Heading hapo juu inasomeka kama haijakamilika vile.
Inawezekana kila mwanaJF akawa amejenga picha yake na uelewa kuhusu hili neno Kupata Mtoto
Mtoto ni tunu na furaha ya wazazi, ingawa inawezekana wazazi hao wakawa wapo ktk mahusiano rasmi ya ndoa, mchepuko na kadhalika. Lakini si mara zote mtoto anafurahisha wazazi. Pata picha ya wazazi ambao kwanza ni wanafunzi kisha tegemezi kwa wazazi/ walezi wao ambapo inawezekana walitamani kuuchoropoa ujauzito bila mafanikio lakini hatimaye wamepata mtoto ambaye labda mzazi mmoja kamkana tangu alipotaarifiwa ama wote hawana amani na ujio huo.
Hakika pia ninashangazwa na wingi wa watoto kwa wazazi ambao uchumi wao ni tia-maji tia-maji na cha kushangaza ni kuwa hawakosi chakula cha kuwalisha watoto wao na kadhalika. Hivyo naamini sasa kwamba mtoto huja na baraka maalum. Sishawishi uzazi usio na mpango.
Pamoja na hayo mtoto anabaki kuwa na haki zote za msingi yaani ulinzi na malezi kutoka kwa wazazi/ walezi wake.
Ninafuraha kuwatabainisha kwamba nimekuwa miongoni mwa wazazi rasmi wenye furaha iliyotajwa hapo juu.
Mkuu kwanza nashukuru kwa wishes...Paw hongereni sana kwa kweli sasa ....unaalkwa rasmi katika klabu ya "wababa" !!!!!!!
Nimefarijika kuona unatambua kuwa kwanza mtoto ni faraja na sio saa zote huwa wanakupa furaha bila changamoto za hapa na pale.
Umeongelea haki za mtoto, ulinzi, kuwalisha vizuri.......lakini pia uko makini kuwa yote haya yanategemea idadi yao!!!!!
Hongereni tena
Mkuu kwanza nashukuru kwa wishes...
Pile nimevutika sana kusoma mara mbili post yako na hapa nawaza kama wewe siyo mwalimu basi fani uliyopo sasa si yako.
Nashukuru tena mkuu
Hivi mke wa Paw humu ndani ni nani?? Loh btw-hongera sana mkuu mungu awakuzie na mumlee katika maadili mema.Best wishes
............................:spy:.................................:boink:...........................
Hukosi neno! hahaha, anaendelea vyema. mwache apumzike mwenziyo
Hongera sana Paw, ni furaha sana kuona fotokopi yako duniani.
Na kiukweli furaha hiyo huzidi na huwezi ona mzigo kulea.
King'asti mbaya sana, hujanishirikisha?
Yaaani huyo uliyemtaja ndio hovyoooo mwili mzima.....khaaaa!!!!?????