Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Pole sana kwa kutoa chozi, pengine kapenda mwingine au umemkosea muulize polepole, kama vipi mpotezee.
Kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
Kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
Nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
Hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
1.haya ni mapenzi originalmoyo ukija kupenda, wenda ukidundadunda,
mtu aanza kukonda, anapomkosa nyonda,
alalama kama konda, mwenzenu kumbe kapenda,
mtu akiisha kupenda, huogopa kuvurunda
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Ukishampenda mtu, moyo usipate kutu
roho yako iwe kwatu, usilie mimi mbwitu
usilete katukatu, kwa kusikia ya watu
mwisho wajikuta fyatu, na penzi likawa butu,
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nilimpenda fulani, yule binti wa jirani,
kaniingia moyoni, penzi hadi mifupani,
leo kanuna jamani, amepata kisirani
kosa langu miye nini, najiuliza watani,
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nikimgusa aruka, kumbusu anangaka,
nyonda mbona washtuka, wanitatiza hakika,
lipi limevurugika, nambie wangu wa shoka,
ni vipi umekwazika, nitonye nikatonyeka,
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Siku zikapitiliza, maswali najiuliza,
kuliza ameniliza, na majonzi kanijaza,
najikunyata nawaza, hadi nimepitiliza,
ni dogo amelikuza, au nikubwa sijaliwaza
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
nabaki nasubiria, nyonda kunihurumia,
na aje kuniambia, ni wapi nimechapia,
mwenzako ninaumia, ninavyokufikiria
fanya hima kunijia, kosa sitalirudia,
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nilichokuandikia, ni kweli nakuambia,
tafadhali fikiria, jibu nalisubiria
mikono nimeachia, niweze kukumbatia
ni mbali tumeanzia, si tayari kuachia
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nafunga ninafungana, ya leo siyo ya jana,
na wewe nafungamana, ee nyonda wangu mwanana,
zikongine zafanana, penzi tulilopeana,
fanya hima kuonana, nina hamu kukuona,
kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Na. M. M. Mwanakijiji (sauti ya kijiji)
Moyo ukija kupenda, wenda ukidundadunda,
Mtu aanza kukonda, anapomkosa nyonda,
Alalama kama konda, mwenzenu kumbe kapenda,
Mtu akiisha kupenda, huogopa kuvurunda
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Ukishampenda mtu, moyo usipate kutu
Roho yako iwe kwatu, usilie mimi ‘mbwitu'
Usilete katukatu, kwa kusikia ya watu
Mwisho wajikuta fyatu, na penzi likawa butu,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nilimpenda fulani, yule binti wa jirani,
Kaniingia moyoni, penzi hadi mifupani,
Leo kanuna jamani, amepata kisirani
Kosa langu miye nini, najiuliza watani,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
Kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
Nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
Hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nikimgusa aruka, kumbusu anan'gaka,
Nyonda mbona washtuka, wanitatiza hakika,
Lipi limevurugika, nambie wangu wa shoka,
Ni vipi umekwazika, nitonye nikatonyeka,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Siku zikapitiliza, maswali najiuliza,
Kuliza ameniliza, na majonzi kanijaza,
Najikunyata nawaza, hadi nimepitiliza,
Ni dogo amelikuza, au nikubwa sijaliwaza
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Nabaki nasubiria, nyonda kunihurumia,
Na aje kuniambia, ni wapi nimechapia,
Mwenzako ninaumia, ninavyokufikiria
Fanya hima kunijia, kosa sitalirudia,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nilichokuandikia, ni kweli nakuambia,
Tafadhali fikiria, jibu nalisubiria
Mikono nimeachia, niweze kukumbatia
Ni mbali tumeanzia, si tayari kuachia
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nafunga ninafungana, ya leo siyo ya jana,
Na wewe nafungamana, ee nyonda wangu mwanana,
Zikongine zafanana, penzi tulilopeana,
Fanya hima kuonana, nina hamu kukuona,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Mapenzi ya kwenye Tamthiliya........ shades etc.1.haya ni mapenzi original
2.mapenzi kama haya ni adimu kuyapata.
3.usanii kwenye mapenzi hivi sasa ndio unatawala kwa kiasi kikubwa.
Kweli kupenda ni kazi,huwa najiuliza kwanini Mungu aliweka upendo wa mapenzi i wish usingekuwepo!! MM hapo penye red ni pagumu sana maana watu wengi ni selfish,full usanii utadhani wote wamepita bagamoyo!Moyo ukija kupenda, wenda ukidundadunda,
Mtu aanza kukonda, anapomkosa nyonda,
Alalama kama konda, mwenzenu kumbe kapenda,
Mtu akiisha kupenda, huogopa kuvurunda
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Ukishampenda mtu, moyo usipate kutu
Roho yako iwe kwatu, usilie mimi ‘mbwitu'
Usilete katukatu, kwa kusikia ya watu
Mwisho wajikuta fyatu, na penzi likawa butu,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nilimpenda fulani, yule binti wa jirani,
Kaniingia moyoni, penzi hadi mifupani,
Leo kanuna jamani, amepata kisirani
Kosa langu miye nini, najiuliza watani,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Kusema nami hataki, akija kwangu habaki,
Kwenye miadi hafiki, nikichekesha hacheki,
Nisimuite rafiki, hata mpenzi hataki,
Hata kudeka hadeki, vya kuvila haviliki
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Nikimgusa aruka, kumbusu anan'gaka,
Nyonda mbona washtuka, wanitatiza hakika,
Lipi limevurugika, nambie wangu wa shoka,
Ni vipi umekwazika, nitonye nikatonyeka,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Siku zikapitiliza, maswali najiuliza,
Kuliza ameniliza, na majonzi kanijaza,
Najikunyata nawaza, hadi nimepitiliza,
Ni dogo amelikuza, au nikubwa sijaliwaza
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi
Nabaki nasubiria, nyonda kunihurumia,
Na aje kuniambia, ni wapi nimechapia,
Mwenzako ninaumia, ninavyokufikiria
Fanya hima kunijia, kosa sitalirudia,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nilichokuandikia, ni kweli nakuambia,
Tafadhali fikiria, jibu nalisubiria
Mikono nimeachia, niweze kukumbatia
Ni mbali tumeanzia, si tayari kuachia
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi.
Nafunga ninafungana, ya leo siyo ya jana,
Na wewe nafungamana, ee nyonda wangu mwanana,
Zikongine zafanana, penzi tulilopeana,
Fanya hima kuonana, nina hamu kukuona,
Kupenda kweli ni kazi, huko kwaja na machozi!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
kaizer sikujua kama na wewe ni mmalenga ...............:smile-big:
Uwe na busara kama Wiselady
Au na upendo kama FirstLady,
Na ma "passion kama queenKammy
Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa!
Na Ukipendwa kama Nyani Ngabu
Watu hawakosi sababu!
Ili mradi mapenzi tabu, na
Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Mfikiriea Zion daughter,
Kila kitu amepata,
Naye JS amedata, kisa
Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa!
Uwe mkarimu kama bacha
Au Fidel80 wa kukacha,
Na The Finest wa kuacha..bado
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Ukiwa mtulivu kama Asprin
Au Mlokole kama Gaijin
Bado utaikuta Acid! kisa?
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa!
Nilidhani katulia Teamo,
Kumbe madhila yangalimo!
Nikamuliza Masanilo! kanambia:
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Ni kwako Cheusimangala,
Je waweza kugangamala?
Manake hayana muamala,
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Alipata kusema Nyamayao,
'kitusimulia ya kwao
Kumbe ndio hayo hayo,
Mapenzi yanatesa 'kiyapatia unatesa....
mwanafasihi mzuri sana wewe Kaizer, vipaji mnavyo mnavikalia, au mnataka watu tuwahamasishe kwa campaign za shuka kwa shuka ili mvitoe vipaji vyenu hadharani?Uwe na busara kama Wiselady
Au na upendo kama FirstLady,
Na ma "passion kama queenKammy
Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa!
Na Ukipendwa kama Nyani Ngabu
Watu hawakosi sababu!
Ili mradi mapenzi tabu, na
Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Mfikiriea Zion daughter,
Kila kitu amepata,
Naye JS amedata, kisa
Mapenzi bado yanatesa, 'kiyapatia unatesa!
Uwe mkarimu kama bacha
Au Fidel80 wa kukacha,
Na The Finest wa kuacha..bado
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Ukiwa mtulivu kama Asprin
Au Mlokole kama Gaijin
Bado utaikuta Acid! kisa?
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa!
Nilidhani katulia Teamo,
Kumbe madhila yangalimo!
Nikamuliza Masanilo! kanambia:
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Ni kwako Cheusimangala,
Je waweza kugangamala?
Manake hayana muamala,
Mapenzi yanatesa, 'kiyapatia unatesa
Alipata kusema Nyamayao,
'kitusimulia ya kwao
Kumbe ndio hayo hayo,
Mapenzi yanatesa 'kiyapatia unatesa....
Kaizer nitakupeleka kurecord hiyo single, baada ya hapo utafanya featuring na Mwanakijiji so itakuwa full mautamu.Love it, hasa hapo kwa Fidel kukacha nikilinganisha na avatar yake mh,,:becky::eyebrows:Dah nimeipenda hii.....
Very creative.....