa tofauti, mbona nilienda eapot bila hata tiketi ikabidi nikamuone for the last time, uzuri hata kwao walikuwa wananifahamu so i had my space msibani. It was hard, very hard. Mitaa yote ya huko wanajua i was dating him na walijua nilienda mzika mpenzi wangu kumbe a friend.
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani pia tunapopendwa kisha sisi tukawa hatujapenda tusiendeleze urafiki mkubwa mno kiasi cha kumpa mtu tamaa.

  Hivi wewe huna hisia za mapenzi kwangu lakini ukifika kwenu huli mpaka uje kwangu kwanza!

  Tusi wa lead people on, kama mtu humpendi punguza mawasiliano (unless useme kaka yako mnawasiliana kila siku, na huli kwenu mpaka ukaonane nae)
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Yeah you did all you could for your friend thats all that matters.., na ameondoka duniani akiwa bado rafiki yako.., kulazimisha kumpenda wakati roho haitaki sio vema huenda mgepoteza hata huo urafiki mkawa maadui...

  Just Cheer Up..!! Thats life na yeye ametangulia wote tutamfata huko.
   
 14. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Daaah hiyo kali!! Haya bwana mpende akupendae... Ila na ww ulimkazia mno mshikaji. . .. Walio sema mapenzi ni kizunguzungu hawakukosea
   
 15. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Pole sana!Yakubali yote yaliyotokea na jitahidi kusahau,then yape nafasi maisha yaendelee kama kawaida maana jamaa ukurasa wake ndio ulishafungwa hivyo.
   
 16. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Usijihisi mwenye kosa kwani ulisema ukweli toka moyoni mwako. Umempoteza kama rafiki na kwa hali ya kawaida lazima ikupain but don't feel guilt kwa sababu hukukubali ombi lake, hiyo ni nature imechukua mkondo wake (R.I.P man)!!
   
 17. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #17
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kosa ulilolifanya ni kumpa too much entertainment wakati unajua kuwa humpendi. And the way ulivyokuwa unamu-entertain ilikuwa inampa hope kwamba ipo siku utakubali. Don't do that kwa mtu mwingine kama humpendi kaa naye mbali wala usimpe entertainments za karibu ya kimapenzi. Hapo umeshiriki kuua ingawa ni kwa manslaughter na sio murder
   
 18. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo kwenye maisha hakuna nafasi ya urafiki bila mapenzi.., na mtu akisema anakupenda alafu ukawa humpendi ndio unamkimbia..?, yaani hakuna nafasi ya urafiki kwa mtu anaekupenda..?, wewe umeshamwambia kwamba unae mwingine kosa lake la kutoku-move on sioni kwanini liwe kosa lako.


  Kwahiyo angempenda asingekufa...?, na ni nani kasema amekufa kwa heartbreak..?
  Tena badala ya kumlaumu mtoa mada inabidi kumpongeza kuendelea na kukaa na huyu rafiki yake kama ndugu bila kumpa false hopes na kuishi nae kama kaka yake, kuliko angemkimbia sioni angesolve nini
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  this is very interesting kwa kweli........
   
 20. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #20
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Na ndio maana simlaumu kwa MURDER bali MANSLAUGHTER> Angalia mtoa mada mwenyewe amesema kile kifo kilikuwa kama kinaacha ujumbe gani kwake. Ujumbe ule alioachiwa mtoa mada unaonyesha kuwepo kwa mchango wake katika kifo (hata kama ni mchango mdogo kama punje ya haradari)
   
Loading...