Kuondolewa Motor Vehicle Licence janga kwa wananchi wa kawaida

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,524
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Licence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

kwani meondolewa
 
Wacha nikaweke oda ya gari yadi kabisa manake mateja watamiminika kwenye mayard ya magari, sasa tunarudi mtindo wa zamani mama ana gari yake mtoto ya kwake, nikivaa suti nyeusi natoka na benz nikivaa jeans natoka na hilux ya blue.
 
Vp naomba Elimu kidogo ,kuhusu hii kitu bima na road license ,kipi kimefutwa ?,je bima huwa nayo inajilimbikiza?
 
Imevunja rekodi kwa kushangiliwa
Waache washangilie bila kujua mashine za kusaga nafaka huko vijijini kwao zinatumia mafuta... hawajui gharama zitaongezeka kwa mitambo/mashine/majenereta zinazotumia mafuta japo haitumii barabara... Na hawajui kama gharama zitaongezeka, mzigo utahamishiwa kwa walaji wa mwisho ambao ni ndugu zao huko.

Labda kama kuna vituo maalum vya mafuta kwa ajili ya mashine/mitambo inayotumia mafuta.
 
Acha iondolewe. Mfano umeenda nje ukakaa huko miaka miwili gari haiko barabarani. Ukirudi unalipia road licence au motor vehicle wakati hujaitumia na penalty juu. Huu ulikuwa ni wizi mkubwa. Hii ni nzuri. Sema kwa upande mmoja yule anaetumia mafuta ya taa au petrol kwa ajili ya generator itakuwa imekula kwake. Ila kwa wenye magari hii ni bombaaa
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
Well,

Unadhani kati ya hiyo fee iliyoondolewa na gharama ya mafuta kuongezeka ipi inazidi ingine...??assume unamiliki gari na unatumia mafuta?? Baada ya hapo ndio unaweza ku draw concl..pia sasa ushuke chini wa wasio na magari ila consider kua nauli za mabasi au vyombo vya moto vina uhusiano na road licence fee..kisha relate na mwananchi wa kawaida kama ulivyotaka.....simply angalia multiplier effect ya mabadiliko ya vyote
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.

Una point, ila point yako ina mashiko kama ukiangalia hicho kipengele kimoja cha bajeti hii. Lakini ukiuchukua hiyo bajeti kwa ujumla utakuta kuna sehemu nyingi Ina wa favour wananchi. Mfano, kuondoa au kupunguza ushuru wa mazao itawasaidia watu wa hali ya chini. Jaribu kuichukua hiyo bajeti kwa ujumla wake ndo utapata logic yake
 
Waache washangilie bila kujua mashine za kusaga nafaka huko vijini kwao zinatumia mafuta... hawajui gharama zitaongezeka kwa mitambo/mashine/majenereta zinazotumia mafuta japo haitumii barabara.

Labda kama kuna vituo maalum vya mafuta kwa ajili ya mashine/mitambo inayotumia mafuta.
Ahsante kwa Uchambuzi Mkuu, wengi wanalichukulia poa.
 
Back
Top Bottom