Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 44,590
- 36,573
ni muhimu sana kuomba mara nyingi uwezavyo, na kadiri unavyonyimwa zaidi ndivyo karibia zaidi kupewa na unavyokua mzoefu zaidi wa kunyimwa na hatimae kunyimwa kwako linakua ni jambo la kawaida tu.Umewahi kuomba jambo fulani ukanyimwa, ilhali unajua kabisa yule mtu alikuwa nalo ila akaamua tu kutokukupa?
(wengine husema akakaza ,akadinda)
Kuomba aibu no uno
Kunyimwa aibu no two
kutangazwa aibu no 3
Kuomba halafu ukanyimwa ni aibu 🤣🤣
Ni kama umejidhalilisha halafu bado husaidiki
Yaani umejianika, umeweka wazi hitaji lako, lakini mwisho wa siku hupewi ng'oo 🤪
Wewe umewahi kuomba nini ukanyimwa? Na ulijisikiaje?
Mara nyingi muombaji akinyimwa hujuta na kutamani asingethubutu kuomba kabisa lakini ni too late 😁
Lakini pia kuna msemo unasema, Ukinyimwa, unajifunza kutafuta vya kwako ( Wahenga🤔)
Lakini sasa najiuliza...
Hivi kweli kila kitu kinaweza kupatikana bila kuomba? 🤪
Au kuna mambo ambayo bila kuomba huwezi kuyapata kamwe? 🤔
Weekend hiyoooo
NB : Kulombana sio anasa
ShesRise_1 🖐
Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa.
usikate tamaa wala usichoke kuomba 🐒