Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni shida

Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni shida

sio kuishi na mtu mwenye mtoto....inatakiwa upime mtu unayeoa habaribza kulitana na mtu gizani ukamfanya mke bila kumchunguza matunda yake ndo kama hayo...


watu kibao wana watoto na wanaishi kwa amani


au wewe mama wa mwanao anakubugudhi?
 
Kuoa mwanamke mwenye mtoto kuna changamoto mkuu, hapo bado hazijaanza story za kuonana na baba wa mtoto sijui na mambo gani mengine. Unatakiwa kua na moyo mgumu ila kama unampenda sikiliza moyo wako unasemaje,jambo la kuishi na mwanae mkae mzungumze isiwe anataka kukuendesha,uwe na msimamo na uonekane kusimamia unachokisema. Usiogope kufanya maamuzi magumu pale utakapoona ujinga.

Na ipo siku atamleta na baba wa huyo mtoto.
 
Hili swala la kuoana maveterani wawili au veterani mmoja ni gumu sana.... Waswahili hawakukosea kusema...Damu ni nzito kuliko maji na Uchungu wa mwana....................tusaidiane kumalizia.
 
Umefanya vzr sana kuomba ushauri kuomba ushauri ,ushauri wangu ni huu achana na huyo mwanamke ,nenda ukamuoe mmoja kati ya wale uliozaa nao ila vzr zaidi muoe yule wa pili wa mtoto mdogo tofauti na huu ushauri utakuwa ni maumivu kwako
 
Kwahiyo huyo wako ataishi huko kwenu hata lini? Na yule ulomzaa huko mbeya sijui??? Mlikosea tangu awali mlitakiwa kukubaliana mstakabali wenu na wa watoto wenu pia. Kwanza nyie wenyewe mnaonekana mna matatizo, Hata jinsi ya kutatua migogoro yenu ni taabu, hao watoto nawaonea huruma.
 
huu ushauri wa hovyo sana.
mwanamke siku zote anajali ndugu zake tu hajali upande wa pili.
hela unayotoa itatumika kulea mwanaye na wa kwako atanyanyasika.
atasimangwa kuliko kawaida na kuishi kama hana ndugu.

Ni uamuzi mgumu kuoa mwanamke mwenye mtoto!!!
 
Kwahiyo huyo wako ataishi huko kwenu hata lini? Na yule ulomzaa huko mbeya sijui??? Mlikosea tangu awali mlitakiwa kukubaliana mstakabali wenu na wa watoto wenu pia. Kwanza nyie wenyewe mnaonekana mna matatizo, Hata jinsi ya kutatua migogoro yenu ni taabu, hao watoto nawaonea huruma.

Nawe niambiage mapema kama unaye
 
Pole sana lakini naomba niulize ni kitu gani kinachokufanya usikubali kuishi na huyo mtoto wa mume mwenzio?
nikupe story yangu kwa ufupi,nimeolewa baada ya mwezi naletewa mtoto wa mume ana miezi mitatu yani siku narudi Honeymoon nimeingia saa 12 jioni saa2 usiku naletewa mtoto nilichoambiwa na mzazi wa yule mtoto ni kua Usione raha yakufungua miguu tuu ujue na kulea yule bwana ugomvi ukaanza,nilichofanya nikamwambia mumewangu mchukue mtoto
tutamlea sababu hata nikimkataa bado ni mwanao na tukijaaliwa mtoto huyu atakua dada yao,
nimemlea leo hii nna 5boys na yeye ndio wakike peke yake na she is my princess nampenda ni rafiki yangu na anafanya vizuri shule kuliko hata wanangu,na ananijali ananipenda,sasa kama kweli unampenda mwanamke mtoto sio kikwazo....

Hongera ni wachache sana kwa dunia ya leo kufanya ulichokifanya.Mungu akuzidishie baraka.
 
Watu Kma Nyie Sijui Kma Kwel Hata Sadaka Uwa Mnatoa?? Haya Fata Moyo Wkao.
 
Mie mwenyewe siwezi ishi bila mwanangu, alifanya makosa kumtenga mtoto wake.
Mtoto raha yake apate malezi ya mama.

Nyie tu hamuelewani, ingekuwa mnaelewana mngeishi vizuri sababu tayari kila mtu ana mtoto.
 
kamchukue na mwanao, mje mwalee pamoja. muongeza na kengine kamoja tu basi!
 
kwangu iko hivi mkuu..
Mimi bana nimekukuta na mtoto unalea pekeako,nimekupenda nikakubeba na mwanao,ukishafika kwangu sitaki tena uniletee habari za baba wa mtoto wala nini,kama anamtaka mwanae mpelekee ww urudi hapa kama wewe na wewe huwezi kuishi bila mwanao nenda usirudi.Sitaki kabisa habari ya kuniambia naenda kumsalimia baba wa mtoto stupid wakati nilikukuta pekeako.

Acha kulia lia mtu na mzazi mwenzie wanaweza kukutana na kujadili hari ya mtoto wao.
 
Back
Top Bottom