Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni shida

Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni shida

kwangu iko hivi mkuu..
Mimi bana nimekukuta na mtoto unalea pekeako,nimekupenda nikakubeba na mwanao,ukishafika kwangu sitaki tena uniletee habari za baba wa mtoto wala nini,kama anamtaka mwanae mpelekee ww urudi hapa kama wewe na wewe huwezi kuishi bila mwanao nenda usirudi.Sitaki kabisa habari ya kuniambia naenda kumsalimia baba wa mtoto stupid wakati nilikukuta pekeako.

safi sana, msimamo huo tupo pamoja sana!
 
Hatukuwa na makubaliano yoyote

Kwanza pole sana kaka ila usijali sana ndo maisha.
Kuhush ushauri.
Kwanza ulifanya kosa la kutokujua mengi kuhusu huyo mchumba wako.
Anyway,baada ya kugundua ana mtoto ungemkalisha chini na kupanga jinsi mtakavyoishi.
Aiidha kwa kuwa ishatokea kwa sasa.Ni bora kufuata ushauri wake ukaachana naye.Au kukubali kuishi naye na mtoto na ikibidi nawe mtoto wako aje muishi wote.Ila angalizo huyo mchumba wako yuko radhi akuache ww na siyo mtoto wake.
Akili kichwani mwako kazi ya mshauri si kukuchagulia uamuzi bali nimeshauri njia mbili unaweza kutumia moja kati ya hizo hapo juu.
 
Ndo ushapenda kaka , penda na anachokipenda ili nae azidi kukupenda!!
 
Ukipenda boga penda na ua lake, ila kwa ushauri wewe chukua watoto wako na yeye achukue wake then muweke sheria na makubaliano alafu muish mkilea watoto wenu.
 
Hutaki mtoto wa mwenzio wakati we unawatoto wako wa pembeni pia nao wakikataliwa utajisikiaje?binadamu tuna roho mbaya hata wanyama hawapo hivi
 
Asanteni kwa ushauri wenu hatimae imebidi nikibali amlete mtoto tumlee
 
Mimi ni kijana na 28 years nilikutana na binti nilimpenda sana kumbe alikua na mtoto kazaa na mwanaume mwingine na mimi pia nilikua na mtoto wa nje niliona isiwe sababu nikaamua kuishi nae toka 2013.

Nilimkuta akitumia sindano za uzazi wa mpango nikamsihi aache akaacha mpaka leo hajawah pata mimba ilileta ugomvi mpaka ikafikia kuniambia mtoto niliezaa na mwanamke mwingine nimesingiziwa iliniuma sana ila nilihamia Mbeya kikazi niliamua kumsaliti nikaanza mahusiano na msichana mmoja akabeba mimba akajifungua mtoto wa kike.

Imeendelea nikaamua kumwambia ilikua ni mziki tuliendelea tukaenda hospital akaangaliwa docta akasema mirija ya uzazi imeziba nilitumia gharama kweli amepona ila mimba bado sasa mimi mtoto wangu wa kwanza yupo std 1 hatujawahi ishi nae yupo kwa wazazi wake na wake yupo kwa wazazi wake.

Imeibuka leo anataka kumleta mtoto aishi na mimi wakati mimi sipo tayari jamani imekua ni ugomvi anaforce kumleta, kiukweli mimi sipo tayari, kaniambia bora tuachane kuliko asiishi na mwanae.

Naombeni ushauri jamani nifanyeje maana kwanza nimechoka kabisa ushauri pliz

Achaneni..
 
Ushauri ninaokupa ni kuwa wewe ni mpumbavu haujafikia level ya kuitwa mwanaume bali una maumbile ya kiume
 
Pole sana lakini naomba niulize ni kitu gani kinachokufanya usikubali kuishi na huyo mtoto wa mume mwenzio?
nikupe story yangu kwa ufupi,nimeolewa baada ya mwezi naletewa mtoto wa mume ana miezi mitatu yani siku narudi Honeymoon nimeingia saa 12 jioni saa2 usiku naletewa mtoto nilichoambiwa na mzazi wa yule mtoto ni kua Usione raha yakufungua miguu tuu ujue na kulea yule bwana ugomvi ukaanza,nilichofanya nikamwambia mumewangu mchukue mtoto
tutamlea sababu hata nikimkataa bado ni mwanao na tukijaaliwa mtoto huyu atakua dada yao,
nimemlea leo hii nna 5boys na yeye ndio wakike peke yake na she is my princess nampenda ni rafiki yangu na anafanya vizuri shule kuliko hata wanangu,na ananijali ananipenda,sasa kama kweli unampenda mwanamke mtoto sio kikwazo....
Awachukue wote tu, mtoto, mama wa mtoto na baba wa mtoto awalee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom