kupenda na kutamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kupenda na kutamani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kireka1980, Jan 27, 2009.

 1. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Eti wanajamii kati ya kupenda (love) na kutamani (lust) kipi kinaanza?
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie naona kutamani ndio inaanza then inafuata upendo/mapenzi.
  enzi hizo kila mwanaume aliekuwa ananitokea nilijiwekea kama anatamani vile, mana usipokuwa makini unaweza kudhani/kuhisi kwamba hiyo kutamani ndio kupendwa kwenyewe huko, kujua mtu anaekupenda kwa mara moja huwa ni ngumu kidogo, ina hitaji muda kujua yapi mapendo.
   
 3. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ila wadada nao hawaendi na wakati wanajua wakimkubalia mwanaume siku ya kwanza wataonekana hawajatulia, yaani hadi wazungushe zungushe sana.
   
 4. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hivi kukutana siku ya kwanza nikakukubali ndio itamaanisha nakupenda?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,610
  Trophy Points: 280
  Hakuna msingi wa kinaanza kipi kama kuku na yai kwa sababu kupenda na kutamani ni vitu viwili tofauti.
  Kupenda ni mambo ya moyoni na kutamani ni mambo ya mwilini. Unaweza kumpenda Mungu lakini huwezi kumtamani Mungu.
  Kupenda kunakidhi haja za moyo na msingi wake ni vitu visivyoonekana, moyo, tabia, wema, ukarimu, unyenyekevu, ustahimilivu, upole etc.
  Kutamani ni vitu vinaonekana, kama sura, umbo, figure,shape,rangi, miondoko, sauti, pua, mwanya, dimples, nywele etc.
  Ukifanikiwa kukipata unachokipenda, hukiweka moyoni na kupata feeling ya gratification na kupenda kunaendelea. Ukifanikiwa kupata kitu unachotamani
  Unapata sense of achievment, na kutamani kunaishia hapo baada ya kukipata unachokitamamu na hamu ikiisha unaweza kukitupa wakati pendo ni la moyoni ndio maana haliishi.
  Kuna watu wanashindwa kutofautisha love na lust katika suala zima la mapenzi. Kijana akimuona msichana mrembo mwenye umbo la kuvutia, anaweza kumtamani
  ili kutimiza haja za matamanio ya mwili wako na ukaamua kumfuuatilia ili upate unachokita. Katika kumfuatilia, unaweza kugundua qualities za huyo dada ikiwemo tabia njema, ukajikuta unampenda.
  Vijana wengi wanatamani na kujifanya wanapenda.
  Ili upende, one needs time. Hakuna kitu kinachoitwa love at first site, hiyo ni tamaa. Love is gradual process, lust is instant.
   
 6. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nyamayao kwani inachukua muda gani kujua mtu unampenda? mm najua ni suala la kuusikiliza moyo wako? sijui kama utaenda nyumbani ukajiuliza nimpende au nisimpende
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Vipi hapo umempenda au umemtamani?
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kile kinacholeta mzuka wa nguvu. Kwa mtazamo wangu kutamani ni bomba sana kuliko kupenda ingawa kunadumu kwa muda mfupi. Wengi wanatumia kupenda kama wanataka kuoa ingawa inakuwa na hatari kwamba unaweza kuwa na mtu ambaye hapandishi mzuka wako kisawa sawa!
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  'Kupenda' ni jitihada ya makusudi haiji kwa bahati. Unaamua 'kupenda' lakini huwezi kuamua 'kutamani'. Kutamani (lust/infatuation) ni hisia zaidi. Kwa mantiki hii, mara nyingi tunatangulia kutamani zaidi na si kupenda.
   
 10. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Niaminivyo mimi,kupenda ni kama vile barafu.Barafu ukiiweka katika friza uwa ngumu kiasi cha kumtoa mtu ngeo kama atapigwa nayo,ingawa bafaru ile ile ukiiweka juani uyeyuka na hata maji kupotea kama hautakuwa makini.Ni kweli unaweza kwenda nyumbani na kujiuliza nimpende huyu binadamu au nisimpende,na ndo mana unasema unausikiliza moyo.Kupenda is a process ni mara chache utokea on your first site.Unauruhusu moyo kumpenda mtu fulani au laa.
   
 11. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu,kupenda ni jitihada za makusudi na ni kwa sababu hiyo ili uonekane unapenda ni lazima uoneshe kwa vitendo kwamba unapenda,na uwezi ukawa unapiga ngonjera tu unajua mie nakupenda huku vitendo vinavyoonesha hilo hakuna,na ukategemea watu watakuelewa
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mimi kwangu kumpenda mtu inachukua muda kidogo, siwezi kukutana na mtu leo nikasema nimempenda.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Tatizo la kina dada wengi ni usumbufu na kumzungusha mwanaume wao wanaona kama ndo kipimo tosha cha kupima mtu kama anampenda au lah kumbe si kweli kuna wanaume wanavumilia hata miaka 2 akila mzigo tu anakula kona na kusema alikuwa ananizungusha muda wote kitu chenyewe ni hiki na hakina kiwango kwanza mambo hajui n.k
  mwanamke anakapo anza kuonyesha kuwa anampenda mwanaume jamaa moyo usha yeyuka kama barafu.
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...unatamani kwanza, kisha unaanza kupenda. Kumbuka, kupenda ni kitendo kinachoendelea, matamanio yanakuja na kuondoka...

  ...unaweza kutamani bila kupenda, lakini huwezi kupenda bila kutamani. Kutamani ni, a desire to be fulfilled, kupenda ni, a matter of choice!
   
 15. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inanikumbusha lyrics za wimbo wa lucky dube 'kiss no frog'
   
 16. L

  Lusajo Kyejo Member

  #16
  Jan 28, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya yote yanaenda pamoja ila linalo anza ni kutamani,hii hali huja ghafla tu ukatamani na ukashindwa kujizuia lakini kupenda kunaanza taratibu then upendo unaongezeka na kukua.
   
 17. Joseverest

  Joseverest Verified User

  #17
  Oct 7, 2017
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 36,187
  Likes Received: 41,374
  Trophy Points: 280
  inategemea ntu na ntu
   
 18. KweliKwanza

  KweliKwanza JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2017
  Joined: Aug 20, 2016
  Messages: 2,723
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Unaanza kutaman
  Love maana yake nyingine ni zuzoea
  Foristance yu love yur mother
   
Loading...