Kupanda mlima Kilimanjaro

Kupanda mlima Kilimanjaro

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,508
Reaction score
13,976
Habari za sikukuu ya Pasaka?

Napenda kuutanganizia umma kuwa kutakuwa tukio la kupanda mlima Kilimanjaro 5895 MT, tarehe 9 mwezi wa SITA mwaka 2014 kupitia njia ya Marangu kwa siku 6.

Wanakaribishwa watu wote wenye mapenzi ya kuona vivutio mbalimbali tulivyojaliwa na Mungu hapa Tz,safari hii ya kupanda mlima itahusisha watu kutoka mataifa mbalimbali kama Urusi nk

Gharama ni laki tatu na hamsini tu ikijumlisha kiingilio,chakula,sehemu ya kulala,mpagazi na watakaofika kilele cha mlima watapewa CHETI cha ushindi.

Gharama haziushishi kulala Moshi kabla na baada ya kupanda mlima,vifaa vya kupandia mlima kama viatu,sticks nk(unaweza kukodi vifaa vyote kwa elfu sabini tu.

Wahi mapema kuna nafasi chache zimebaki,mwisho wa kujiandikisha ni 15 Mei 2014.
Mawasiliano: 0787140432 au tours@infotanzania.net

Usiwe na magonjwa kama Kisukari,TB,Pumu (Uwe na afya njema)

"KUWA MZALENDO TANGAZA UPENDO"
 
Kwa pesa hiyo akuna uzalendo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wenye pesa zao nendeni

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Gahli sana bila sababu ya msingi.

Changanua gharama uone ulivyo mwizi

Kama hivi,
Kiingilio kwenye hifadhi Ths 2000 * 6 = 12,000
Chakula 10,000* 6 = 60,000
Vifaa 100,000
Guide 5000
Uokozi 3000
JUMLA 180,000
 
Gahli sana bila sababu ya msingi.

Changanua gharama uone ulivyo mwizi

Kama hivi,
Kiingilio kwenye hifadhi Ths 2000 * 6 = 12,000
Chakula 10,000* 6 = 60,000
Vifaa 100,000
Guide 5000
Uokozi 3000
JUMLA 180,000

Nadhan wanatoza gharama sawa na watalii wa nje ya nchi.

Kwa jins nnavyojua mie watz wanalipa gharama tofauti na watalii watokao nje .
 
350,000/= ? Sijapata ka bustani ka mboga mboga hapa? Tufundishane kuzitafuta kwanza, kutumia baadaeee...
 
350,000/= ? Sijapata ka bustani ka mboga mboga hapa? Tufundishane kuzitafuta kwanza, kutumia baadaeee...

Wewe kila ukiwa na 350,000/= unawaza kuongeza biashara huwa huweki pesa kwaajili ya matumizi?!...au matumizi wewe ni kula...

Go out sometime and have some fun...
 
Hiyo elfu kumi ya chakula kwa siku unanunua mgahawa gani huko mlimani.?
Hiyo elfu tano ya guide ni kwa siku zote sita..?
Uhitaji porter wala mpishi.??
Vipi gharama nyingine kama usafiri wa kutoka moshi kwenda maragu gate na kurudi mishi mjini.
Tuache upotoshaji usio na msingi kama wewe huna pesa waachie wenye pesa.ACHA UJINGA KAMA HUJUI ULIZA..!

gahli sana bila sababu ya msingi.

Changanua gharama uone ulivyo mwizi

kama hivi,
kiingilio kwenye hifadhi ths 2000 * 6 = 12,000
chakula 10,000* 6 = 60,000
vifaa 100,000
guide 5000
uokozi 3000
jumla 180,000
 
Kawaone wataalamu watakuelekeza,lakini hata wao pia watahitaji uwalipe hakuna cha bure dunia hii.!!
350,000/= ? Sijapata ka bustani ka mboga mboga hapa? Tufundishane kuzitafuta kwanza, kutumia baadaeee...
 
Tangazo zuri ila limepata upinzani sana nimekata tamaa
 
Pole sana,unajua mgeni wa nje ya EAC analipa kiasi gani kwa siku.?
Kwa faida yako Park fee 70$ X 6days=420$
Hut fee 60$ X 5 Nights=300$
Rescue fee 20$ for 6 days
Grand Total payable to KINAPA 740$
Hapo hakuna gharama za chakula,mpishi,guide,porters nausafiri.
Wewe unaposema gharama ni sawa na wageni wa nje je unaona hiyo gharama ipo sawa..?? Any way sio kosa lako. Waweza pata gharama za viingilio hivyo pia kwenye The official site of the Tanzania National Parks - Home
Nadhan wanatoza gharama sawa na watalii wa nje ya nchi.

Kwa jins nnavyojua mie watz wanalipa gharama tofauti na watalii watokao nje .
 
Mkuu kukata mzizi wa fitina ebu weka mchanganuo hiyo 350k ilivyopatikana
 
Onesha interesting kwanza ya kupanda mlima then ninaweza kuweka mchanganuo.
Ni kitu chepesi tu wewe kama unaona hiyo pesa ni nyingi,acha au tafuta kampuni itakayoweka kukubaliana na bajeti yako.!
Pia ukumbuke hii ni biashara kwa hiyo siwezi anika kila kitu hapa.

Huu ndio wizi jamvini na utapeli! Acha kabisa bwana mdogo! Watu hawanunui tu siku hizi package bila mchanganuo, tena usiache kuweka na menu day by day from breakfast lunch and dinner. Acha kutaka kupata hela kivivu 350k inatakiwa uifanyie kazi si kutumia jamvi bure na kupata hela kizembe. Na ukiainisha hivi vyote ndivyo nitawapatia habari wafanyakazi wenzangu hapa Silicon Valley kuja kula hard time mlimani. Sawa!

Hii utauza zaidi na kila mtu atauona uwazi na kutaka kushiriki zoezi hilo. Hii ndio akili na siyo kuwa too defensive.
 
Kwenye hyo 350k kuna kahela kake ka juu watot wake wasife njaa-njie mnaofa hyo safar ya mliman mnatoka kampun gan?
 
Kwanza niseme wewe huna pesa ya mimi kukutapeli,pili inaonekana ni wa kulelewa huwezi toa hiyo pesa laki tatu na nusu.
Sawa menu unaweza kupewa lakini wewe huna hizo pesa za kulipa,sasa upewe Menu ya day to day (na siyo day by day) kama wewe ulivyoandika,hata kiingereza cha kitoto kinakushinda.??
Hili zoezi la kupanda mlima sio lazima upande na kampuni yangu,tafuta kampuni nyingine utakayokubaliana nayo masharti na vigezo vyako. Katika group zote ninazopeleka mlimani watanzania ni 2% angalia moja kati ya wageni wangu,japokuwa wengine hawapo kwenye video https://www.youtube.com/watch?v=a8rPnJI0GVM
Kama huu ni wizi na utapeli peleka kesi polisi.!

Huu ndio wizi jamvini na utapeli! Acha kabisa bwana mdogo! Watu hawanunui tu siku hizi package bila mchanganuo, tena usiache kuweka na menu day by day from breakfast lunch and dinner. Acha kutaka kupata hela kivivu 350k inatakiwa uifanyie kazi si kutumia jamvi bure na kupata hela kizembe. Na ukiainisha hivi vyote ndivyo nitawapatia habari wafanyakazi wenzangu hapa Silicon Valley kuja kula hard time mlimani. Sawa!

Hii utauza zaidi na kila mtu atauona uwazi na kutaka kushiriki zoezi hilo. Hii ndio akili na siyo kuwa too defensive.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom