sirluta cdhani km lengo lake ni kupotosha watu. anatupa uzoefu wa changamoto anazoziona katika maisha ya ndoa.
wanawake kwa % kubwa wana kero saaaaana ndani ya ndoa. mi maisha ya ndoa naona ni kama sanaa tu! mbona wengi tu akitoka nje smile kubwa, wkt wa kurudi home anaanza kujiuliza. matokeo yake wengine wanaamua kupiga maji(pombe).
umemaliza binamu yangu....Binamu hata mimi nahisi hivyo... Mke huwa anajitambua na anafahamu majukumu yake na mipaka yake.
Kama mkeo hana hayo basi hajafundwa...
Habari za jumapili wanajamvi,
Hakika kama unaishi na mwanamke kuna raha yake na karaha zake.Nijikite kwenye kero. Mfano mwanamke anataka kila unapokwenda muongozane.
Huu kama ni upendo, utakuwa upendo wa kuongezeana gharama na pia kunyimana pumzi. Yaani muda wote mkae pamoja huku kila asubuhi anataka matumizi ya familia.
Kero namba mbili ni kukushawishi uboreshe maisha ya wazazi wake na jamaa zake kama kwao hawana uwezo na wewe mume una uwezo ila hapendi ndugu zako.
Kero nyingine ni ya kupenda vitu vya gharama na vya kujaza nyumba bure bila maana. Kila siku atashauri vitu vya kununua ila hashauri vya kuuza. Kero kero kero hasa hiyo ya kuongozana kila mahali.
Jumapili njema.
Kama ni kero usioe na ye asioe
kila raha na karaha mnakua mmezianzisha nyinyi wenyewe. Ndio maana unaambiwa usianze kitu ambacho hutaweza kuendelea nacho. Usianze kuomba ruhusa kama baadae utataka kuaga, usianze kujitutumua kutwa unatoka na mkeo, sasa ndio kama hivyo penzi limepungua, unaona kero. usimuonyeshe mwenzio wewe ni ukoo wa SS Bakhressa kumbe ni mkuda Fulani, penzi likipungua unaona kero. muwe waangalifu wakati wa kutongozana, urafiki, uchumba hadi kuoana. Be yourself. Umelikoroga sasa ulinywe, acha kutulilia hapa, kwani yeye angekurupuka tu kutaka kuongozana na wewe kila mahali kama wewe hukumuanzishia au angetaka kununua kila kitu bila wewe kumuonyesha una pesa..??
da asia mi nimependa kauli kuwa "usianze kitu ambacho hutaweza kuendelea nacho" ila kumbuka duniani kuna vitu vingi kama vile shule,biashara, nk