Kupenda kuna sababu?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,876
2,740
Nauliza hivi kwa vile naona ni wanawake zaidi ndio ving'ang'anizi ktk mahusiano. Ni utam wa uroda, hofu ya kuishi peke, kufuata mali, mkumbo, au ni janga tu la asili? Wajuzi nifahamisheni
 
Nauliza hivi kwa vile naona ni wanawake zaidi ndio ving'ang'anizi ktk mahusiano. Ni utam wa uroda, hofu ya kuishi peke, kufuata mali, mkumbo, au ni janga tu la asili? Wajuzi nifahamisheni

Nani kakwambia kwamba wanawake ndio ving'a'nganizi katika mahusiano? Na wakati wanaume ndio ving'ang'anizi kama ruba, akianza kumfuatilia msichana atang'ang'ana kama nini. Na nyie si ndio huwa mnaanza kuaproach msichana, basi nyie ndio mna janga la asili.Mwanaume bila mwanamke bado hajakamilika.
 
Nauliza hivi kwa vile naona ni wanawake zaidi ndio ving'ang'anizi ktk mahusiano. Ni utam wa uroda, hofu ya kuishi peke, kufuata mali, mkumbo, au ni janga tu la asili? Wajuzi nifahamisheni

Ndugu yangu..hakuna cha wanawake kuwa ving'ang'anizi wala nini- hivi sasa kuna taarifa ya mwanaume kukodi taxi kwenda kilometer kadhaa kumfuata mwanamke aliyekuwa amemkataa na kumpiga risasi! Mziwanda..kwanini huwa hamtaki kuachwa lakini????

Kupenda ni hulka tuliyopewa wanadamu wote .... haijalishi mwanamke wala mwanaume!Kuna wenye kupenda JUST BECAUSE!

Mvuto unaopelekea mtu kumpenda mtu unatofautiana baina ya mtu na mtu.Hivyo ulivyoviweka hapo juu siyo vivutio vya mapenzi...ni vikorombwezo tu.Huwezi kumpenda mtu kisa unaogopa kuishi mwenyewe...kama ni hivyo kwanini usiende kuishi na nduguzo wa damu? Kama ni mali... huo sio upendo bali ni ujangili tu...kama ni uroda....hicho siyo kivutio.
 
Duh! Basi tukubaliane kuwa mwanaume aking'ang'ania ujue ni kwa ajili ya ngono zaidi. Mwanaume anaweza kuua anapogundua tunda lake linaliwa na mwingine. Kwa mwanamke ni ngono na kadhalika zingine. Ila mjue kuwa ngono ndio sababu kubwa wapenzi kupendana. Mwanaume hutamani zaidi na ndio maana hutumia mda mwingi kutafuta. Kwa upande wa mwanamke ni abstract zaidi. Pia kama si mali na jina, ingekuwa rahisi kwa mwanamke msomi kuolewa na mwanaume wa elimu ya chini yake.
 
Mada yako hukuifafanua zaidi tuelewe unazungumzia watu kwenye mahusiano casual au mahusiano rasmi kama ya kindoa au uchumba.

Kwenye ndoa mtu anaweza kuonekana king'ang'anizi kwa sababu kuna nira na yahusianayo.Kwenye casual - urafiki tu..sioni kwanini mtu ang'ang'anie.... labda kama wapenzi hao "wamewekeza" kiasi cha kufanya kuacha/kuachwa kuwe na athari.Hili linahitaji mjadala wa kifilosofia zaidi. Unaweza kukuta mmoja ana matarajio yaliyovuka mpaka wakati mwingine hana habari kabisa.Hivyo basi kuepuka hili kutokea, ni bora wewe unayetaka kung'ang'ania ufanye kazi ya ziada kumfanya mwenzio naye awe kwenye level ile ile uliyo wewe ya kihisia. Vinginevyo, unapohisi hamko wave length moja, ni afadhali uanze kujiondosha mara moja maana utakuja kujikuta unafanya kitu kibaya kama hata kuua!
 
Una uhakika gani kuwa wanawake peke yao ni ving'ang'anizi?
Bwana wewe, mapenzi ni by nature! kama wewe ni binadamu halisi huwezi kukwepa wala huwezi ishi bila mapezi.watu wote ni ving'ang'anizi kwa sababu tunahitaji mapenzi.
 
Wanawake wanaongoza kwa kung'ang'ania wanaume wengine hata kama humpendi unamwonyesha LIVE lakini wapi ataendelea kukuletea vizawadi n.k chukueni ile roho ya uhuruma basi na kwenye penzi ni hivyo hivyo.
 
Mada yako hukuifafanua zaidi tuelewe unazungumzia watu kwenye mahusiano casual au mahusiano rasmi kama ya kindoa au uchumba.

Kwenye ndoa mtu anaweza kuonekana king'ang'anizi kwa sababu kuna nira na yahusianayo.Kwenye casual - urafiki tu..sioni kwanini mtu ang'ang'anie.... labda kama wapenzi hao "wamewekeza" kiasi cha kufanya kuacha/kuachwa kuwe na athari.Hili linahitaji mjadala wa kifilosofia zaidi. Unaweza kukuta mmoja ana matarajio yaliyovuka mpaka wakati mwingine hana habari kabisa.Hivyo basi kuepuka hili kutokea, ni bora wewe unayetaka kung'ang'ania ufanye kazi ya ziada kumfanya mwenzio naye awe kwenye level ile ile uliyo wewe ya kihisia. Vinginevyo, unapohisi hamko wave length moja, ni afadhali uanze kujiondosha mara moja maana utakuja kujikuta unafanya kitu kibaya kama hata kuua!

ung'ang'anizi hauna mipaka dada. Uwe ndoani au nje yake. Wapo wanaooa maslah ya ndoa yamedoda wakaamua kuziacha ndoa zao. Nimepata picha kuwa sababu halisi ni maslah
 
Wanawake wanaongoza kwa kung'ang'ania wanaume wengine hata kama humpendi unamwonyesha LIVE lakini wapi ataendelea kukuletea vizawadi n.k chukueni ile roho ya uhuruma basi na kwenye penzi ni hivyo hivyo.

We Fidel acha kutudanganya hapa,kuna ving'ang'anizi kama wanaume kwenye sayari hii,tena hata mkionyeshwa vituko vya aina gani bado mnang'ang'ania hivi kwa nini?huwa nawashangaa kweli nimeshakuonesha dalili zote kuwa sikutaki lakini bado unalazimisha ni kwa kwa nini eti? inabidi tuanzishe mada nyingine,kwa nini wanaume ni ving'ang'anizi hata pale inapotokea umeoneshwa vituko vya kila dizaini ili mtupe sababu.
 
Duh!mnaniacha hoi jamaa..naona mada imegeuzwa toka nini sababu ya kupenda hadi nani king'ang'anizi ktk mapenzi..hahahaha...naona huu mjadala hata kwa jokes unafit kabisa.
 
Back
Top Bottom