Kuongeza mke bila taarifa

Kuongeza mke bila taarifa

livewise1

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2019
Posts
837
Reaction score
972
Habari za jioni wakuu!
Kuna mdau tupo nae job juzi alinialika harusini kwake.
Alikuwa anaongeza mke wa pili. Kumbe mke wa kwanza amemwambia na amemruhusu japo kinyongeee...ila waliongea wakayajenga.

Mke mpya baada ya kuolewa jumamosi ya wiki ileee iliyopita amekaa siku 7 bila kujua kuwa yeye ni mke wa pili alijua ni pekeake.

Jamaa alivoona zamu ya kwenda kwa bimkubwa imefika akaona isiwe kesi akayaweka wazi.

Bibie akabidi akubaliane kiunyonge ila leo kawapa taarifa wanafamilia wake.
Balaa ndipo limeanzia hapo kumbe muoaji na mshenga hawakusema bayana...wanafamilia wamempigia mshenga aende na bibie amemwambia mumewe aende kwake japo zamu ni kwa bimkubwa.

Sasa jamaa anajiuliza wakwe wata react vipi na wakati bibie alionesha kukubaliana na hali ila baada ya kutoa taarifa inaonekana amejazwa upepo.

Tupo nae kijiweni anajiuliza aende hom kwa bimdogo au akaushe kwa bimkubwa! ???

Hivi hili jambo limekaaje kwa wanaoruhusiwa kuongeza mke na ikatokea hawatoi taarifa kama hivi?!

Haiwezi kumfanya mke mdogo apoteze imani kwa mumewe kwa kuona anafichwa mambo flani?!?!


Wakwe hawawezi kuhisi wamedharaulika?!?

Kwa kisa hiki namie naomba kuelimika wakuu.

Nawakilisha!
 
Back
Top Bottom