king Davidson
JF-Expert Member
- Feb 9, 2017
- 252
- 1,063
Mh. Rais yawezekana alikuwa na nia nzuri lakini sidhani kama alifanya utafiti juu ya mapungufu na ubora wa udahili kupitia TCU kwa kutumia CAS (Centrel Admission System). Je anafahamu na anaelewa subabu za viongozi waliopita kuanzisha mfumo huo wa udahili? Duniani kote ambako wameendelea katika sayansi tekinolojia na elimu wanatumia Central Admission System (CAS) mfano Turkey, Canada, United Kingdom, South Africa, Austria, Switzerland, na nyinginezo.
Madhara ya kuondoa Central Admission System (CAS)
+Dual admissions (wanafunzi kudahiliwa mara mbili katika vyuo viwili tofauti ndo maana hata NACTE walipo gundua swala hilo wakaanzisha CAS kwa udahili wa Astashahada na Stashahada.
+Upendeleo na kujuana, kigezo cha kusoma chuo kikuu Tz ni principle pass mbili hivyo basi kutokana nakujuana hiki kinaweza kuwa kigezo cha kuruhusu upendeleo kwa watu wenye ufaulu mdogo kusoma vyuo bora.
+Mianya ya rushwa katika udahili, watoto wa maskini watashindwa kucompete na wakishua katika kuhakikisha wanasoma vyuo bora wanavyovipenda.
+Itachochea ubadhilifu katika utoaji wa mikopo na baadhi ya wanafunzi kupata mikopo mara mbili kutokana Dual admissions.
Angalizo
Maswala yote na maamuzi yanayohusu elimu yasifanyike kisisasa na katika majukwaa ya kisiasa.
Elimu ni utafiti, nguzo pekee ya mabadiliko ya mifumo ya elimu na mifumo mingine inaongozwa na tafiti, na hata sera za elimu zinatungwa kutokana tafiti hazitungwi na kauli mbiu za majukwaani.