Kupata mkopo bila dhamana

Kupata mkopo bila dhamana

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,542
Reaction score
127,848
Kwa wale mlio wazoefu na masuala haya ya mikopo,

Je! Kama mtu hana kazi au ajira ila ni msomi mzuri tu na maisha yamempiga na hana jinsi wala namna anataka kukopa pesa benki ili ajikwamue kimaisha kwa kuanzisha mradi je ataweza kukopesheka?

Katika dhamana ataweka nini ili aaminike benki au katika hizo taasisi za mikopo? Na Je! Ni benki gani au taasisi zipi hapa nchini Tanzania zinazotoa huduma hii ya kuwakopesha watu wasio na ajira / kazi wala mali lakini wamesoma?

Tusaidiane tafadhali ili wenye mahitaji kama haya na wao waweze kujikwamua kimaisha ili matapeli, malaya na majambazi wapungue mitaani.
 
Mkuu Crdb walikuwa wanatoa mikopo ya dizaini hyo, ila ilikuwa ni kwa wasomi wa SUA pekee na wawe wamehitimu miaka ya karibuni. Kwa maelezo zaidi tembelea kwenye branches zao.
 
Mkuu hii post inaweza kuwa post ya week!!!!
 
Back
Top Bottom