DamianMalle
Member
- Jul 16, 2018
- 56
- 54
Mapwenz
Kwanini mnapenda kusumbua wazazi kwa vitu vidogo na vya kipuuzi kama hivi? Seriously hili nalo ni la kuita wazazi? Wao ndio wameoa?Unasubiri barua ya mwenyekiti wa kijiji hili kuthibitisha kuwa mkeo hakupendi?
Waite wazazi wake na yeye akiwepo wambie ukweli na msimamo wako iwapo hatabadili tabia.
Halafu kuwa mkali hili ijulikane humo ndani mwanaume ni nani.
Kaza sura
Kaza sauti.
Mke amefungua pub bila kunishirikisha na anauza mwenyewe kama bar maid nyumba imewaka moto Sababu mke amekua jeuri na kiburi,so aggressive hakuna unachouliza ukajibiwa kistaarabu. Kila mteja anayeenda pale akiomba namba anapewa tu bila shida yupo bize muda wote ni pub pub na `wateja wake" kama anavyowaita hajali familia wala ndoa tena nyumba,chumba chakulala kimekua km stoo kitanda ndio usiseme hajali na imefikia hatua naambiwa nisifike hata kwenye biashara yake sababu namfukuzia wateja wake.
Tupo kwenye ndoa yakikatoliki mwaka wa 4 sasa na tuna watoto wawili wadogo 4yrs na 2yrs.
Ushauri, nifanye nini?