sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,324
- 2,494
Habari za jumapili wanajamvi,
Hakika kama unaishi na mwanamke kuna raha yake na karaha zake.Nijikite kwenye kero. Mfano mwanamke anataka kila unapokwenda muongozane.
Huu kama ni upendo, utakuwa upendo wa kuongezeana gharama na pia kunyimana pumzi. Yaani muda wote mkae pamoja huku kila asubuhi anataka matumizi ya familia.
Kero namba mbili ni kukushawishi uboreshe maisha ya wazazi wake na jamaa zake kama kwao hawana uwezo na wewe mume una uwezo ila hapendi ndugu zako.
Kero nyingine ni ya kupenda vitu vya gharama na vya kujaza nyumba bure bila maana. Kila siku atashauri vitu vya kununua ila hashauri vya kuuza. Kero kero kero hasa hiyo ya kuongozana kila mahali.
Jumapili njema.